Mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Mary Nathan akipita katika njia ndogo iliyofunguliwa na mwekezaji raia wa kigeni anayemiliki ardhi katika eneo la kitongoji hicho kilichopo Kijiji cha Kipera Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro. Mwekezaji huyo analalamikiwa sana na wakazi wa kijiji hicho kwa kufunga njia na kuvamia mashamba yao. Wakazi hao bado wanalalamika kuwa njia hiyo licha ya kufunguliwa lakini imetengenezwa kama ya kupitisha mifugo kwani ni nyembamba na hairuhusiwi kupitisha gari wala pikipiki jambo ambalo bado ni kero kubwa kwa wakazi hao.
Mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Nuru James akipita katika njia ndogo iliyofunguliwa na mwekezaji raia wa kigeni anayemiliki ardhi katika eneo la kitongoji hicho kilichopo Kijiji cha Kipera Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro. Mwekezaji huyo ambaye analalamikiwa na wakazi wa kijiji hicho kwa kufunga njia na kuvamia mashamba yao.Wakazi hao bado wanalalamika kuwa njia hiyo licha ya kufunguliwa lakini imetengenezwa kama ya kupitisha mifugo kwani ni nyembamba na hairuhusiwi kupitisha gari wala pikipiki jambo ambalo bado ni kero kubwa kwa wakazi hao. (Picha na Mroki Mroki).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. aliye mjanja keshamuuzia mgeni ardhi. mgeni hataki watu wapite kwenye ardhi yake mtamlaumu nani?

    Tatizo ni ufahamu wa matumizi ya ardhi kwetu watanzania na wageni. Sisi tumeshazoea kukata njia popote pale kijijini bila ya kujali tupitapo ni mali ya nani almuradi tutafika twendako, wageni wana mentality zile zile za wanakotoka, ukishakuwa unamiliki ardhi basi ni mali yako na ukiwa hutaki watu wapite basi una haki ya kufanya hivyo. Si hasha hata huko mbele akaanza kukaa na kobole lake kuzuia wapita njia.

    solutio ni kutowauzia ardhi wageni.

    ReplyDelete
  2. hivi kuna sheria ipi? inayo ruhusu mgeni kununua ardhi bongo? wakati watanzania wengi tunaogopa kuruhusiwa uraia pacha kwa watanzania walio nje maana wasije wa israel nao wanyakua ardhi kwa kigezo cha uraia pacha,lakini cha kushangaza hapa wageni wanauziwa ardhi ,nani ? anayewauzia ?

    ReplyDelete
  3. walime njia nyingine tuache tabia ya kulalamika sasa akilima hapo mtapita wapi?

    ReplyDelete
  4. Tatizo la wabongo wanpenda sana shortcut si tu maofisini hata kwenye njia, wanaweza kuacha njia hapa na kubuni kajinjia pale, poleni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...