Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo wa soko la Mwanjelwa jijini Mbeya,wakiwemo na watoto waliwa wamefunga barabara huku wakiwa juu ya gari bovu waliloliangusha ili kufunga barabara hiyo kutokana na vurugu zilizokuwa zikiendelea leo za kutokubaliana na amri ya mkoa ya kuwataka waondoke pembezoni mwa soko hilo la Mwanjelwa.
 Yaani ilikuwa ni mtafaruku mtupu jijini Mbeya leo maana wafanyabiashara hao walipambana vikali na askari wa Jeshi la Polisi wa mkoa huo.
 Askari Polisi wakiwa ndani ya gari lao huku wakirusha mabomu ya machozi ili kuwatuliza Wafanyabiashara hao ambao leo walizua vurugu kubwa sana jijini Mbeya.inasadikika kwamba watu kadhaa wamepoteza maisha katika purukushani za vurugu hizo huku wengine wakijeruhiwa vibaya sana.
 Askari Polisi wakiwakamata baadhi ya wafanyabiashara hao ambao walikaidi amri ya jiji na kuanzisha vurugu.
 Moja ya Bango walilokuwa nalo wafanyabiashara hao.
 Moto mkubwa wa Matairi ukiwaka katikati ya barabara maeneo ya Kabwe.
 Kofia ikiwa imeachwa baada ya mwenyewe kukimbia.
 hapa hata supu haikupanda maana vurugu lilikolea.
 Mtaa mweupeeee.... kila mtu kakimbia kivyake kujinusuru.Picha zote na Mdau Deus Mosha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. ndugu zangu bado maandamano na vurugu halisi hazijafika,mimi nasema huo ni mfano tu wa kujua kwamba watanzania si wapole bali Mungu amefumba wasifanye fujo kwa faida ya wachache wanaokesh wakisali.
    serikali,imekithiri kubeba matajri na huku vijana wengi wakizidi kusota.
    Tujifunze kwa kuangalia tulipojikwaa na kuanguka.

    ReplyDelete
  2. Jamani naomba msaada ktk picha ya 3 huyo askari ktk gari mbona anaangalika kama mzungu au macho yangu yanazeeka.

    ReplyDelete
  3. TUMECHOKA TUMECHOKA TUMECHOKA NA VURUGU ZA CHADEMA, MBOWE WAO HUKU YEYE NYERERE HAUKUTAIFISHA BIASHARA ZAO ANACHOCHEA ZA WENGINE, SLAA NAYE MTU MZIMA MAPADRI HAWANA TABIA KAMA YAKE LABDA NDIO MAANA KANISA LILIMSHINDWA, SUGU ASIFIKIRI HIYO NI STUDIO ANACHEZEA MAISHA NA MITAJI YA MASKIN KUSHAWISHI WATU KWA UONGO.
    TUMEWAPA BUNGE KAMA NI WANAUME TOSHA WAKAONYESHE UIMAHIRI WAO HUKO.
    TUMECHOKA TUMECHOKA NA SI HASA ZA CHADEMA TUNATAKA UTULIVU WA KUFANYA KAZI ZETU. WAENDE MAHAKAMANI KAMA HAWARIDHIKI NA MAMBO.

    NJAU MAKUNDI

    ReplyDelete
  4. nshimimana aka dumisaneNovember 11, 2011

    wamachinga wa Mbeya kama NTC vile,

    = = =
    buffalo,
    new york

    ReplyDelete
  5. tujilaumu wenyewe serikali na halimashauli za miji na manispaa kwani tumekuwa tukidekeza wenyewe huwa tunawaona wanapoanza kuvamia lakini huwa tunaona labda tutawabughuzi au wapiga kura wetu hawa kumbe ndio mizizi inajijenga kuanzia hapo na kwa kweli kama watakuwa wapiga kula basi c zaidi ya asilimia 15 sasa wao wanaona wanaonewa lakini wengelitimuliwa mapema raia wote wengelikuwa na utii wa sheria za usafi na mipango miji, dawa kama mmewatimua basi ni kuweka ulinzi wa kuzuia nakumbuka manzese ilikuwa hivyo huko nyuma sijui kwa sasa kama wamerudi tena - mdau richie wa ughaibuni

    ReplyDelete
  6. Rais Kikwete pole bora umalize muda wako upoe wa achie wenye kujifanya wana uchungu na nchi hio watu wame kua hawana adabu kuheshimu Serikali kila mtu sasa anajifanya anajua sheria ya kugombea haki tatizo hivyo vyama vingi nchi yenyewe ndogo vyama vingi uta fikiri vilabu vya mipira wata kukumbuka mpuuzi mmoja ataechukua nchi lazima watu wataipata kukataa ya musa kukubali ya firaun
    MICHUZI TAFADHALI USINI BANIE HII POST as is KIKWETE wape nchi wajeshi watufunze adabu tafadhali mkong'oto tuu hapo una faa Arusha na Mbeya

    ReplyDelete
  7. Huu ni UHUNI

    David V

    ReplyDelete
  8. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kazi imemshinda!

