Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu,  ametembelea taasisi ya Wakala wa Vipimo na Mizani iliyo chini ya Wizara yake ili kuonana na wafanyakazi na kujionea baadhi ya shughuli zao.

Naibu Waziri Nyalandu alipokelewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Bwana Deo Maneno na kupewa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo ambayo imeonesha mafanikio makubwa katika kulinda haki za watumiaji hasa wakulima dhidi ya vipimo batili.

Akizungumza mara baada ya ziara yake, Mh Nyalandu ameitaka taasisi hiyo kuongeza juhudi katika kudhibiti vipimo ili kuhakikiksha kuwa, watumiaji wanapata bidhaa na huduma zinazolingana na thanmani ya fedha wanazotoa.

Ameahidi kuusaidia Wakala huo ili kupata sheria mpya yenye nguvu zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo wakosaji huamriwa kulipa faini ndogo zinazowafanya kuendelea kutumia vipimo batili bila wasiwasi wowote.

“ Kazi yenu ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa, watu wa kada zote wanawategemea katika kupata haki.. Kuanzia wakulima mpaka wanunuzi wa bidhaa za viwandani, wote wanataka vipimo sahihi,pigeni vita kangomba na lumbesa,  shirikianeni na mamlaka nyingine kutimiza wajibu huu, wajengeeni watumishi wenu mazingira bora ya kazi, mtafanikiwa kuliko ilivyo sasa”, amesema Nyalandu. 
  
 Mh Nyalandu akipata maelezo ya kazi za idara hiyo
Mh Nyalandu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa idara hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mhe Naibu Waziri hiyo Idara ya Weights & Measures inatakiwa iwe karibu na wananchi ili haki zao ziweze kupatikana kwa urahisi. Ni kama Polisi tu. Wako wananchi wengi wanadhulumiwa na wafanyabiashara wasio waaminifu wanaowaibia wananchi hususan masuala ya mizani. Utakuta Bucha kuna jiwe la Kg 2 lakini sio chuma mimi nimeliona sehemu za Namanga. Kwanza tunahitaji simu zao ziwe wazi kwa watu wote ili kukabiliana na hali mbaya. Halafu wafanye ukaguzi mara kwa mara sehemu za Kariakoo na Namanga na Kinondoni Bucheries. Ichube

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...