TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea barua ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuomba viongozi wa chama hicho kukutana na Mheshimiwa Rais kuzungumzia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Mheshimiwa Rais Kikwete amelipokea ombi hilo kwa furaha kwa sababu ni jambo jema.

Kufuatia kukubali kwake ombi hilo, Mheshimiwa Rais ameagiza mawasiliano yafanyike ili kupanga tarehe mwafaka ya kukutana na viongozi hao wa CHADEMA na kuzungumzia suala hilo.

IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NOVEMBA 22, 2011
DODOMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. JK ni muungwana sana. Anaharibiwa tu na hao waroho wa madaraka wasiokuwa na "vision". Na hao CUF muwaangalie sana hawana uchungu na Tanganyika. Kwanza wengi wao wanatoka Zanzibar ambao tayari wameshaonesha hawautaki muungano. Sasa haohao mtarajie wawatengenezee katiba nzuri.

    ReplyDelete
  2. Hivi ni CHADEMA tu ndio wana UCHUNGU na nchi hiii? Mbona wabunge wa CCM waliupisha? wanaitakia nini nchi hii? tatizo ubinafsi ndio umewajaa na tunawasubiri watakapokuja kuomba kura tuwahukumu!

    ReplyDelete
  3. Bora hata amekubali kuoanana nao ila tunaomba wakatuwakilishe vyema huko wasirudi kimya kimya... wakumbuke kuwa sisi wananchi ndio tunawatuma maana nilisikiliza Hotuba ya Rais,kuna baadhi ya maneno aliyoyaongea,kama Rais wetu inasikitisha sana!

    ReplyDelete
  4. Asante sana Mheshimiwa Rais kwa uamuzi huo wa busara.weka vijembe,ushabiki wa bungeni pembeni wasikilze kwa umakini na toa uamuzi.Suala la Katiba ni la nchi yetu sote halina itikadi.

    David V

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Jk!huu ndio uungwana bwana jamee wameambiwa na wametii na ukawapa nafasi tena kubwa na pana...Ila kaka huku kitaaa hali ni mbaya saaana.Hata kama hao wakubwa wa dunia wakipata shida nasi tupate?mbona wakila raha si hatupati?sa uhuru uko wapi?miaka 50 ya uhuru fanya hima jembe shilingi iwe stable kulingana na maisha...najua uwezo huo upo...Kipindi hiki ndio cha kudhihirisha upendo na uhitaji wako kwa wabongo...Godbless Jah
    Chotta-mkuranga

    ReplyDelete
  6. hawa chadema tusipokuwa nao makini watanzania tumekwisha...hawana jema hawa ni uroho tu nawaambia

    ReplyDelete
  7. Baadhi ya wabara (watanganyika)mnafurahisha sana eti Wazanzibari hawana uchungu na Tanganyika sasa jiulize wewe binafsi una uchungu na Zanzibar....Usimwage pumba kama huna la kusema

    ReplyDelete
  8. Tunaomba kikao kitumike kwa busara na sio kuonyeshana ujuzi zaidi, ili sote kwa pamoja tuweze kufikia lengo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...