Baadhi ya Vijana wadogo ambao ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyandira, Tarafa ya Mgeta, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, wakisakata soka kwa kutumia mpira wa ‘chandimu’ kwenye uwanja wenye mawe yakiwemo makubwa na madogo kama walivyokutwa na Kamera Man wa Globu ya Jamii hivi karibuni.

Watoto wengi katika Kijiji hicho wanapenda soka na walipohojiwa walielezea matarajio yao ni kuwa wachezaji wa kulipwa, mmoja wao akisema anataka kuwa kama mchezaji Beki wa timu ya Yanga , Shadrack Nsajigwa na mwingine akiwa na ndoto ya kuwa mchezaji wa timu ya Taifa.

Lakini vijana hawa licha ya kuhusudu soka, wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya mchezo huo kama mipira na kutokuwa na walimu wa kuwajengea uwezo wa kisoka pamoja na hali mbaya ya uwanja wanaoutumia na kwamba wanaeleza kuwa siku zote wanakuwa makini wanapocheza ili wasiangushane chini wakihofia kudondokea kwenye mawe. Picha na John Nditi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Halafu mnaimba kwamba mna ardhi ya kutosha hadi mlitaka kuigawa kwa wageni. Ninaamini Tanzania ikitathmini mahitaji yote ya ardhi kwa watu wake na Taasisi zake na ikaamua kuigawa kulingana na mahitaji hayo, ni dhahiri hakuna kipande cha ardhi kitakachobaki bila matumizi. Matumizi duni ya ardhi ndiyo yanayofanya sehemu zingine zionekani hazitumiki na hivyo kuwapa wageni kishawishi cha kuitaka ardhi hiyo. Ukosefu wa viwanja vya Michezo ni moja ya matokeo mabaya ya matumizi ya ardhi huku wanaoihitaji wapo.

    ReplyDelete
  2. JINSI WANAVYO ONEKANA PICHANI YAELEKEA WANAUJUA!!! DEKSHIA CHENGA MBAKA MTU KENDA DOWN???

    ReplyDelete
  3. Ankal, nimetumia muda mrefu sana kutafakari hizo picha. Thanks Bro, unaruhusu nizi frem kwa ajili ya matumizi binafsi?

    ReplyDelete
  4. Hao ndiyo wachezaji mahiri wataoweza kuhimili sulubu zote za uwanjani.

    Unaona kabumbu linavyosakatwa bila ya kiatu au kwa kiatu che yebo yebo? Utaweza kweli kucontrol mpira kwa kiatu hicho bila ya kuwa makini?

    ReplyDelete
  5. Tuwe wakweli,future ya soccer hakuna hapo...

    ReplyDelete
  6. kweli nakubalina hapo hakuna future ya soka hapo,hebu wadau tufikirieni,tz inawania kuingia katika soccer ladunia ,jee wachezaji tuliona wana proffesional gani ya kuweza kupambana na spain,brazil,england, na nyengngine ?

    Mtoto melavyo ndivyo akuavyo,ni nyema chama cha soka kufungua shule maalum ya socer,kuwafatilia vijana mashuleni ambao wanaonekana na future ya footballer,kuwachukua vijana hao nakuwa training hadi kufukia kima 18 KUWEZA KUINGIA KATIKA timu ya taifa na kuwa na wachezaji wazuri wenye elimu ya mpira sio kubutua tu,Beckam uwengereza alichukuliwa akiwa na umri wa maika kama 12 kama sikosei na kusomea mpira hadi kufuka utajiri alinao na kujenga historia nchini uwengereza

    TUSOME NYAKATI

    ReplyDelete
  7. Huko ndiko tulikotoka wote. Ila jitihada zinahitajika ili kubolesha hali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...