Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(wa sita kutoka kushoto mstari wa pili nyuma) akiwa katika pamoja na Mkuu wa Jumuiya ya Madola Malkia Elizabeth II pamoja na wakuu wengine wa nchi za jumuiya ya Madola wakati wa ufunguzik wa Mkutano wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Perth,Austraslia.(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (watatu kulia mstari wa pili) akimsikiliza Malkia Elizabeth II wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya madola leo mjini Perth nchini Australia.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (watatu kulia mstari wa pili) akiwa na baadhi ya wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya madola wakimsikiliza mtu mwenye asili ya watu wa Australia ( anaeonekana kwenye king'amuzi) akielezea asili ya nchi hiyo leo mjini Perth nchini Australia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya madola.


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete wakikaribishwa na Aaron Verlin (kulia) ambaye ni Meneja wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo Perth Nchini Australia. Malkia Elizabeth II wa Nchini Uingereza ndiye aliyefungua mkutano huo.Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hivi sisi tunafaidika vipi na jumuia ya Madola?Tangu nipo shule ya msingi tunafundishwa Jumuiya ya madola..Faida zake ni zipi hasa kwa nchi kama Tanzania..

    Michuzi team m-publish...msi-publish maoni yangu..lakini Body Guard wa Kiongozi mkuu wa nchi tunaomba serikali imbadilishie mavazi; hayo ymepitwa na wakati(avae suti safi za kiraia)..Rais wetu anaonekana kama vile ameingia madarakani kwa mtutu..

    David V

    ReplyDelete
  2. nimesikia moja ya ajenda zao ni kushinikiza nchi zote duniani kuwatambua mashoga na wasagaji na pia kuondoa sheria zinazokataza ushoga. Tunaomba Tanzania msije mkakubaliana na uchafu kama huo hata kama ni shinikizo la kimataifa. Ushoga/usagaji si utamaduni wetu na imani zetu za dini (wakristo na waisilamu) piz zinakataza ushenzi kama huo.

    ReplyDelete
  3. Jumia ya madola haina tofauti na Vatican Sheria zao ni kuvuruga na kama mdau alivyosema Ushoga u freemasons na hatufaidiki kitu zaidi ya kuwa bado tupo utawala wa kitumwa na ndomana mnapigishwa magoti kupata zile MBE,OBE NK ujinga mtupu VISA zenyewe tunapewa kwa kutapeliwa hakuna uhuru wowote wa jumuiya ya madola. MZ

    ReplyDelete
  4. Anony wa pili naomba nikujibu kama hivi: Njaa zenu ndizo zitakazowafanya mkubali ushoga na usagaji. Hao jamaa wanachofanya nikutumia misaada yao kushinikiza kile wanachofanya kisionekane ni cha kijinga kwa baadhi ya mataifa.

    ReplyDelete
  5. Mdau uliyetaja viza inaonyesha mekuuma sana hiyo. Ukweli jumuia hii imeshapitiwa na wakati na TZ tuachane nayo. Hiyo misaada yao kwanza ni midogo. Ukerewe sasa wanaangalia zaidi EU, Australia na NZ wanaangalia asia, Canada wanaangalia USA na Mexico. Zamani walikuwa wakitutumia kuwalinda na kuwafanyia kazi za kifua. Sasa wameshapata wenzao wa EU, hivyo jumuia hii haina umuhimu tena!!

    ReplyDelete
  6. Hivi freemasonry ni kitu gani hasa? Michuzi, naomba uiweke hii kama mada watu watueleweshe wengi tusiojua maana yake. Mimi huwa nadhani ni dini ya kishetani. Inawezekana nikawa sahihi? Freemasonry ni ukweli halisi duniani ila wengi hatuujui kwa undani. Msaada wadau.

    ReplyDelete
  7. huyo nyuma mwenye migwanda ya jeshi ni nani?

    mbona kila sehemu viongozi wetu lazima wafatane na wanajeshi?

    hivi hakuna nguo aina nyingine wanazoweza kuvaa walinzi wa viongozi wetu isipokuwa ni hayo magwanda?

    aibu kuzama na migwanda kila sehemu

    ReplyDelete
  8. Jamani mmeona picha za wenzetu mpangilio wao? wako so organize hata maua yamewekwa kwa namna nzuri ya kuvutia na si shangalabangala tu huku tukiharakisha kupata hela. I like the way nchi za wenzetu wanavyojipanga sijui viongozi wetu wanaiga nini wakienda. Kiongozi anasema ukweli hadi unajisikia vibaya, na believe me wengine hata dini hawana, hawaendi misikitini au makanisani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...