    ReplyDelete
  9. Mkuu wa mkoa kazi imemshinda!

    ReplyDelete
  10. Kampeni za kummaliza Sugu??

    ReplyDelete
  11. hilo bango limeniacha hoi ha ha haaaa watu wana mbinu! "mbeya nchi raisi sugu duh"

    ReplyDelete
  12. Njau Makundi, maandamano hayo si ya Chadema wala hayahusiani lolote na Chadema. Hao ni wamachinga wa Mkoa wa Mbeya wameamua kuandamana na kuandika Sugu ni Raisi wao. Hapo ndipo Serikali yetu inapojiangamiza kila kukicha kwa kuilaumu Chadema kwa kila Jambo na kusahau wananchi ndio wahitaji. Chadema ni Jina la Chama ila wananchi wa Tanzania ndio wanaoandamana na kero wazipatazo. Nchi tayari imefilisika natambua wachache wenu sana ndio mtakuwa au mmelikia hili jambo sasa ninachowashauri fungeni mkanda.

    ReplyDelete
  13. Mdau Njau kaa ufikirie unachokiandika kwanza. Huyo mkuu wa mkoa wa Mbeya alikuwa analeta hizo vurugu na wamachinga tangu alivyokuwa Dar na alipoenda Mwanza mambo yakawa ni yale yale, na vipindi hivyo vyote uongozi wa mikoa ilikuwa chini ya CCM, sasa chadema wamehusika nini kwenye wamachinga na polisi kwenye hili? Ni uongozi wa Kandoro ndio mbovu kutumia mabavu.

    ReplyDelete
  14. SHEIKH ABBAS:::BAMIA NA KABECHI KUUZWA MTAANI SIO ISSUE HATA AMSTERDAM UHOLANZI KULIKOENDELEA NA KWINGINEKO HILI LIPO ISIPOKUWA IZINGATIWE HAYA:

    1.PAWE NA UTARATIBU WA KUFANYWA
    -MFANO MAZINGIRA NA KANUNI VIWEPO, KAMA KIPINDI FULANI SOKO LA KARIAKOO DAR UTARATIBU WA MEZA ZA WAVU NA NAMBA ULIWEKWA,HIVYO KUTOA UHAKIKA WA USAFI NA USIMAMIZI KAMA KUKUSANYA ADA.
    2.HALI YA UCHUMI WACHA MBEYA , AU NCHINI TANZANIA, BALI DUNIA NZIMA NI NGUMU, NA KWENYE JAMII ZILIZOENDELEA WAMEZINGATIA SANA HILI NA KUTOA FURSA ZAIDI KWA WATU WA CHINI HASA (SME) Small Medium Enterprises NA HILI LIMELETA MAFANIKIO SANA NA NI NJIA HATA IMF NA WORLD BANK WANAPENDELEA ILI KUWAKWAMUA WATU KOTOKA KTK UMASIKINI.
    3.USIANGALIE UPANDE MMOJA TU WA MWONGOZO WA BOSI WAKO(SERIKALI), BALI PIA UIANGALIE ILE JAMII UNAYOITAWALA NA HALI HALISI YA KI UCHUMI ILIVYO, HASA KI DUNIA KUNA (GLOBAL ECONOMIC SLUMP NA GLOBAL FINANCIAL CRISIS) AMBAPO ATHARI ZAKE ZINATUFIKIA HATA SISI HUKU TANZANIA.
    4.TAZAMA KTK ENEO LAKO, UNA STASTISTICAL DATA ZA KUTOSHA ZA WAKAZI WAKO, IDADI YA WATU NA RIKA ZAO, UFANISI WA KIUCHUMI NA MZUNGUKO WAKE KWA IDADI YA AJIRA ZILIZOPO ,HIVYO UNAPOONA WATU WANAINGIA UMACHINGA NI SUALA LA KIUCHUMI WEWE UNATAKIWA UTOE MAZINGIRA NA TARATIBU NA SIO KUKWAMISHA KWA MINAJILI YA KUMRIDHISHA MWAJIRI WAKO TU.

    ReplyDelete
  15. Mlioshiba hamjui kama kuna wenye njaa. Wamachinga wana njaa waonesheni chakula kilipo hamtaona fujo zao.

    ReplyDelete
  16. Huo ni mwanzo tu. Mengi tutayaona kama hamtabadili mifumo yenu ya kiuongozi.

    ReplyDelete
  17. ndio kusema muziki wa kina Ras Makunja umeshindwa kuwachezesha machinga wa mbeya ?

    ReplyDelete
  18. Huyo bwana askari mung'avu kwenye picha ya tatu sio mzuka ila ni mnyatulu.

    ReplyDelete
  19. PICHA DHAHIRI ZA WALOFANYA FUJO ZINAONEKA. POLISI WANASUBIRI NINI KUWAKAMATA NA KUWAPELEKA MAHAKAMANI? KAMA WAO NI CHADEMA, WA CCM WANAWAJUA HAO WOTE KWA HAWANA PA KUJIFICHA! SIMPLE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...