Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi wa Precision Air Bw. Michael Shirima (kulia) akitoa tamko rasmi kuhusiana na mpango wa Uuzaji wa Hisa katika Soko la Awali (IPO) utakaoanza tarehe 7 Oktoba mpaka tarehe 28 mwezi huu. Tamko hilo lilitolewa na Mwenyekiti huyo mapema leo katika Hoteli ya ‘Kilimanjaro’ Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko akifuatiwa na Meneja Uhusiano wa Wateja katika Benki ya Stanbic Bi. Naomi Vincent.


Bodi ya Wakurugenzi wa shirika la ndege la Precision Air Services Plc inapenda kuwataarifu kwamba mpango wetu wa Uuzaji wa Hisa katika Soko la Awali (IPO) na kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE) imepatiwa vibali vyote husika na sasa ipo tayari kwa hatua zinazofuata. 

Kilichoidhinishwa ni ratiba ya matukio ya utaratibu mzima wa mchakato huu: 

  Tarehe ya Ufunguzi wa OfaOktoba 7 2011 ; 0300 asubuhi
  Tarehe ya Kufungwa kwa OfaOktoba 28 2011 ; 1000 jioni
  Kutangazwa kwa matokeo ya OfaNovemba 11 2011
  Kuingiza hisa katika akaunti za CDS, kutoa risiti/cheti za malipo na marejesho ya hundiNovemba 25 2011
  Kuorodheshwa na kuanza biashara    ya kununua na kuuza katika  Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)Desemba 8 2011

Kampuni itatoa jumla ya hisa 58,841,750 kwa ajili ya ununuzi kwa bei ya 475 kwa kila hisa. Huku idadi ya chini ya kuanza kununua hisa ambayo mtu ataruhusiwa kununua itakuwa ni hisa 200. 

Nakala ya waraka wa matarajio ya kampuni ambayo pamoja na mambo mengine, maelezo maalumu ya ufafanuzi na ununuzi wa hisa zinapatikana katika tovuti ya Precision Air www.precisionairtz.com tarehe 4 Oktoba 2011. 
 

Kwa niaba ya Wakurugenzi ya Bodi, utawala na wafanyakazi wote napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wateja wetu kwa mchango wao na ushirikiano yakinifu ulioweza kufanikisha maendeleo na ukuaji wa shirika la ndege hili tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hizo zimekuja wakati sio. hali haioneshi shirika kufanya vyema kibiashara hapo siku za usoni kwani tunatarajia ujio wa nguvu wa atcl, shirika la fly540 nalo limekuwa kiimarika na kuna tetesi azam nae anaanza kuwekeza kwene usafiri wa anga. kazi ni kwenu

    ReplyDelete
  2. Hivi kwanini Watz tunapenda kukatishana tamaa kama mdau wa Oct 05, 07:42:00 AM 2011, watu wanapoamua kuuza hisa maana yake wanataka kukuza mtaji ili waweze kushindana na soko, sasa mtu uanaposema "hizo zimekuja wakati sio"labda ulitaka zije lini?

    ReplyDelete
  3. watanzania ndugu zangu tuache tabia ya kuwa negative all the time ,be positive and you will see the change ,we always give up and and be un supportive or negativity ndio maana atuendelei

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...