Mshambuliaji wa Yanga Davies Mwape akifurahia baada ya kumchinja mnyama leo Nesho. Kwa lugha ingine ni kwamba Yanga imeibanjua Simba bao 1-0 katika mpambano wao wa ligi Kuu ya Vodacom
Timu ya Yanga leo imeibuka kidedea kwa kuwachapa mahasimu/watani wao wa jadi Simba bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Nyomi ya Yanga na Simba leo

Picha kwa hisani ya
http://www.shaffihdauda.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Ankal acha uongo bwana, Simba walisema hawatapoteza mechi na ni lazima washinde mechi ya leo. Ina maana unasema Simba ni waongo na hawawezi kusimama kidedea kutetea tenzi zao???

    ReplyDelete
  2. Bado sijaelewa. Hivi ina maana Yanga waliposema sisi Simba ni baiskeli ya miti walikuwa sahihi???

    ReplyDelete
  3. Kishindo cha Manji!

    ReplyDelete
  4. Je, kanuni hii ni sahihi?

    Manji + Papic = Simba kwishnei + Ubingwa.

    ReplyDelete
  5. Saafi sana kwa ushindi dhidi ya Simba na kupata point tatu muhimu ambazo zinapunguza tofauti na kuondoa historia ya mnyama kutofungwa tangu ligi iannze

    YANGA HOYEEEEEEEEEEEEE!

    ReplyDelete
  6. Kaka Michuzi, najua wewe Simba tu! Wacha kubania picha na news. Zikiweke kwenye blogu Wana Yanga tuburudike. :)

    ReplyDelete
  7. Mbona hii habari inaonekana imeripotiwa kishabiki sana,mwandishi wa habari hii anaonekana ni Simba.Jinsi habari ilivyoandikwa utafikiri Simba katoka suluhu na Milambo ya Tabora au Mecco ya Mbeya,kumbe mnyama kafungwa na mtani wake wa jadi Yanga.Ikumbukwe Yanga leo walikuwa wenyeji wa mechi hii,iweje sasa habari inaripotiwa kama Simba alikuwa mwenyeji na katoka suluhu.Jamani tuangalie na kujifunza kutoka vyombo vya kimataifa wanavyoripoti habari za michezo,hata kama mwandishi wa habari ni mshabiki wa timu iliyofungwa wanaelezea ukweli wa kilichotokea uwanjani.

    ReplyDelete
  8. Hongera sana Yanga!! Hizi ni dalili za mwanzo kuelekaea kuutetea ubingwa kwa uhakika.Kila la heri katika mitanange iliyobaki.
    GLK

    ReplyDelete
  9. Mazungumzo kati ya Yanga na Simba kabla na baada ya mechi ni kama ifuatavyo:

    Yanga: Sasa?
    Simba: Kuhuthu nini?
    Yanga: Unajua nini.
    Simba: Mwendhio mi staki ivyo.
    Yanga: Nitakuachia ubingwa.
    Simba: Kama ivyo thawa.

    Baada ya 'ngoma'

    Simba: Uthinisaliti mwendhio, uliniahidi ubingwa kabla hujala.
    Yanga: KWA HERI!
    Simba: Uuuuwiiiiii, nafwaaaaaa, mwendhenu nimetendwa tena, mamaaaa!

    Msamalia mwema: Vipi tena mwana?!
    Simba: Si MANJI...ah ah thio, PAPIC...ah thio, YANGA!
    Yanga (kwa mbaali): KWA HERI!

    ReplyDelete
  10. Watasema tumebahatisha Nani anaongoza ligi Hakosi la kujitetea Sijui Milioni 5 hata laki 1 Moja watawapa vijana wao YANGA JUU.

    ReplyDelete
  11. Jamani Michuzi, tupo Ughaibuni tunaomba picha za kutosha. Na magazeti yalivyokuwa yanampamba mnyama, sasa kageuka kuwa swala. UNgefikiri magazeti ndo yanacheza mpira.Kuna mwandisgi mmoja anaitwa Somoa Ng'itu wa magazeti ya Nipashe na Guardian anapenda kuipaka Yanga sana, aseme tena atakacho.

    ReplyDelete
  12. Duh! yaani watu wamejaa mpirani namna hii? Ina maaana hawa watu hawaogopi al-shabbaaby?

    ReplyDelete
  13. Duh, kama ni Mwape basi itakuwa ni kwa bonge la shuti, jamaa ndio zake. Mapunda alilengwa akazuia kisha akageuka majeruhi ghafla, naamini Kaseja alikwepa kudadadeki. Big up Mwape, ni kuwalenga tu hakuna kupiga pembeni, hata kwenye penati.

    ReplyDelete
  14. Ina maana hao Yanga ndio Al-Shabaab au? Eti Kova?

    ReplyDelete
  15. Mbona Simba hawakukata umeme?

    ReplyDelete
  16. Simba dawa yao ni kuwafunga kipindi cha pili, ukiwafunga kipindi cha kwanza baada y amapumziko hawarudi tena...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...