Kwa wenye kutaka kufuatili mchezo wa Taifa Stars vs Morocco usiku huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. naangalia mechi hii, mimi kama mtanzania nakubali kuwa morroco
    wanacheza vizuri saana kuliko sisi. yaani hapa tunaweza kufungwa hata 4-0.

    ReplyDelete
  2. tanzania imeimprove sasa, tena sana ktk dakika hizi za katikati. inabidi tuwapush saana morroco sasa

    ReplyDelete
  3. Mpira ni mzuri na ni mapumziko sasa tuko sare ya 1-1 na goli letu ni zuri sana

    ReplyDelete
  4. mambo yakoje huko, nashindwa kuona hapa

    ReplyDelete
  5. HuyuNamba 15 wa Tanzania sijui hatakamaanamuelewa kocha, maana mara ya tatu sasa anaua offside trick, Nusra jamaa wafunge mpaka Kaseja kaumia kwa kuwa yeye tu ( no 15)alijisahau nyuma

    ReplyDelete
  6. Haya sasa Moroko washapiga goli la pili kwa njia ya Faulo,mchezaji wetu Namba 15 amecheza Rafu ya k....e kwenye eneo la hatari, huyu jamaa hata sijui kwaniniyupo ktk National Team

    ReplyDelete
  7. gori la taifa stars amefunga nani na kwa mazingira yapi?

    ReplyDelete
  8. he sasa sisi tunacheza nini naona hata kugusa hatugusi maana hata kurusha mpira basi hatupati,tushapigwa 3 hao wachezaji hata kufukuza mpira hawafukuzi,futa timu yote peleka TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR MIAKA IJAYO

    ReplyDelete
  9. Tumedumisha mila na desturi yetu katika soka, na sasa turejee nyumbani tuendelee na ligi yetu.

    ReplyDelete
  10. Natamani siku moja atokee kiongozi mwenye mapenzi ya dhati na soka la Tanzania. Kama ni mimi, viongozi wa TFF wahesabu maumivu ya hali ya juu, ni jela maisha kwa udhalilishaji wa Watanzania miaka nenda miaka rudi.

    ReplyDelete
  11. Endapo huyu Kaseja ni kipa nambari moja Tanzania, hao wengine sijui hata wakoje kwa kweli...

    ReplyDelete
  12. Tunacheza soka utafikiri tunatarajia kugungwa badala ya kucheza kwa kusudio la kupata ushindi. Hebu tujiulize, Moroko wangekuwa ni black mamba (nyoka) na kazi yetu ingekuwa aidha tumuue au tuuwawe sisi, tungepambana kilege lege namna hiyo???

    ReplyDelete
  13. Tushatandikwa 3, na mpira umeisha na hivyo kutupwa nje ya mashindano. Jamaa wanatuzidi sana hawa. Hata hizo tatu mungu anatupenda, sijui kwa vile tuwapole, hata umeme ukatwe 2 wks watu wote kimyaaaaa. Imeniuma sana. dah, sijui hatma ya babu poulsen ni vipi huko bongo.

    ReplyDelete
  14. nini kinaendelea kule morocco?

    ReplyDelete
  15. Mpira umemalizika na Tumepigwa 3-1.Mpira nimeutazama mwanzo mpaka mwisho na huu ndio mtazamo wangu Kiufupi.
    Kiujumla Timu bado ni mbovu kabisa yani tusijipe moyo hata kidogo,

    Tatizo naona wachezaji hawachezi kama timu,iliyo na mbinu za ushindi.
    Wakipata mpira hawajui wafanyaje na mara moja wanapoteza kama sio kubutua.
    Kapteni wetu amepiga soka safi sana yeye pikee ndie niliye muona kama mchezaji aliyetulia na kuelewa afanye nini,Ukiachilia na huyo no 15, sijui huyo super star wetu no 8 aliingia kufanya nini maana salikuwa anataka kufanya mambo kama ya Mesi wakati kiwango duni,na huyo no 9 alikuwa anaukimbiza mpira tu toka alipoingia mpaka mpira unaisha hata kuugusa hakufanikiwa.
    Chamsingi nafikiri Tanzania inabidi sasa kuuanza kuwekeza kwenye Soccer Academy ikiwa ni pamoja na kuwaleta walimu wakutosha, sisi kwa sisi nafikiri tunajazana masifa tu,
    Wenzetu kila timu ina Kama watoto wa miaka 6 yaani U-6 Mpaka U-23 katika kila timu. Lakini sisi tunaishia zengwe tu na kutafuna pesa.
    Sikuweza kuamini kama wale wachezaji ni masuper star wenye majina makubwa Tanzania.
    Bila Soccer Academy za kutosha tutabakia kuwa kichwa cha Mwendawazimu.
    Mdau Vienna.

    ReplyDelete
  16. sisi tukubali kuwa ni "KICHWA CHA MWENDAWAZIMU" Hatutaki kusikia sababu zozote maana tukifungwa kunakuja sababu kibao, Sijui wachezaji walichoka kwa safari, hali ya hewa, refa katuuma, tulipewa chakula kibovu, sijui maandalizi yalikuwa madogo!!!!!!. namalizia" MPIRA SIO LELEMAMA" Hilo tulikubali tukitaka tusitake. na tukitaka tufanye vizuri basi lazima tuwaandae watoto wadogo wenye umri usiopunguwa miaka 7 kuwa hiki ni kikosi cha timu ya taifa cha baadae na wawe wanapata mahitaji yote. mdau Leicester.

    ReplyDelete
  17. Tulizoea kusema kosa la Maximo. Aibu tuliyoipata safari hii haikuwahi kutokea enzi za Maximo.

    ReplyDelete
  18. ndicho tulicho panda,maneno mengi kuliko vitendo.

    ReplyDelete
  19. serikali inatakiwa kuchukua vijana wapatao 20 wenye miaka 12 nawawatafutie scholorship kwenye academics za timu kama becelona na timu zingine kubwa ulaya kwa gharama ya serikali kama walivyotoa scholorship kwa wanafunzi kwenda kusoma nje ya nchi...hadi watakapokuja kufanya hilo ndio tutakuwa na matumaini ya kucheza kwenye michuano mikubwa ya bara letu
    mdau-Moscow Russia

    ReplyDelete
  20. Mtakula biriani halafu mcheze mpira? Biriani haiendani na mpira kabisa kabisa. Chakufanyika hapa ni hao wachezaji waache kula wali na hizo nyama choma waone Njisi wata cheza kabumbu. Biriani inamafuta mengi sana na hizo nyama choma ndo kabsaaaaa. Mdau toka buja

    ReplyDelete
  21. Tanganyika kama kawaida utaendelea kufungwa mpaka kiama haahahahahaha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...