Shughuli ya ya kuzika mabaki ya miili ya abiria waliopata ajali walipokuwa wakisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma juzi. Ajali hiyo ilitokea Kibaha,  mkoa wa Pwani, baada ya gurudumu la mbele la basi la Delux kupasuka na kusababisha kudondoka na kuwaka moto na kuteketea kabisa pamoja na  abiria 12 hapo hapo. Mazishi hayo ya pamoja yamefanyika katika makaburi ya eneo liitwalo Air Msaehapo  Kibaha ambako mwaka 1999 ajali ingine  ilitokea sehemu hiyo hiyo. Marehemu imebidi wazikwe pamoja baada ya miili yao kuungua vibaya sana kiashi cha kushindwa kutambulika. 
Picha na mdau Chris Mfinanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. nungu awalaze marehemu wote mahali pema peponi Amina!

    ReplyDelete
  2. Nungu ndoo naomba nielimishwe nilifeli kiswahili

    ReplyDelete
  3. Mimi naomba nielimishwe "ndoo" ndiyo kiswahili gani!

    ReplyDelete
  4. Mungu awalaze mahali pema peponi hao ndugu zetu Watanzania waliopoteza maisha katika ajali hiyo
    na Mungu awajalie tumaini la faraja wale wote waliofiwa na nduu na wapendwa wao katika ajali hiyo,, Kwa kweli nawapa pole sana na msiBa huu ni wetu sote watanzania
    MUNGU ALITOA NA MUNGU AMETWAA JINA LAKE NI KUU LIHIMIDIWE MILELE DAIMA.AMEN!

    ReplyDelete
  5. Wewe wa pili acha hizo..huo mchezo tunauweka kwenye topiki za kawaida siyo masuala ya misiba..Wewe inaonekana siyo Mtanzania..Huyo alitaka kuandika Mungu..Wewe umesoma ulichoandika?Unajidai kukosoa:MUNGU AWALAZE MAHALA PEMA PEPONI.

    David V

    ReplyDelete
  6. Jamani kweli japo tuliumbwa kwa udogo na tutarudi kwa udongo na pia kati ya hao hatujui yupi ni msilamu au mkristo ila kweli kama Rais alitoa rambirambi zilienda wapi hadi watu hawa wazike kwanye najeneza kama hayo yanayoonekana ni mbao na misumari bila hata ya polish wala aina yoyote ya kujua kama ni jeneza kwali mafisadi mpaka kwenye maiti jamani MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WALAFI WA HII NCHI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...