Baadhi ya wageni waalikwa katika mnuso wa kusherehekea mafanikio ya kanda ya Miss Ilala katika kutoa Miss Tanzania ambapo mwaka huu Miss Salha Israel pamoja na washindi wa pili na wa tatu katoka Ilala. Hata hivyo hafla hii iliingia dosari pale waandaaji wa Miss Tanzania kumzuia Miss TZ 2011 Salha Israel asihudhurie kwa sababu ambazo hazikujulikana mara moja, kitendo ambacho kimelaaniwa sana na waandaji wa mnuso huu uliofanyika usiku kuamkia leo hoteli ya JB BELMONT (zamani Paradise City) ndani ya jengo la Benjamin Mkapa Towers mtaa wa Azikiwe jijini Dar 
 Ankal akiwa na Hartman, Kanumba na JB mnusoni
 Muddy Bawazir na Mwenyekiti wa ASET Baraka Msiilwa
 Mwandaaji wa Miss Ilala Jackson Kalikumtima akiwa na mmoja wa washindi wa Miss Ilala wa miaka ya nyuma
 Jackson Kalikumtima akimtambulisha Miss TZ 2011 wa tatu ambaye
 Mwandaaji wa Miss Tabata Freddy Ogot na mwalimu wa warembo wa kitongoji hicho wakisalimia wageni
 Mratibu wa hafla wa JB BELMONT hotel Muddy Bawazir akitoa neno
 Rhumba kali lililoporomoshwa na Kisauji na kundi lake
Ankal akiwa na Baraka Msiilwa, Muddy Bawazir na Mharirir wa Tanzania Daima kaka Absalom Kibanda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Lundenga amechoka, anatakiwa kupumzika! Hivi hatambui kuwa Salha alitoka Ilala? hivi hajui kuwa bila kalikumtima kumtafuta, kumfunda na kumfundisha asingefika kwake? yeye anavuna asichopanda na wale waliopanda anawanyima kuvuna mazao ya jasho lao!!

    ReplyDelete
  2. Mnuso wa nini sasa; au mambo ya chagulaga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...