Ndugu Mhariri wa Globu ya Jamii,

naomba uwawekee hoja hii wadau wa Globu ya Jamii ili waweze kutoa maoni yao.

Kwa takribani wiki mbili sasa nimekuwa nikufuatilia vikao vya kamati za Bunge kupitia vyombo vya habari. Kwenye vikao hivyo, mambo mengi yamejiri hadi kunifanya nichanganyikiwe na hivyo kutojua nini cha kufanya. 

 Mathalani, Wabunge wamesikika wakilalamika na kulaani vitendo vya watendaji wa taasisi mbalimbali. Wengine wamefikia hadi kutamka maneno mazito ambayo kwa haraka haraka unaweza kudhani ni ya dhati.

Jumatatu ya tarehe 31 Oktoba, 2011, kamati ya Bunge ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma ilikutana na Uongozi wa Bodi ya Mikopo. Katika kikao hicho, wabunge hao walilalamika kuwa kuna watoto wa vigogo wamepewa mikopo na kuwaacha watoto wa masikini.

 Ninasikitika sana kwa kuwa maneno haya si ya dhati. Wako watoto wa wabunge ninaowafahamu ambao waliweza kupata mikopo nikiwa chuo pale Mlimani. Waliweza kupata mikopo kwa kubadili majina ya wazazi na hata kushinikiza mamlaka husika. 

 Hivi, tunapozungumzia vigogo katika nchi hii ni kina nani? Je wabunge si vigogo? Tumechoshwa na matamko ya kukejeliana.Hiyo ni kejeli kwa kuwa ukweli wa mambo si huo unaotamkwa na waheshimiwa hawa.

Mbunge mmoja wa kanda ya ziwa alisikia akisema eti Bodi hiyo imekiuka sheria katika kufanya kazi kwake. Kinachonisumbua mimi ni je kama hivyo ndivyo anayetunga sheria ni nani? Je Bunge limeshindwa kuhakikisha sheria hiyo inafuatwa, hata kama italazimu kumpiga marufuku Waziri mwenye dhamana ya elimu kutoa maagizo kwa Bodi hiyo?

Ninachokiona mimi ni kiini macho tu. Hii ni mbinu ya kuwafanya wanafunzi waamini kuwa wabunge wana uchungu na matatizo ya wanafunzi. Wanajaribu kuonyesha kuwa wanaguswa na matatizo ya jamii.

Kama Bunge linaona umuhimu wa kushughulikia tatizo la mikopo kwa wanafunzi basi lipange bajeti ya kutosha kwa ajili ya mikopo badala ya kukilaumu chombo ambacho kimsingi hakina uwezo wowote.

Wanafunzi watainuka na kuivaa Bodi pale watakapoona imeshindwa kusambaza pesa ambazo zipo kwa wale wanaostahili. Wanafunzi wengi wamekosa mikopo mwaka huu kwa ufinyu wa bajeti na Bunge letu halioni kuwa hilo ni tatizo kwake.

Selina M.
Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Dada Selina pole sana.Mimi naona hivi mwanafunzi anayepasua Form Six na akawa na sifa za kujiunga na chuo kikuu asomeshwe bure na serikali.kama Libya vile.Mimi nilikuwa kati ya wale wa kwanza kwanza kupata hiyo mikopo 1994..sijawahi kuwalipa hata senti tano;;na sitarajii kuwalipa.Nasikia tunatafutwa!!!

    David V

    ReplyDelete
  2. SISTER TATIZO LA WABUNGE WETU KILE WANACHOKIONGEA SI KILE WANACHOKITENDA. UKIWAANGALIA USONI TU UTAGUNDUA NI WANAFIKI, WANAONGEZA PESA HADI SH 7500 LAKINI WANAOPEWA MIKOPO WANAPUNGUA SI BORA WANGEACHA ILEILE 500 LAKINI WAPATE WATU WENGI MIKOPO, WAO KILA KITU NISIASAA TU, ITAWACOST SIKU 1.

    ReplyDelete
  3. Hata leo hii kamati ilipokuwa TIB ilionekana baadhi ya wajumbe wake walijaa unafiki tu kwani naamini wanazo njia nyingi sana ya kutatua matatizo ya wanachi kuhakikisha mikopo inawanufaisha walengwa badala ya kufanya siasa kwenye masuala ya kitaalamu kama walivyotaka tuamini leo walipokuwa TIB.

    ReplyDelete
  4. Hahahaha wajina wangu hapo juu umenifurahisha sana. Na mie ni kati ya wale wanaodaiwa huo mkopo ila sirudi bongo ngoo sa sijui wataupataje hakyanani..

    ReplyDelete
  5. Tatizo la wabunge ni kutaka kuonekana kuwa wanaongea kwa niaba ya wananchi. Wanashindwa nini kutafuta vyanzo vya fedha vyenye uhakika ili kila mwenye kupata udahili akopeshwe? Vyanzo vyenyewe ni pamoja na kupunguza posho zao.

    ReplyDelete
  6. Kweli bodi ya Mikopo hakuna kitu pale kwani mimi nimeshuhudia uhozo wa uchaguzi wa mwaka huu nikajua hapa bongo bora ufanye ujuacho ili utengeneze maisha lakini ukitegemea serikali itakuvusha unatakiwa uwe na moyo mgumu. Nasema hivyo nikiwa na mfano hai wa mtoto ambaye ni yatima kabisa (yaani hana baba wala mama) amelelewa na wastaafu wa serikali ambao ni jamaa zake na kusoma kwake ilikuwa kwa watu kuchangishana na mtoto amepata majibu mazuri form 6 amechagulia chuo lakini mkopo zero wanasema hakustahili. Sasa hapo unategemea nini ikiwa mwingine amepata div 3 na anawazazi wenye kazi nzuri CHUO KAPATA NA MKOPO KAPATA. Uliyesema bora wapate sh. 500 wengi kuliko 750 wachache!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...