Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (mwenye kiremba kulia) akigonganisha glasi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, wakati wa halfa fupi iliyoandaliwa na Uongozi wa Wilaya ya Mvomero.Sherehe hiyo ya kuangwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, ambaye hivi sasa ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Mkoaa wa Tabora, watumishi na wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo na wenzao wa Halmashauri,walijumuika na wageni waalikwa kushiriki halfa hiyo iliyofanyika Oktoba 7, mwaka huu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Nashera iliyopo Mjini Morogoro, miongoni mwa wageni waalikwa alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa , Halima Dendego.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa, akionesha keki aliyopewa zawadi na wafanyakazi wa Wilaya ya Mvomero, Mwassa kabla ya kuteuliwa alikuwa ni Mkuu wa Wilaya hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora akikabidhiwa Mzinga wa Nyuki pamoja na Vifaa vya kulimia asali.
Akina mama wa jamii ya kabila la kimasai wa Kijiji cha Wami Sokoine , Wilaya ya Mvomero, wakivisha taji ,RC Fatma Mwassa, wakati wa hafla ya kuagwa.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa kwenye halfa ya kuangwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, kabla ya uteuzi huo.
Picha ya Pamoja , Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa ( mwenye kilemba),na wafanyakazi wa Wilaya ya Mvomero. Mwassa alikuwa ni Mkuu wa Wilaya hiyo kabla ya kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora hivi Karibuni.Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hii nchi yetu imekuwa ni ya ma-party tu kila kukicha, tena ya gharama. Je tunaweza kujua party kama hizi zinagharimu fedha kiasi gani katika bajeti ya serikali, ambazo ni pesa za walipa kodi?
    Kwa nini tusiwe tunafanya pale inapolazimu tu na tena watu wachache kubana matumizi ya serikali?
    Nchi masikini kama yetu hatuoni wenzetu nchi tajiri wanavyobana matumizi jamani?
    Hivi ni lini mwafrika ataamka usingizini? Je mpaka apigwe rungu la kichwa kwanza kumuamsha?
    Jamani tuamke!!

    ReplyDelete
  2. Utajuaje labda wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero wamechanga pesa na kumfanyia sherehe mpendwa wao.
    Usikurupuke tuu..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...