Michuzi habari za masiku? Hongera kwa kazi nzuri ya kuliendeleza libeneke.
Leo asubuhi wakati niko njiani nilimsikia redioni Waziri Mkuu Mheshmiwa Mizengo Pinga, akiwahamasisha na kuwaomba watanzania kuupigia kura Mlima Kilimanjaro uwemo katika maajabu 7 ya Dunia!!
Na pia wiki yote hii nimekuwa nikisikia wengi wakihimiza tuupigie kura ‘mlima wetu wenyewe’ eti uwemo uwemo katika maajabu ya dunia!! Ni ajabu sana, hivi ni nani asiyejua kwamba Mlima Kilinjaro ni maajabu ya dunia!!?? Mimi nina tatizo na ninaomba msaada wenzangu wanielimishe maana sielewi mantiki ya kuupigia kura Mlima Kilimanjaro.
Ni ukweli usiopingika na ambao hautabadilika kwamba Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote katika Afrika, sasa hili suala la kuupigia kura litabadilisha nini?
Mlima au kitu kama ni cha kipekee kitabaki kuwa cha kipekee milele na milele, hatuwezi kuubadilisha ukweli huu kwa kura za katika simu zetu za mkononi au mitandao ya kompyuta. Ni muhimu kufahamu kwamba utamaduni wa kumiliki au kuzisikia simu za mkononi na kompyuta na kuvitumia vitu hivi kwa ajili ya kupigia kura mlima ni vitu viwili tofauti kabisa ukilinganisha na utamaduni wa kwa wenzetu wa nje.
Tusikubali kufanya kila wanalotaka wao maana isije ikawa kuna ajenda ya siri ya kutaka kupandisha chati vivutio fulani vya asili vilivyopo katika nchi zao.
Kuna baadhi ya nchi zinafanya juhudi kubwa sana kuwaweka wanyama wengi pamoja katika mazizi ili mazingira yafanane na mbuga zetu za wanyama, hatimaye wasihangaike kuja huku kuangalia wanyama.
Mwenye kujua zaidi atupe elimu. Binafsi sikubalini na hili na sitaweza kuupigia kura Mlima ambao najua kwamba tayari ni maajabu ya dunia.
Mkereketwa Mtanzania
Leo asubuhi wakati niko njiani nilimsikia redioni Waziri Mkuu Mheshmiwa Mizengo Pinga, akiwahamasisha na kuwaomba watanzania kuupigia kura Mlima Kilimanjaro uwemo katika maajabu 7 ya Dunia!!
Na pia wiki yote hii nimekuwa nikisikia wengi wakihimiza tuupigie kura ‘mlima wetu wenyewe’ eti uwemo uwemo katika maajabu ya dunia!! Ni ajabu sana, hivi ni nani asiyejua kwamba Mlima Kilinjaro ni maajabu ya dunia!!?? Mimi nina tatizo na ninaomba msaada wenzangu wanielimishe maana sielewi mantiki ya kuupigia kura Mlima Kilimanjaro.
Ni ukweli usiopingika na ambao hautabadilika kwamba Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote katika Afrika, sasa hili suala la kuupigia kura litabadilisha nini?
Mlima au kitu kama ni cha kipekee kitabaki kuwa cha kipekee milele na milele, hatuwezi kuubadilisha ukweli huu kwa kura za katika simu zetu za mkononi au mitandao ya kompyuta. Ni muhimu kufahamu kwamba utamaduni wa kumiliki au kuzisikia simu za mkononi na kompyuta na kuvitumia vitu hivi kwa ajili ya kupigia kura mlima ni vitu viwili tofauti kabisa ukilinganisha na utamaduni wa kwa wenzetu wa nje.
Tusikubali kufanya kila wanalotaka wao maana isije ikawa kuna ajenda ya siri ya kutaka kupandisha chati vivutio fulani vya asili vilivyopo katika nchi zao.
Kuna baadhi ya nchi zinafanya juhudi kubwa sana kuwaweka wanyama wengi pamoja katika mazizi ili mazingira yafanane na mbuga zetu za wanyama, hatimaye wasihangaike kuja huku kuangalia wanyama.
Mwenye kujua zaidi atupe elimu. Binafsi sikubalini na hili na sitaweza kuupigia kura Mlima ambao najua kwamba tayari ni maajabu ya dunia.
