Mafundi wakimalizia kuweka sawa vimbwete chini ya mti mkuu katika bustani ya Maukumbi makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ionayokaribia kumalizika na kuanza kutumika hivi karibuni katika eneo lile lile ilipo Makumbusho ya Taifa jirani na chuo cha IFM jijini Dar es salaam. Tarehe ya ufunguzi wa kiota hiki cha makumbusho na utamaduni bado kujulikana lakini kazi iliyofanyika hapo si ya kitoto. Pamoja na kuwa na ukumbi wa kisasa wa maonesho ya jukwaani wenye uwezo wa kubeba watazamaji 500 kwa wakati mmoja, pia kutakuwa na studio ya kurekodia muziki, mgahawa wa vyakula vya Kitanzania, ukumbi wa maonesho ya sanaa pamoja na makumbusho
 Eneo la bustani likiwa na jumba la makumbusho la kwanza nchini
 Sehemu ya ukumbi wa m aonesho ya sanaa za jukwaani yenye uwezo wa kubeba watu 500 kwa mpigo
 Jukwaa la kisasa lililosheheni mataa na mapazia pamoja na vipaza sauti vilivyofichika.
 Sehemu ya watapokuwa wanaketi watazamaji
Mlango mkuu kuingilia ukumbi wa maonesho (exhibition hall) ukiangaliana na makumbhsuo ya awali. Fanaka hii imetokana na ushirikiano wa karibu kati ya serikali za Sweden na Tanzania chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt. Paul Msemwa ambaye ameshapewa tuzo ya kutukuka kwa usimamizi mzuri wa mradi huu ulioanza toka mwaka 2003. Architect wa jengo hili, Bi Inger Thede toka Sweden ameweza kufanya maajabu kwa kujenga jengo ambalo halihitaji viyoyozi, ambapo popote utakapokuwa hutopata joto. Hakika ni kazi iliyotukuka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ukweli wa mambo, dr Msemwa ni jembe la ukweli Makumbusho. Waswid wamemkubali ni shujaa wa miradi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...