Ndugu Michuzi, Habari za leo

mimi ni mfuatiliajai mzuri wa siasa za Tanzania, na haswa katika kipindi hiki cha harakati za kupata katiba mpya.

Katika siku za hivi karibuni, Jeshi la polisi hapa nchini limekuwa likizui shughuli za wanaharakati ikiwa ni pamoja na mikutano,maandanamano na makusanyiko kwa kisingizio cha taarifa za kiintelijensia juu ya uwezekano wa kuwepo kwa mashambulizi kutoka kwa kikundi cha alshabab…….,

Jeshi la polisi wanafanya hivyo kwa kigezo cha “bora kinga kuliko tiba” hivyo kuzuia hata mikutano na makusanyiko ya vyama vya siasa hasa vyama vya upinzani. Lakini Jeshi hilo limesahau kuwa linatumia kodi za watanzania, na ni kwa kigezo cha kuhakikisha usalama kwa wananchi na pia kuhakikisha utawala wa sheria unakuwepo ndio maana watanzania wanakubali kodi zao kutumika kuwalipa mishahara pamoja na kuwanunulia magari ya kifahari kama Land cruiser V8.

Lakini Jeshi hili limekosa uhalali wa kutumia kodi za walipa kodi kwa kile ninachokiita kuamua kwa makusudi kulinda maslahi ya watawala wachache, kwa azma ya kufanikisha kile ambacho wengi hatukijui. Mifano ni mingi sana, lakini michache kama yaliyotokea kule Arusha, na jana walipositisha maandamano yaliyoandaliwa na jukwaa la katiba.

Kwa nini viongozi wa jeshi hilo hawajifunzi kwa yanayotokea katika nchi nyingine…??? Wanachi wakiamua hata nyie polisi mtalazimika kuwaunga mkono, tazameni yanayotokea Misri, Syria, Baharain na Libya. Kazi ya polisi ni kuhakikisha usalama wa raia, hata kama raia huyo ni mwizi, polisi wanatakiwa kumlinda ili utawala wa sheria uendelee kuwepo, na ndio maana polisi wanatakiwa kuhakikisha maandamano na mikutano inafanyika kwa amani na sio kuzuia mikutano hiyo.

Ninashaka na kiapo cha polisi hao, kwani nimepata taarifa kuwa katika kiapo chao wanaapa kukitumiakia na kukilinda chama cha TANU.

Ni Kwa mantiki hiyo hiyo basi, ya vitisho vya alshabab… ninashawishika kulishauri jeshi la polisi kufanya mawasiliano ya mapema na wajumbe na waratibu wa safari ya raisi wa zamani wa Marekani George W Bush, na kuwashauri waahirishe safari yake ya kuja Tanzania kwa sababu wanaweza kushambuliwa na Alshabaab…………………………………!!

Mdau wa blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Anakuja kukagua migodi yake.

    ReplyDelete
  2. Ah, shemegiiiii...!

    ReplyDelete
  3. hawa al shabaab waache zao hizo. kama wao ni wababe sana mbona jeshi la kenya limeingia nchini kwao kwa urahisi. hawana lolote hawa. raisi bush na mkewe wanakaribishwa tanzania kwa mikono yote.

    ReplyDelete
  4. anony 25,03:17:AM 2011 huna maaana na hujui ulitendendalo na unachekelea kwa kile ambacho hukijui.

    ReplyDelete
  5. ndugu yangu hoja yako haina mashiko hata kidogo, hebu jiulize hivi kama siku moja ikifika polisi wakatangaza mgomo ni nini kitatokea? au hao polisi wasingekuwepo je wewe ungefabyaje hizo kazi zako kwa uhuru namna hiyo? basi wakati mwingine kama huna cha kuongea ni bora ukae kimya kuliko kuongea utumbo!!!!!!

    ReplyDelete
  6. Shaabab hawana nini wala nini, hakuna Dini pale, wala Msimamo wa Kisiasa, ndio hao hao Maharamia baharini unafikiri jeuri na pesa ya kuendeshea vita wanapata wapi?,,,angalia watu wao walikabiliwa na njaa utawala ukakataa hata wasipatiwe msaada wa kibinaadam, hivi kweli ndiyo dini inasema hivi?

    ReplyDelete
  7. Hamjamuelewa mtoa hoja. Anataka muone wenyewe jinsi jeshi la polisi linavyokandamiza demokrasia kwa kutoa visingizio vya uongo. Ndio maana amesema je na Bush azuiliwe kuja kwa sababu ya taarifa za kiitelijensia?

    ReplyDelete
  8. Na wewe ulieandika hivi inawezekana ukawa al shabab

    ReplyDelete
  9. its shit!! kuja kwa huyo bush na wengine kama wao, unafikir wanakuja kwa wema hao!? wanayao hao. Mwl. alituaasa afrika tunaweza kujitawala, jaman
    wakolon wapya siku hizi wanawapa hata pesa na mbinu nyingi za kutumia, oohh!! tumekwisha tusipojielewa! , alshabaab hawatutaki sie ila kujipendekez kwetu ndio mtihan wetu! haya polis tanzania handle bwana mkubwa, tupa ngedere nyeusi, hatari sana kwa kizazi chetu haya mambo jamani, maana uzalendo ziro.
    mdau japan.

    ReplyDelete
  10. POLISI WANAFANYA HIVO KWA MAELEKEZO YA MABOSI WAO.SASA TUTAANDAMNA KISANYANSI ZAIDI.POPOTE UTAKAPOKUWEPO MKUTANO WA SERIKALI AU KIONGOZI YEYOTE WA NCHI FULANI NASI TUTAENDA NA MABANGO NA MAANDAMANO YETU SI KWA KUWAUNGA MKONO BALI KUFUKISHA KILA UJUMBE TUNAOTAKA UFIKE KWA HAO WAKOLONI MAMBOLEO

    ReplyDelete
  11. Mwandishi wa hii topic sijui kama wachangiaji hapo juu mmemuelewa, Hapa anazungumzia kuhusu Polisi wa Tanzania wanavyozuia maandamano ya wananchi, wanaharakati, chadema, na wengineo wanaotaka kupinga mambo mbalimbali yanayoiharibu nchii hii kiuchumi hususan Rushwana Ufisadi kwa kisingizio cha Al shabaab. Manake kisingizio hicho ka Al shabaab kitumike basi kuzuia Bush asije manake usalama wake utakuwa hatarini.

    Narudi kwako mwandishi wa mada hii, Hawawezi kumzuia Bush kuja manake al shabaab ni kisingizio tu cha kumzuia mtanzania haki yake ya "kuprotest"

    ReplyDelete
  12. Al Shaabab waelewe kuwa Uislamu hauhusiani na maujaji ya watu wasio na hatia wala ukatili wa aina yeyote ile, na si umwamba na Ujambazi!

    ReplyDelete
  13. Al Shabaab, aah jamani Uislamu unasisitiza juhudi na sio kulazimisha mambo na kutokujali kama mnavyofanya ninyi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...