Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa akikata utepe kuzindua mnara mpya wa mawasliano wa kampuni ya Airtel Tanzania katika kijiji cha Mlola, Lushoto Mkoani Tanga mwishoni mwa wiki. Kushoto kwa kwake ni Mbunge wa Lushoto, Henry Shekifu,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Lucy Msofe na nyuma ya waziri ni Meneja wa Airtel Kanda ya Kaskazini, Steven Akyoo.
Mbunge wa Lushoto, Henry Shekifu (wa pili kushoto) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mnara mpya wa mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania katika kijiji cha Mlola, Lushoto mwishoni mwa wiki.Kulia ni waziri ni Meneja wa Airtel Kanda ya Kaskazini, Steven Akyoo.Kushoto kwake ni Waziri wa Wawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa na Meneja wa Airtel Kanda ya Kaskazini, Steven Akyoo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akisalimiana na Maofisa wa Airtel katika hafla ya uzinduzi rasmi mnara mpya wa mawasliano wa kampuni ya Airtel Tanzania katika kijiji cha Mlola, Lushoto Mkoani Tanga mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja wa Airtel Kanda ya Kaskazini, Steven Akyoo na kulia ni Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo Wilaya ya Lushoto, Walter Changlaw.
Serikali imeyashauri makampuni ya simu za mikononi kuanza kutumia teknolojia ya nishati ya jua katika kuendesha minara yao ya mawasiliano ili kujiepusha na matumizi ya genereta ambayo yana gharama kubwa huku yakiwa na athari katika mazingira.
Waziri wa mawasiliano ,Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema hayo mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Mlola wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakati akizindua mnara wa mawasiliano wa kampuni ya simu za mikononi ya AIRTEL.
Sasa imefika wakati kampuni za simu Tanzania tuanze kutumia nguvu ya nishati ya jua ili kuepuka kutegemea matumizi ya mafuta kwenye majenereta ambayo yanaongeza gharama za uendeshaji wa huduma ya mawasiliano na kukwamisha maendeleo hasa vijijni"
ninaipongeza sana Airtel kwa kufanikisha kuwekeza katika mkoa huu na vijiji vyote hivi hapa Tanga na Tanzania kwa ujumla. Uwepo wangu hapa leo pamoja na viongozi wengine wa serikali kunathibitisha mahusiano mazuri kati ya serikali na wawekezaji wake, pia ni kuwashukuru Airtel na kuwaunga mkono waendelee kutoa huduma bora na nafuu zaidi nchini kote
leo nimekuja kuzindua rasmi mawasiliano haya ya simu za mkononi kupitia kampuni ya simu za mkononi ya Airtel hapa kijiji cha Mlola wilaya ya Lushoto mkoa wa Tanga. Ninawashukuru Airtel Tanzania kwa kujitoa na kujenga mawasiliano haya bora yatakayonufaisha zaidi ya vijiji 26 hapa Lushoto
Nae Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel Bw Stephen Akyoo amesema kampuni hiyo imedhamiria kuboresha mawasiliano ya simu za mikononi na kuongeza kwamba mnara huo uliozinduliwa utaweza kutoa mawasiliano vizuri kwa umbali wa kilometa 60 kutoka mahali ulipo.
Mawasiliano haya yatafaidisha vijiji vifuatavyo:-Lwandai,Ungo,Mazashai,Kilole,Mbelei,Makole,Bombo,Kweulasi,Bwaya,Kwetongo,Mavului,Mdando,Kwekanga,Mshangai,Mziragembei,Kigumbe,BomboKamgoboro,Mategho, Mbwei Mhezi,Malimbwi pamoja na Mlola .
Mnara kama huu unaweza kutoa mawasiliano hata kwa zaidi ya umbali wa Kilometa 60 kutokea hapa mlola hivyo ni imani yetu utasaidia kuinua maisha ya wakazi wa vijiji vyote hivyo.
Vile vile Baadhi ya wananchi wa maeneo hayo akiwemo mbunge wao Mh Henry Shikifu wameipongeza na kuishukuru kampuni ya Airtel kwa kuwaletea mawasiliano ya simu za mkononi na wameongeza kuwa yatawasaidia katika kuboresha hali zao za uchumi huku akitoa angalizo kwa wananchi kuulinda na kuutunza mnara huo ili uweze kuwa chachu ya maendeleo kwao kama ilivyokusudiwa
"Kwanza kipekee naomba niwapongeze Airtel kwa kuboresha mawasiliano ni kweli mawasiliano yalikuwa sio mazuri kwa vijiji hivi lakini leo hii unaweza kuongea na simu ukiwa mahali popote na kufanya shughuli zako za kiuchumi sasa naomba wananchi tuungane kwa pamoja na kuulinda mnara huu ili uweze kutumika kama sehemu ya kitega uchumi chetu sasa kwa kuwa sasa tunaweza hata kufungua biashara za huduma za simu kama vile kuuza vocha na kutumiwa na kupokea fedha" alisema Mh. Heny Shikifu Mbunge wa Mlalo
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikiimarisha na kupanua mawasiliano katika maeneo mbalimbali hapa nchini hasa ya vijijini ikiwa ni jitihada za kutimiza kwa vitendo kauli mbiu yake Uhuru wa kuongea.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...