Mkereketwa Mtanzania
Mdau una akili sana ungesoma kidogo ungekua bar made..maana sioni haja ya kupigia kura za "Buu Baa" why?? watu wameanza toka 2009 sisi bado siku 4 ndo tuna motivate watu..Failure Govt
ReplyDeleteAsante Mkereketwa Mtanzania
ReplyDeleteMaantiki ya kuupigia kura Mlima wetu Kilimanjaro ni wazo zuri.Duniani kuna maajabu mengi zaidi ya saba(7).Lengo hapo ni kuutangaza mlima kilimanjaro.Tukiupigia kura na ukawa ktika maaajabu 7 ya dunia itautangaza vizuri na kuzidi kuuweka katika ramani ya dunia hasa katika mambo ya utalii.Kuna faida nyingi sana katika kuupigia kura Mlima Kilimanjaro.Faida moja ni kuwa watalii wengi wa nje wanaamini kuwa mlima kilimanjaro uko Kenya.Kwa kuupigia kura na unakwa kwenye maajabu 7 ya dunia mbali na kuutangaza bali utaonekana kuwa uko Tanzania.
Mdau wa USA
Wewe kama Mtanzania ni muhimu kwako kuupigia kura mlima huu.Sababu kubwa ya kuupigia kura ni kuvutia watalii zaidi ili kuingiza pesa ktk nchi.Wenzetu walio na maajabu ambayo yapo ktk chati kama tunavoutakia mlima wetu,Wanapata wageni wengi kwenda na kuangalia maajabu hayo.Tanzania kuna vingi vya kujivunia lakini tatizo letu ni uongozi tu ndio unarudisha nyuma.Miundo mbinu hakuna ili kuwapa watu ajira na kupokea wageni ambao ni moja ya kujipatia kazi kwa namna moja au nyingine.Lakini ni vizuri kuupigia mlima wetu ili kuutangazia maana kuna nchi nyingine wanajua huu mlima upo Kenya.
ReplyDeleteBiashara matangazo mkereketwa. Upigie tu haikugharimu chochote. Faida zake ni mlima kujulikana zaidi duniani, watalli huenda wakaongezeka na kutuingizia fedha za kigeni zaidi. mantiki hapa sio kama ni maajabu au sio, ni kuutangaza tu mlima wetu ili utunzwe vizuri na kuleta manufaa zaidi,
ReplyDeleteMdau Mohamed
Kusema ukweli hata mimi nina maswali mengi kama ya kwako, hivi hata wakisema kilimanjaro si maajabu ndo mlima utakuwa mfupi! mambo ya ajabu ajabu tu siku hizi haya unashangaa mtu ameshupaliwa apigie kula mlima kilimanjaro ili iweje? vurugu tu za mabepari hizi ngoja tuone mwisho wake wapi
ReplyDeleteNi wachache sana wanaofikiria kama wewe. Mlima kilimanjaro ukiwemo katika maajabu 7 ya kimataifa, kwanza watalii wataongezeka hiyo moja tu... Tatizo lako wewe hujiamini na unaogopa sana unatakiwa upambane hii nchi haiko kwenye ujamaa na ndo maana unashabikia ulimbwende na miziki ya kimagharibi, ndiyo ubepali huo. Sasa unaambiwa kupiga kura kwa mlima unajitia hujui!! Nani kakwambia kila mtu duniani anajua kuwa kilimanjaro ni mlima mrefu afrika? Akili ya ajabu kabisa. Piga kura leo wewe acha utoto.
