Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni mstaafu Chiku Galawa akimwagilia mche wa mti mara baada ya kuupanda wakati wa shughuli ya kupanda miti iiiyofanyika katika shule ya sekondari ya ufundi Tanga sambamba na uzinduzi wa michezo ya shimiwi mwaka huu iliyofanyika mwishoni mwa wiki, miti hiyo imepandwa na kampuni ya simu za mkononi Airtel ikishirikiana na kampuni ya Tumbaku TLT. Pichani (Kulia) ni Afisa maziingira wa Airtel Mkama Manyama akifatiwa na mkuu wa wilaya ya Tanga Ibrahim Hassan Hussein, akifatiwa na Afisa shughuli na utekelezaji wa TLT bwana Fridoline Takis, nyuma yao mwenye suti ni mkurugenzi wa Executive Solution Aggrey Marealle
Makamu mwenyekiti wa SHIMIWI bwana Daniel Mwalusamba akipanda mti katika shule ya sekondari ya ufundi Tanga, Kushoto ni Mtaalamu wa Miti wa TLT bwana Hamisi Mbonga akifukia shimo na kulia ni Afisa mazingira wa Airtel Bwana Mkama Manyama akimwagilia mche. miti hiyo imepandwa na kampuni ya simu za mkononi Airtel ikishirikiana na kampuni ya Tumbaku TLT wakati wa uzinduzi wa michezo ya SHIMIWI mwishoni mwa wiki.
Washiriki wa Mashindano ya michezo ya SHIMIWI 2011 wakipanda miti katika shule ya sekondari ya ufundi Tanga wakati wa ufunguzi wa michezo hiyo inayofanyika mwaka huu Mkoani Tanga ambapo kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imedhamini michezo hiyo na kushirikiana na kampuni ya Tumbako Tanzania TLT katika zoezi zima la kupanda miti
AIRTEL TANZANIA NA LEAF TOBACCO ZAPANDA MITI TANGA UZINDUZI WA MICHEZO YA SHIMIWI
· Michezo katika mashindano ya SHIMIWI ni SOKA, NETIBOLI, BAO, KARATA, Kuvuta kamba na DRAFTI
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya Tobaco TLT mwishoni mwa wiki imejumuika na mamia ya wananchi waliohudhuria michezo ya SHIMIWI inayofanyika katika mkoa wa Tanga katika zoezi la kupanda miti katika shule za sekondari za Galanosi na Ufundi Zoezi hili la kupanda miti limefanya katika uzinduzi wa michezo hii inayaofanyika mkoani Tanga kwa muda wa wiki mbili kwa kupanda miti elfu tatu.
Halfa hii imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwamo Mgeni Ramsi mkuu wa mkoa wa Tanga Kanali Mstaafu Chiku Galawa pamoja na mkuu wa wilaya ya Tanga Ibrahim Hassan Hussein ambapo nao walishiriki katika upandaji wa miti hiyo Wakizungumza kwa katika shughuli hii ya upandaji miti, Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni Kanali mstaafu Chiku Galawa aliwashukuru kampuni ya Airtel na TLT kwa kupanda miti mkoani Tanga na kuwashukuru waandaaji wa michezo ya SHIMIWI kwa kuleta michezo hiyo mkoani hapo ambapo kwa muda wa wiki mbili shughuli za biashara zitaongezeka na kuinua pato la wakazi mkoani Tanga. Pia aliwaasa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari hizo kutunza mazingira na kuitunza miti iliyopandwa leo na kuhakikisha inastawi na kukuwa kama inavyotarajiwa.
Afisa mazingira wa Airtel bwana Mkama Manyama alisema “leo tunayo furaha kujumuhika na wenzetu shimiwi pamoja na kampuni ya Tobacco TLT katika zoezi la kupanda miti ambalo linaweka historia ya pekee katika shimiwi mwaka huu wa 2011 hapa mkoani Tanga . Sisi Airtel tunachukua nafasi hii kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira na kutunza rasilimali asili ambazo zitasaidia hadi kizazi kijacho.
Kwa upande wake mwakilishi wa TLT bwana Fridoline Takisi aliongeza kwa kusema Tanzania Leaf Tobacco imekuwa mstari wa mbele katika kupanda miti kwenye mikoa mbalimbali nchini, hadi sasa TLT kwa kushirikiana na wadau wake imepanda jumla ya miti zaidi ya 10,000 katika miji na mikoa mbalimbali nchini, hii ni katika kutimiza dhima yetu ya kutunza na kuhifadhi mazingira Mashindano ya Wizara, idara na mashirika ya umma (SHIMIWI) yameanza rasmi mwishoni mwa wiki hii mkaoni Tanga na yatadumu kwa muda wa wiki mbili mfululizo huku zaidi ya TIMU 42 zikiwa zimethibitisha kushiriki Katibu wa shirikisho hilo, RAMADHAN SULULU amesema”Sasa Mambo SHIMIWI yameiva, Michezo itakayokuwepo katika mashindano haya ni SOKA, NETIBOLI, MCHEZO WA BAO, KUCHEZA KARATA, Kuvuta kamba na DRAFTI.
Tunashukuru kwa post nzuri. Ila kwa masahihisho kidogo idadi ya miti ni zaidi ya 10,000,000 (Ten Million). na Kampuni husika katika upandaji wa miti hii ni Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC).
ReplyDeleteJina la Mwakilishi kwenye Mashindano ya Shimiwi ni Ndugu Fridoline Takis.
Tunatanguliza shukrani.