Ally Muhdin akiwa na Khadija Omar Kopa
Kutoka kushoto Mariamu Luseko, Yusuf, Ruben, Khadija Omar Kopa, Fatah, Abdul, Sigo na Zainab, Muda mfupi baada ya kumpokea Khadija Kopa,  uwanja wa ndege wa London Heathrow.


Na Ally Muhdin LONDON, UK.


Malkia wa mipasho Bi. Khadija Omar Kopa ameingia leo jijini London akitokea Dar es Salaam tayari kwa ajili ya onesho lake litakalofanyika Milton Keynes siku ya Jumamosi 29th October 2011 katika ukumbi wa The Golden Lounge, Unit 35 Baton Rd, Milton Keynes, MK2 3LH.

Akizungumza na mwandishi wa blog ya TZ-ONE ya UK Bw. Ally Muhdin, Malkia wa mipasho aliwaahidi wapenzi wake kuwa atawafurahisha na kuhakikisha wataburudika na nyimbo zake mpya na zile za zamani.

Vilevile kampuni ya African Splash promotions pamoja na Infinity Entertainment wamewaomba wapenzi wote wa Khadija Kopa kujitokeza kwa wingi kwenye ukumbi wa The Golden Lounge, Milton Keynes kwa ajili ya kuweza kumuona mwanamuziki huyo - Malikia wa Mipasho. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...