ReplyDeleteNdugu yangu umesema ukweli pia mimi sishabikii mambo haya je? unapoupigia mlima kilimanjaro kula unatumia ela ya nani kwenye simu yako ni ya kwako au unaupigia bule ujue hii ni biashara wala usishangae wanabadilisha kuwa wanatafuta mshindi atakaye upigia mlima kilimanjaro ndiye mshindi wangapi watakao upigia mlima huu kilimanjaro hii ni biashara
ReplyDeleteYou're a SPOILER - vote kwanza halafu majadiliano baadae. Ukisikia wengine wamechaguliwa utalalama. Kama una objection wasiliana na waandaaji sisi hatuna majibu wa maswali yako
ReplyDeleteKuhuliza sio ujinga, tunavyopigia kura mlima kilimanjaro ni pesa unatumia lkn kama ulifatilia kwa makini kampuni za simu nchi zimetoa hiyo huduma bure kupigia kura mlima kimanjaro, na kingine unapouliza jaribu kufailia na kuangalia internet, maajabu ya duniani kila siku yanaongezeka sasa kama utawakumbusha watu kwa kuweka front page ya kila gazeti,vitabu na internet nani ataujua, sisi wenyewe tulio uku nje tunautangaza lkn aisaidi kama nyie wenyewe wanyumbani amtoi support, mnaendelea kuponda,unafiria kuupigia kura watu wakajua uko wapi lkn wewe ndio wakwanza kulalamikia wakenya wakisema huko kwareo. Watanzania tuchangamke
ReplyDeleteKama hamna majibu ya kutosha mnachojitia kujibu nini!?! Mkubali mkatae, hii ni biashara, kama biashara zingine tu! Kura zimeanza kupigwa leo?!?! walikuwa wapi wanadakia mambo katikati!?! Watanzania tumekuwa wavivu wakufikiri,,,tumebaki kudakia vitu na kuiga tu! acha tuone mwisho wake! Uzushi mtupu!
ReplyDeleteAma kweli wabongo tnakazi wkeli kweli, Duh kama ndio hivi kweli hatutafika popote.
ReplyDeletekUPIGIA KURA NCHI YAKO ETI UNAMAINDI VISENTI UTAKAVYOTUMIA KATIKA SIMU YAKO?
Na pia tuondoe kasumba eti Tanzania au Kilimanjaro inajulikana, si kweli hata kidogo. Mimi ni ulaya miaka zaidi ya kumi sasa, ni vigumu sana kumshawishi mzungu wengi hawaijui Tz NA KILIMANJARO hawajui iko wapi, au wengine watakuambia ni Kenya. Hala mnataka tukae tubweteke, eti tunajulikana? Eboo, tuamke.
Biashara matangazo bwana!!!
Mdau uliyetoa mada hii una akili sana. Huu ni uzalendo zaidi kuliko facts. Mpigie kura kwasababu ni mgogo mwenzetu lakini siyo kwasababu ana sifa kuliko wengine. Nilisikia before ngorongoro ndio maajabu kwasababu animals lives in the crater!
ReplyDeletepiga kula, idiot!
ReplyDeletesipigi kura ng'o, tena naombea usishinde kwenye hayo maajabu 7. wanashindwa kushusha bei za vyakula wanakazania tupigie kura milima, hovyooooooo
ReplyDeleteMtu ambaye hajui mantiki ya Maajabu ya Dunia basi hastahili kusaidiwa. Hata vyovyote atakavyoambiwa hatasikia wala kuelewa. Kwa wenzetu wa dini fulani wangemwita TOMASO. Hakuna haja ya kueleweshana arudi darasani tu ataelewa zaidi.
ReplyDeleteyaani nawachukuia sana watu wenye kufikiria kidogo bila kuangalia mambo kwa undani. Mimi ni mwenyeji wa kilimanjaro japo kwa sasa siishi kilimanjaro lakini kila ninapokwenda ninaona wadogo zetu wanavyofaidika na kazi ya kupeleka watalii mlimani na kuwarudisha (porters) wale akina kaka kwa nguvu walizonazo wangekuwa hawana hiyo ajira wangefanya nini?..... tafakari. Halafu wenzetu wa Kenya wanapenda sana kujishaua mlima uko kwao lakini hii ni fursa pekee Watanzania Tumepata ya kuonyesha ULimwengu Mlima upo kwetu. Kura ni Bure bado unaspoil watu wasipige unataka nini? jaribu kuwa MZALENDO kama kitu haukiafiki si lazima uconvice na wenzio wasifanye. Iache Meli yetu ifike Salama tafadhali maana nakuona unaitoboa ili Tuzame. Tusinagalie maswala ya ufisadi tuangalie hata wadogo zetu, ndugu zetu wenye ajira, mahoteli wanafaidika vipi. Asante
ReplyDeleteFedha ndio maajabu saba ya dunia alio kuwa nazo ni mshindi. sasa kusanya ujitayarishe na uchaguzi ujao.
ReplyDeleteSawa, tumeitikia wito wa ku vote...isipokuwa kama mlima Kilimanjaro utashinda na kuanza kuingiza mapato, tunaombwa pia kushirikishwa ktk kufuatilia mapato hayo!.....Isiwe ni siri ya watu wachache kujua mapato hayo, Ni kawaida sana ktk nchi yetu yenye idadi ya watu 45 milioni maamuzi yanafanywa na watu wasiozidi 100 tu na familia zao.
