Moja ya watumishi wa kampuni ya AAICO ambayo ndiyo wamepewa dhamana ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari jijini mbeya akitoa mnyororo kulifunga gari la wachina hao huku mama wa kichina akilia kwa hasira
Mama wa kichina akimtolea maneno makali binti Eliza mkusanya ushuru wa maegesho ya magari huku mchina huyo akiendelea kugoma kuwa hawezi lipa ushuru siku ya jumamosi na jumapili kwani ni siku za mapumziko siyo siku za kukusanya ushuru
Mume wa mama wa kichina akijaribu nae kuwaelewesha wakusanyaji ushuru wa maegesho ya magari kuwa wameshazoea hivyo kutolipa siku ya jumamosi na jumapili kwani ni siku za mapumziko
Mama wa Kichina akiwa amechachamaa na kuelekea katika Jengo la NMB Tawi la Mbalizi Road Mjini Mbeya kuomba msaada kwa Askari Polisi waliokuwepo hapo.Picha na Mbeya Yetu Blog
Huyo mama wa Kichina asilete za kuleta. Huku kwao wala hakuna kubishana na wala hakuna cha jumamosi au jumapili. Inatakiwa zitungwe sheria ndogondogo kali na majiji au manispaa ili wapuuzi kama hao walipe mara mbili na kwenda jela siku nne ili uwepo utii wa sheria. Kama sheria hizo zipo tunaomba zitumike bila kuangalia rangi.
ReplyDeleteIn all fairness in a lot of places in other countries parking is free on the weekends
ReplyDeleteMama wa Kichina yuko sahihi.....Nchii hii ni yetu ila kodi ni nyingi sana
ReplyDeleteNamuunga mkono...hivi lakini kweli hii sera ya ushuru siku za weekend na mapumziko ni sahihi??? mbona naona kama hawa wachina wana point?? maoni yangu jamani naomba ya kwenu maana natarajia kununua ka bajaji ka kwendea ibada na miss my family...
ReplyDeleteNadhani wachina hawa wana haki. Kama Jumamosi si siku ya kukusanya kodi, iwaje watu hawa wakusanye kodi?
ReplyDeleteNakubaliana na Wachina 100%. Ningewaona wana dosari endapo tungekuwa tukishuhudia mabadiliko katika miundombinu yatokanayo na huo ushuru, lakini kwa staili hii wakusanye ushuru siku moja tu ya wiki kama kigezo cha ajira.
ReplyDeleteNadhani kodi siku ya weekend si sahihi. Nchi karibu zote duniani hazitozi kodi siku ya Jumamosi. Halafu hao jamaa naamini kabisa kuwa hiyo pesa ilikuwa inakwenda mifukoni mwao. Hii Tz bwana, ulaji nje nje kila mtu anajua hata waziri anayeshughulikia masuala ya ushuru, hili analijua. Kama anabisha, muulize kodi ngapi ilitozwa leo jumamosi Mbeya? Hakika hana jubu kwa sababu hajatengeneza mfumo wa kudhibiti mapato ya kodi. Watoza kodi wasiibe hapo. Mtuuumeee!
ReplyDeleteInategemea. Kuna sehemu jumamosi wanatoza parking fee na kuna sehemu hawatozi. Uamuzi ni watu wa Mbeya wameweka utaratibu upi. Mdau aliyeko China, hawa wa China bom sana mimi ninao hapa Ukerewe wanajipendekesa sana kwa wakerewe tena wanachukua maneno kwako wanawapelekea wakerewe. Ni watu wanafiki sana tena ningeomba serikali yetu isiwape kila sehemu maana wana agenda za kama wazungu. Angalieni jamani. Wamekuja kujitajirisha kwetu wakajenge kwao!!
ReplyDeleteHuyo mchina sileta mbwe mbwe hapa. Sheria ni msumeno. Hula mbele na nyuma. Kama utaratibu ni kulipa kodi hadi siku za weekends basi na alipe. Masuala ya kubishana nadhani hayatakiwi. Ni masuala ya kisheria zaidi. Kama weekend haitakiwi kulipa kodi basi itabidi sheria zibadilishwe kwanza. Kwa sasa itabidi alipe tu hata kama akipandiah hasira namna gani. Kwanza huku kwao ni wabaguzi acha.
ReplyDeleteWewe mdau wa kwanza kutoa maoni yako, mimi nakushangaa sana.Kwanza si sahihi kutoza ushuru wa maegesho siku zisizo za kazi, halafu pia,hichi hakipo kwenye mada, kwa nini watoleshe watu kodi ya maegesho wakati wao hawajatengeneza hizo parking? wamekuta tayari barabara zimeshajengwa wao wameingilia tu kukusanya hiyo kodi.Wajenge parking kubwa tuone kama watu watakataa kutoa kodi, wao hawaja-invest chochote wanataka kuchukua hela za wananchi bila ya wao kutoka jasho lolote (to invest).Wewe mdau ni MBAGUZI, na wa TZ wengi ni waoga na hawajui hata haki zao na ndiyo maana wamezoea kuonewa, sasa wanapopata watu kama hao wanaojua haki zao ndiyo mapambano yanatokea.Wewe mdau wa kwanza unaishi nchi gani hiyo ambayo hata siku za mapumziko mnalipa kodi za maegesho ya magari.Acha kutudanganya wewe.
ReplyDeleteTatizo hizo parking hazinz hata sign za kuonyesha ni muda gani na siku gani mtu anatakiwa kulipia kama kungekuwa na saini hakuna mabishano
ReplyDeleteHIZO PESA ILIKUWA ZIKUSANYWE KWA AJILI WA BOSS KWANI HATA DAR ES SALAAM HAKUNA KULIPIA PARKING WEEK END, NI KAMA TRAFIC WETU HAPA WANAPANGIWA KITUO CHA KUKUSANYA ETI KWA AJILI YA BOSS MIMI IMENITOKEA NILIPOBISHANA NAE AKANAMBIA NATAKA NIMFUKUZISHE KAZI KWANI PESA YA BOSS HAIJAKAMILIKA NA TATIZO HILO JK ANALIANGALIA TU
ReplyDeleteSasa inamaana hizo Parking hazina vibao vinavyoeleza siku na masaa ya Free? kama ni hivyo mgeni atajuaje? wekeni vibao ili kuepuka migogoro kama hiyo.Mbeba box.
ReplyDeleteWEKA MUDA WA KUPAKI NA SIKU ALAFU MTU ALETE UBISHI, HUYO NILETEE HAPA
ReplyDeletenataka kuwaambia ukweli jumapili sio siku ya kazi, na wanadumia document bandia kuibia watu, hao kama unabisha chukua document kaulize ofisini watasema hawaitambui.
ReplyDelete