Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani akifafanua Jambo Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala mara baada ya Kuwasilisha baadhi ya mabadiliko katika Muswada huo yaliyoletwa na Serikali. Kamati hiyo ndiyo inayoshughulikia Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, kabla haujawasilishwa Bungeni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala Mhe. Pindi Chana (Mb) akishauriana Jambo la kikanuni na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Angela Kairuki (Mb), mara baada ya kupokea ufafanuzi wa kutoka kwa Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani (Kulia) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema (hayupo Pichani) ambao waliitwa mbele ya Kamati leo kufafanua baadhi ya vifungu katika muswada wa Mabadiliko ya Katiba.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema akifafanua mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala baadhi ya vifungu vilivyomo katika Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, ambao unashughulikiwa na kamati hiyo kabla haujawasilishwa Bungeni. Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliitwa mbele ya Kamati leo kufafanua baadhi ya vifungu katika muswada huo.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala wakifuatilia maelezo kutoka kwa Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani (Mb) aliyeitwa mbele ya kamati kutoa maelezo kuhusu Maboresho katika Muswada wa Mabadiliko ya katiba. Kamati hiyo ha Bunge iliwaita Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani (Mb) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema kufafanua baadhi ya vifungu katika muswada wa Mabadiliko ya Katiba. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Safi sana..Msikurupuke...tulizeni vichwa vyenu kabisaaa..Weka tofauti za vyama pembeni..Acheni kufikiria Tanzania ya leo tu..Fikirieni na Tanzania ijayo(Wale ambao wako chekechea kwa sasa wale..!!).Hatutaki kubadilisha Katiba mara kwa mara.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    David V

    ReplyDelete
  2. Tafadhali katika mabadiliko ya katiba msisahau kubadilisha yafuatayo:-
    Ubenge wa viti maalumu ufutwe kwani unaliingizia taifa hasara na matumizi yasiyo ya lazima. Hatuhitaji bunge lenye wabunge wengi ambao hawajawahi kuchangia lolote kwa miaka 4. Na hakuna ulazima wa kuwa na wabunge wa kuteuliwa(special seat kwani hawana wanaemwakilisha hapo inaonekana ni kupeana ulaji tu wa pesa za walipa kodi. Naona hili swala lifikiriwe.
    Kingine sifa moja wapo ya kuchagua mbunge kwenye majimbo ni mbunge awe angalau na Diploma ya chuo chochote nchini au nje ya nchi. Wabunge wengi waliopo bungeni ukiangalia elimu yao ni duni na hawajawahi kufanya lolote katika kuongeza elimu inayoendana na mabadiliko ya dunia ya sasa. Tunahitaji wabunge walio wasomi na wenye uwezo wa kufikiri kwa undani sio wasindikizaji tu bungeni, ndo maana unaona miaka 50 ya uhuru tanzania inamabadiliko madogo sana ukilinganisha na nchi za jirani.

    Natumaini haya yatazingatiwa katika mabadiliko ya katiba mpya.
    Asanteni na mnakaribishwa kutoa maoni yenu vilevile watanzania wenzangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...