ReplyDeleteMkereketwa.. hoja yako mhh... the only issue I have ni kwa hii serikali yetu pendwa, hivi kweli leo asubuhi hii kumekucha ndio Waziri Mkuu anasimama na kurekodi sauti yake kuhamasisha hili? walikuwa wapi before? wametangaza mlima Kilimanjaro kuwa nominated into this lini?
ReplyDeletela pili, mkereketwa, inakushinda nini kuupigia kura mkima huu uwe kwenye list ya maajabu 7 ya dunia? tena kampuni za simu zinapigana vikumbo kukurahisishia hili? japo nao wameamua this veeeeery late...SHAME. utakuwa mkereketwa wa kweli kutuma sms japo for your country kwa bure badala ya kuforward a joke to 20 people in your phone book. Hebu jaribu ku browse ujue the benefits of being listed in the 7 natural wonders of the world... you will be surprised majirani zetu watakavyorukia hii opportunity once Kilimanjaro is listed....AJIRA, UTALII AND REVENUE.na kwa taarifa yako, mlima haujawa nominated for being the highest mountain in Africa BUT having a SNOW CAPPED PEAK in the middle of the TROPICS.....Welcome to the world.
kupiga kwa mitandao ya simu za voda na airtel ni bure, tatizo liko wapi....kuna mmoja kasema maajabu ni mengi sasa tunataka yale 7 ya juu zaidi. hii ni kura kama kura nyingine tu, unapompigia rais kura haina maana kuwa yule aliyemaliza muda wake hafai isipokuwa anawapishe na wengine waifanye kazi hiyo ambayo yeye anaweza kuendelea kuifanaya na ndo maana watu wanalalama demokkrasia kila siku..kuachiana madaraka..kuna umuhimu gani wa kubadili kiongozi kama aliyeko anafanya vizuri?...maana yake, pamoja na kuleta mawazo mapya lakini pia atainufaisha familia yake..kwa hiyo maajabu 7 yaliyopita yatabakia kuwa maajabu na haya yatakayochukua nafasi yazinufaisha nchi zao kwa namna moja au nyingine na muda ukifika yatawapisha na wengine..ni rahisi tu kuelewa wala si lazima uwe umemaliza form two...kama hutaki kupiga kura hilo ni suala jingine lakini si kwa vile hujui faida yake..
ReplyDeleteni hayo tu
Naunga mkono kutopigia mlima kilimanjaro kura, mlima huu ni maajabu ya dunia tangu mzungu wa kwanza kuuona alishangaa! akandika kuwa haamini macho yake kuwa kuna mlima wenye barafu karibu na ikweta!!!! sasa leo tunafanya nini?waache hao wenye mawazo duni!!!tujaribu kujipanga kimikakati ilituweze kujitangaza maana chema chajiuza kibaya........
ReplyDeleteDuh..Nimepitia maoni yooote taratibu na nimeyapenda..Pointi muhimi iliyojitokeza sana ni KUUTANGAZA ZAIDI MLIMA kuliko hayo mambo ya maajabu.Nawashukuru sana wadau.Huyu aliuza mantiki ya kuupigia kura mlima(Swali zuri sana)..wengi wamemwelewa,wachache wamemkejeli.Ndiyo Tanzania yetu;
ReplyDeleteDavid V
Yaani sisi watanzania tutaendela kuburuzwa kila siku! Kwa hiyo kama hoja ni kuutangaza Mlima ili uvutie watalii wengi zaidi, sasa kwanini tusitangaze mpaka tusubiri waje watu wa 7Wonders Of The World watuaambie tupige kura?? Kwanini isiwepo kampeni ya kudumu ya uhakika nchi nzima, kwa wanachi wote kwa ajili ya kuutangaza mlima wetu? Tusisubiri watu wa nje watutangazie
ReplyDeleteMimi nafikiri msikae mkafikiri kuwa ni Tanzania pekee ndiyo inatafuta kupigiwa kura mlima wake no, nchi nyingi hata nchi zilizo kwenye dunia ya kwanza nazo zimo kwenye kinyang'anyiro hiki.. sasa hapo kuburuzwa kunatoka wapi jamani au ni kwamba wewe lazima tu uwe na hoja tofauti ili nawe ujulikane upo? Naamini kabisa majirani wanapiga kura za kutosha ili nchi yao ifaidike kwa statement yao ya "COME TO ..... AND SEE THE AFRICA'S HIGHEST MOUNTAIN ONE OF THE NEW 7 WONDERS OF THE WORLD" ohoo sasa hapo sisi tumebakia kupiga soga tuu kwenye mijadala iliyo wazi kabisa.
