Naibu waziri wa viwanda ,biashara na masoko Bwana Lazaro Nyalandu akisisitiza jambo juu ya msimamo wa Serikali kuwachukulia hatua wafanyabiashara ambao wanajihusisha na vitendo vya ulanguzi wa sukari nchini,Mh Nyalandu ameyasema hayo mapema leo asubuhi alipotombelea studio za Clouds Fm na Clouds TV. Amesema kuwa Serikali itawakamata wafanyabishara hao kwa kuwa tayari wanawafahamu kwa vitendo hivyo vya ulanguzi sambamba na kuweka msako madhubuti wa kuwakamata wale wote wanaosafirisha sukari katika njia za panya. 

Hata hivyo Waziri Nyalandu amewataka wakulima nchini kuongeza kasi  zaidi katika kilimo cha miwa kwa ajili ya kuongeza sukari kwa wingi katika viwanda itakayotosheleza katika mahitaji mbalimbali.
Naibu Waziri , Lazaro Nyalandu akiagana na mtangazaji wa Power Breakfast ya Clouds Fm  Barbara Hassan baada ya kumaliza mahojiano yao.
Naibu waziri wa viwanda na biashara na Masoko Lazaro Nyalandu akiwa ndani ya studio ya Clouds Fm pamoja na muaandaji wa kipindi cha Njia Panda Simon Simalenga  na kulia kabisa ni mtangazaji wa Power Breakfast Gerald Hando
Meneja wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga kushoto akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Lazaro Nyalandu alipotombelea studio za Clouds Fm na Clouds TV asubuhi ya leo. Kulia kwa Mh. Nyalandu ni mwandaaji vipindi Bw. Simon Simalenga, na mwenye tai ni Mhariri Mkuu Msaidizi wa Habari na Matukio Bw. Lazaro Matalange.
Meneja wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga kushoto akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Lazaro Nyalandu alipotombelea studio za Clouds Fm na Clouds TV asubuhi ya leo. Kulia kwa Mh. Nyalandu ni mwandaaji vipindi Bw. Simon Simalenga, na mwenye tai ni Mhariri Mkuu Msaidizi wa Habari na Matukio Bw. Lazaro Matalange.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nilivyokua nafikiria kuhusu Babra, Gerald ni tofauti sana na walivyo... interesting. Keep up a good job

    ReplyDelete
  2. Lazaro Matalange ... sauti yako tu mie hoi....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...