Kampuni ya African Stars Entertainment imeandaa tamasha kubwa la burudani kwa jili ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Uzinduzi rasmi wa Albamu ya 11 ya Bendi yake ya African Stars "Twanga Pepeta".

Tamasha hilo linataraji kuwahusisha wasanii wa fani mbalimbali za Muziki wa hapa nchini na kutoka nje ya nchi. Fani zitakazohusishwa ni pamoja na Taarab, Muziki wa Kizazi kipya na Muziki wa Dansi na msanii mmoja kutoka Nchini Kenya ambaye bado uongozi wa ASET unaendelea kufanya naye mazungumzo.

Tamasha hilo la uzinduzi linataraji kufanyika katika viwanja vya Leaders Club vilivyopo maeneo ya Kinondoni Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili ya tarehe 06-11-2011 kuanzia saa sita za mchana.

Albamu itakayozinduliwa bado haijapatiwa jina ila nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo ni pamoja na "Mapenzi hayana Kiapo" utunzi wake Saleh Kupaza, "Penzi la Shemeji" utunzi wake Mwinjuma Muumini au Kocha wa Dunia, "Umenivika umasikini" utunzi wake Luizer Mbutu, "Dunia Daraja" utunzi wake Charlz Baba, "Mtoto wa Mwisho" utunzi wake Dogo Rama na nyimbo ya mwisho ni "Kauli" iliyotungwa na Rogart Hegga.

Nyimbo zote zimesharekodiwa katika CD kwenye studio ya Metro chini ya Mtengenezaji Allen Mapigo na nyimbo tatu zinatamba redioni na kwenye stesheni za redio mbalimbali hapa Nchini na nje ya nchi.

Maandalizi ya Tamasha yanaendelea vizuri na katika kufanikisha Tamasha hili, ASET imeandaa ligi ndogo itakayoshirikisha timu 12 ikiwemo Timu ya Twanga Pepeta FC iliyoundwa na wanamuziki na wadau wa karibu wa Bendi.

Uzinduzi wa mwaka huu tumeamua kuuweka tofauti kama zinduzi zilizopita ili kuenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara. Bendi inataraji kuingia kambini wiki moja kabla ya tarehe ya uzinduzi ili kujitayarisha vizuri kwa ajili ya shoo kali.

HASSAN REHANI.
MENEJA ASET.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. HIZO BUTI ZINAVALIWA KIPINDI CHA AUTAM ULAYA,NYIE UKO BONGO MNAZIVAA NA JOTO HILI!!!MICHUZI WEWE UNASAFIRI SANA SAIDIA WENZETU AMBAO HAWAJUI MATUMIZI YA MAVAZI..

    ReplyDelete
  2. mkono huo? au nyie ndio wafuasi wa freeM? vidole kukunja hivyo mnajuwa maana yake au mnaiga?

    ReplyDelete
  3. hizo alama mnaelewa maana yake au mnatuonyeshha tu bila kujua maana,

    ReplyDelete
  4. ama kweli bongo ni nchi ya marekebisho ya kila kitu..tunarekebisha hata fasheni za ulaya..ushauri wangu tu jamani ..prevention is better than cure...hivi hizi buti na hili joto ni athari gani za kiafya atapata mvaaji..jamani enyi wadau wetu wa ile wizara yetu ya uzima tele naomba msaada....

    ReplyDelete
  5. waache watu wafurahi

    ReplyDelete
  6. mi nahis nyie(mlio ughaibuni-na kutukana mlikotoka) mnaowakandia hawa wadada ni wavivu wa kufikiri...hawa ni wasanii na hzo picha walipiga wakati wakiwa studio,sa hilo joto linahusika vp?kama wangekuwa stejin hapo ruksa kulaumu...kuhusu hizo alama:Na nyie vioo vya jamii usifanye ishara ambayo hujui maana yake itakukost na mi nahic hawa wote ni malimbukeni hawafuatilii ulimwengu unaendaje,kutwa na magazet ya udaku,kushinda v pub vya uswahilini mwisho wa cku unaonyesha vitu vya ajab ktk picha mnazopiga...mi nadahi ni wakati muafaka kwenu kuelewa tafsri ya picha hasa ukiwa msanii.

    ReplyDelete
  7. Yaani wabongo bwana, haya mabuti angevaa mtu wa feki (fleva artist) ingeonekana fashion. Bongo shida kweli kweli!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...