ReplyDeleteand by the way ndugu zetu walioko huko nje ya nchi wanaelewa ni jinsi gani inakuwa rahisi kwa wale wenye vitu kama hivyo inavyokuwa rahisi.... baada ya hapo mtasema ooho hivi ooh vile hebu tuamke jamani ajira ndio hizi hizi
mdau,una akili japokuwa huyo mdau wa kwanza kaku abuse lkn sina shaka juu ya umakini wako,Hivi tuna hitaji kupiga kura au kuutangaza mlima wetu wenyewe?kura ndio nn!!kuhusu kujulikana kwamba uko kenya ni ujinga wa viongoz wenye dhamana tuu..
ReplyDeletemuumini wa nguvu ya umma...
Mdau naona akili yako ni fupi, ndo ndo maana wahaya wanausemi usemao "ATAKYALA ATI MAE ACHUMA", maana yake ni kwamba mtu yeyoye asiyetembea kwa majirani hudhani kwamba mama yake ndi mpishi bora, kumbe hiyo ni kuwa ndani BOX.
ReplyDeleteMaajabu ya dunia yapo mengi mno. Haijarishi ni ya aina gani ila inategemea limetokeaje kwa uasilia wake. Mfano kuna Amazon South America, Bu Tinah Island United Arab Emirates na mengine mengi. Haya yote yanatokea kwa uasilia wake.
Uajabu wa kilimanjaro sio urefu wa mlima kwani kuna mlima everest ambao ni zaidi ya kilimanjaro, bali ni kuwa na theruji miaka yote, ambayo watu wanajiuliza itakuwaje mlima uko kwenye tropical zone ambako kuna joto sana alafu mlima uwe na barafu mwaka mzima? Hivyo theruji ya kilimanjaro kwenye tropical zone ndo uajabu wenyewe.
Hivyo nashauri watu wasiojua mambo waache kuropoka. Suala hapa ni kupiga kura maana maajabu yako mengi.
Nawasilisha
Mh! mi naona hamna mantiki hapa. mlima mrefu kuliko yote afrika... ndio ni kilimanjaro, CHA AJABU NI KIPI? si ni mlima tu au? ungekuwa unaelea angani kweli tungesema maajabu ya dunia
ReplyDeleteNIMEGUNDUA TATIZO LETU...YAANI BAADHI YA WATANZANIA NI WAZAIFU SANA WA KIMAWAZO NA KIFIKRA....MDAU ALIOTOA MADA HII AMESEMA WAZI ANAHITAJI KUELEWESHWA SAFI SANA NADHANI KUNA WATU HUMU WAMEELEZEA VIZURI NA NATUMAINI UMEELEWA SAWASAWA....UNAJUA MLIMA KILIMANJARO USHINDE USISHINDE HADHI YAKE IKO PALE PALE...CHA KUFAHAMU TU NI KIMOJA TUSIDHANI KUA MT. KILIMANJARO NDIO KIVUTIO PEKEE DUNIANI...VIPO VINGINE VINGI NA PENGINE NI ZAIDI YA HATA HIVI 28 VILIVYOPO KATIKA LIST....NEW7WONDERS NI KAMPUNI KUBWA SANA AMBAYO INAJIENDESHA KIBIASHARA, HIVYO BASI HUWA INAANDAA MICHAKATO KAMA HII NA WASHINDI WATAPATA COVERAGE YA KUTANGAZWA,KUSAIDIWA KUFANYA CONSERVATIONS, NA KUFANYA PROMINENT MOVIE SHOOTINGS...NA DEAL HILO NI LA MAISHA, NI NANI HUMU, AU NI NCHI GANI DUNIANI ISINGEPENDA MTEREMKO HUO??....MFANO MWINGINE NI HAYA MASHINDANO YA MAMISS(MFANO TU) MBONA HUWA MWAPIGA KURA KUMCHAGUA MLIMBWENDE MMOJA TU WA KIPEKEE?? KWA NINI MAJAJI WASINGEMUONA TU NA KUAMUA KUMTUNUKU TAJI?? NA PIA JIULIZE AKISHINDA FAIDA GANI HUPATA???....UZARENDO NI KITU MUHIMU, TATIZO NALOONA HAPA NI WATU KUJIFANYA WAJUAJI WA KUHOJI KILA JAMBO BILA YA KUFANYA RESEARCH...UVIVU WA KUFIKILI NA KU TAFUTA DATA ZA KWELI NI TATIZO PIA.NI BORA UKAKAA KIMYA KULIKO NA KUTOPOTOSHA UMATI
