Mkurugenzi Mkuu wa Ifakara Health Institute,Salim Abdallah akizungumza na waandishi wa habari juu ya kongamano la kimataifa linalojadili mambo mbalimbali ikiwemo kuboresha hatua za kuwafikishia wananchi dawa za kutibu malaria na udhibiti wa ugonjwa huo kwa kutumia dawa za ALU. Kongamano hilo lilianza leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa mipango ya Utafiti ya Ifakara Health Institute Dkt. Honarati Masanja (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu tafiti mbalimbali zilizofanyika zinazolenga kudhibiti ugonjwa wa malaria katika kongamano la kimataifa linalojadili jinsi ya kudhibiti malaria. Kongamano hilo lilianza leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mhadhiri kutoka Shule inayoshughulikia masula ya Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu ) cha Ghana (School of Public Health – University of Ghana) Profesa Fred Binka.
Mhadhiri kutoka Shule inayoshughulikia masula ya Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu ) cha Ghana (School of Public Health – University of Ghana) Profesa Fred Binka akitoa ufafanuzi kuhusu tafiti mbalimbali zilizofanyika zinazolenga kudhibiti ugonjwa wa malaria katika kongamano la kimataifa linalojadili jinsi ya kudhibiti malaria. Kongamano hilo lilianza leo jijini Dar es salaam. Kulia Mkurugenzi wa mipango ya Utafiti ya Ifakara Health Institute Dkt. Honarati Masanja.Picha na Tiganya Vincent, Dar es salaam.
Watu na majina havipo sawa!!! fanyeni quality assurance kabla ya kurusha
ReplyDeleteMasahihisho; picha ya kwanza anayeongea ni Fred Binka, picha ya tatu ndio Salim Abdulla
ReplyDeleteankali umechanganya maelezo ya picha ya kwanza umeweka picha ya tatu na maelezo ya picha ya tatu umeweka ya kwanza
ReplyDelete4 50yrs still fighting malaria teh teh teh
ReplyDeleteAliyeposti habari hii amechanganya maelezo. Mkurugenzi wa IHI ni huyu ambaye anaonekana kwenye picha ya tatu amesimama na sio yule kwenye picha ya kwanza kama ilivyoelezwa.
ReplyDeleteGeuza maelezo hayo....mkurugenzi ni salim huyo aliesimama picha ya chini hapo
ReplyDelete