Na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar

UONGOZI wa Jimbo la Dole Wilaya ya kati umeandaa harambee itakayofanyika Hoteli ya Bwawai Zanzibar kwa lengo la kuchangisha shillingi millioni 500 ili kujenga Kituo cha Ujasiriamali kitakachotoa elimu kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

Akizungumza na mwandishi wa habari Mbunge wa Jimbo hilo Sylvester Masele amesema kuwa uongozi wa jimbo hilo umeandaa harambee Oktoba 8 ya wiki hii ili kuwasaidia watoto kupata taaluma juu ya mambo mbali mbali.

Mbunge huyo wa Jimbo la Dole amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kuanzisha kituo hicho ili watoto wapate taaluma ambayo itawasaidia katika masuala ya maisha ya baadaye.

Amesema kuwa miongoni mwa mambo ambayo yatapatikana katika kituo hicho ni kuwa watoto hao pamoja na mambo mengine wataweza kusoma study za maisha.

Amesema kuwa kituo hicho ambacho kinakusudiwa kujengwa katika Shehiya Kiyanga kitakuwa na shughuli za kitaaluma ikiwemo masuala ya ufundi seremala, ushonaji, masomo ya komputa, ufundi magari pamoja na masuala ya ujenzi.

Aidha mbali na taaluma hiyo ambayo itapatikana katika kituo hicho kutakuwa na fursa za nyumba kwa Walimu wa kituo hicho,Mabweni kwa ajili ya watoto hao, huduma za afya na maji.

Mbunge huyo amesema kuwa harambee hiyo ambayo itafanyika katika hoteli ya Bwawani inakusudia kuchangisha fedha hizo ili ziweze kusaidia watoto hao yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika jimbo hilo la Dole

Harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika huko Bwawani mjini Zanzibar viongozi mbali mbali wakitaifa wamealikwa kuhudhuria katika tukio hilo la kuchangia kituo cha ujasiriliamali kwa jimbo la dole

Aidha Mbunge huyo aliwataja washiriki wa harambee ambao watakaohudhuria kuwa ni pamoja na wafanyabiashara mbali mbali, wanasiasa, mabalozi waliopo Zanzibar pamoja na taasisi ya mfuko wa jamii ZSSF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. wazo zuri lakini kwa maoni yangu kuna jambo la muhimu sana amabolo wana jimbo la dole tulalihitaji zaidi ya shule ya ujasiriamali kwanza shuli ya namna hiyo tayari ipo katika jimbo la dole ni shule ya jumya ya wazazi maboyo ipo kati eneo la iliyokuwa hospitali ya kifua kikuu ya dole nahisi kilicho baki ni kuwashajihisha wazazi, walezi na wananchi wa jimbo kuelewa kuwa shule ipo na kuwasaidia watoto wapate sifa za kujiunga, kwa wingi, lakini kuna jambo amablo ni pasuwa kichwa sana katika jimbo hili mheshimiwa mbunge nalo ni hospitali jimbo zima la dole kuanzia masingini penye makazi ya mbunge regeza mwendo,maili sita,kiyanga, dole yenyewe,kizimbani,mmdo,mapinduzi,mkanyageni mpaka bumbwi sudi na hata mipaka ya majirani zetu wa jimbo kama ndagaa, mwakaje hakuna zahanati kabisa hospitali ipi ya mission machuwi jimbo lengine au uje mjini na hili jimbo lina watu sihaba wengi mh, mbunge huoni haja ya kuuanza na hospitali kwanza kwakuwa shule ya ujasiri amali ipo tayari jimboni kwako?
    nadhaniutaliona hili na kilishughulikia
    mkaazi wa jimbo la dole

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...