ReplyDeleteWatanzania kweli malimbukeni sijawahi kuona kitu kitokee bila kulumbana kwani mkiupigia kura mlima kilimanjaro kuna ubaya gani..acheni kulumbana hiyo ni faida ya wote usiangalie tu kuingiza pesa kwa serikali hata wewe au ndugu yako anaweza kupata ajira pindi watalii wakianza kuingia wengi...mtaanza kuulizana walikuwa wapi airtel,vodacom..hayo sio mambo ya kuulizana kwa sasa..i wish huu mlima ungekuwa kenya then muone wanavyochangamkia dili...AH! WATANZANIA BWANA
ReplyDeleteUKOLONI WA KIGENI!,UTUMWA MAMBOLEO!, UPUUZI HUU!. ETI UPIGIE KULA NDIO UWE MAAJABA, UPIGE USIPIGE KAMA NI MAAJABU YATENDELEA KUWA MAAJABU KAMA SI MAAJABU YATAENDELEA KUWA SI MAAJABU. SIPO TAYARI KUTUMIKIA KILA IDEA INAYOLETWA NA WAZINGU..SIPI KURA NGOOOO!
ReplyDeleteMTZ HALISI
Lol, hivi jamani bado wapo watu ambao bado wanafikii ndani ya box? Kweli mtu unauliza kwa nini uupigie kura mlima kilimanjaro?
ReplyDeleteWenzetu wakenya walianza kusema mlima huu upo kwao, watalii waliotaka kuja kuuona wanashukia Kenya, halafu wanapelekwa na daladala Tz. Sasa hivi Kenya Airways kwenye vipeperushi vyao ndani ya ndege zao wanasema Mlima Kili upo Tanzania ila you get the best view while in Kenya. Na nakwambia people believe them. I was once (during summer- holiday time in European countries) going to Tanzania with KLM. More than 90% of the people destination was in Kenya. It hurts, to hear from a Tanzanian who is questioning why shouldn't we let this mountain known that it is actually in Tz. This will not only advertise this mountain, but also with all other beautiful things Tanzania have to offer to tourists. Shime Tanzanians AMKA, AMKA.. Other countries spend billions on advertisements like this, you cant even send a free sms?
Mdau kweli unahitaji elimu. Dunia tuliyomo sasa ivi inahitaji mapambano, ukikaa kimya eti najua basi wengine hawajui wafahamishe basi ili waujue, waje na wauone.
ReplyDeleteMimi nilifikiri utasema kwanini ukienda kuvoti kwemye mtandao kwanini unalazimishwa kuvoti maajabu saba, inabadi uvoti kitu hata kama hukijui. this is where i see the problem.
Hivi mna habari kuwa zipo list nyingi sana za wonders of the world, na zinamilikiwa na kampuni tofauti duniani? Nani aliamua kuwa mlima Kilimanjaro ndo kitu cha ajabu kuliko vyote Tanzania na kinafaa kupigiwa kura? Mdau kauliza swali la msingi sana: kama ni wa ajabu kwanini upigiwe kura? Kwanini usishinde tu? hatimaye nani anazihakiki hizi kura? Swali la mwisho: Kama kweli kuna umuhimu (mimi siuoni) kuupigia kura mlima Kilimanjaro, ni uzembe wa hali gani kwamba siku nne kabla ya two-year deadline serikali ndo inahimiza watu kuupigia kura???
ReplyDeleteAcheni wizi wa mchana. Experimental facts haziwi fact kwa kupigiwa kura. Fact ni fact tu hizi sasa ni siasa za Ubepari. Tunataka KATIBA mpyaaaaaaa si vinginevyo. Isomwe mara ya KWANZA
ReplyDelete