Klabu ya michezo ya Biafra kwa kushirikiana na klabu za michezo za Namanga na Kunduchi Kwanza wanawakaribisha wanamichezo, wadau wa michezo na wananchi kwa ujumla katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira pamoja na kutoa misaada katika hospitali ya Mwananyamala ambayo ni Hospitali ya wilaya ya Kinondoni.
Zoezi hilo la kufanya usafi na kutoa misaada katika hospitali hiyo ni katika kutimiza wajibu wetu kama jamii hasa katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania ambao kilele chake kitakuwa tarehe 9 Disemba, 2011. Kamati teule ya maandalizi ya shughuli hiyo inakaribisha maoni, mapendekezo, ushauri, michango na misaada kutoka kwa watu wote watakaoguswa na dhamira hii kwa kuwasiliana na Katibu wa Biafra Sports Club ndugu Yahya Poli: +255 715 253 653, au tuandikie barua pepe biafra.jsclub@gmail.com
Kauli mbiu ya sherehe za miaka 50 ya uhuru kwa mwaka huu 2011 ni TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNASONGA MBELE! na sisi wanamichezo tunaongezea MICHEZO NI AFYA, MICHEZO USHIRIKIANO, MICHEZO NI UMOJA!
kwa Mawasiliano zaidi:
Biafra Sports Club,
Hse. No. MNY/KMB/639
Isere Street, Kinondoni 'B'
Email: Biafra.jsclub@gmail.com
Blog: www.biafra-jogging.blogspot.com
Phone: +255 715 253 653
P. O. Box 75333,
Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...