Beki wa timu ya Rwanda akiruka juu wakati wa Purupushani za kuokoa mpira, chini ni Beki wa Kilimanjaro Stars, Juma Jabu.katika mchezo huo Rwanda iliifunga timu ya Kilimanjaro Stars bao 1-0.
 Mchezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars,Thomas Ulimwengu akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Rwanda,Gasana Eric katika mchezo wa Tusker Challenge cup uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar jana.Kilimanjaro Stars ililala kwa bao 1-0.
 Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars,Mussa Hassani Mgosi akimiliki Mpira huku mshambuliaji wa Rwanda, Haruna Niyonzima akiunyemelea mpira huo.
 Mshabuliaji wa Kilimanjaro Stars, Thomas Ulimwengu akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Amavubi, Eranzi Jean Claude
 Mbwana Samata akiwatoka walinzi wa timu ya Rwanda
Mashabiki lukuki walifurika kwenye uwanja wa Taifa kuisapoti Kilimanjaro Stars.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. haya je hawa waliokuwa hawanywi urojo vipi......au wameacha kula UGALI siku hizi........hahahahahahaa mdomo mrefu ila vitendo ni zero ila ndio MACHOGO

    ReplyDelete
  2. mdau wa hapo juu nakupa saluti kwani unaambiwa usimcheke mamba kabla hujavuka mto naona wamekula ugali mboga yao urojo

    ReplyDelete
  3. MACHOGO WALA UROJO hakuna sote tunakanyaga tope, hatuna chetu bora tutafute akili mpya...Visiwani mrudi michezo ya, MASHINDANO YA MBIO ZA MAJAHAZI NA MITUMBWI, KUFUKUZA MBUZI na BAO na Bara turudi kwenye KURUSHA MAWE MILIMANI,KUVUTA KAMBA na MANGUMI...kwisha kazi tuache fitna!!!

    ReplyDelete
  4. RAISI amejituma sana tu ktk suala la kuinua michezo akiwa na busara kuwa Duniani sasa michezo sio Burudani bali ni Uwekezaji na Uwezeshaji kiuchumi kwa maana hizi:

    1.Itakuza ajira na kuongeza rasilimali watu.

    2.Itasaidia kuitangaza nchi kiutalii na itapanua mzunguko wa kiuchumi.

    3.Itasaidia kujenga mahusiano ya kimataifa na hazina ya uakisi wa Tanzania miongoni mwa mataifa ya dunia nzima.

    4.Itakuza uwekezaji na kutupatia njia mbadala za kipato mbali na kutegemea sekta ya kilimo cha jembe la mkono huku tabia nchi na mabadadiliko ya hali ya hewa yanaathiri kilimo.

    5.Imedhihirika kuwa hali ya kiuchumi sasa ni mbaya duniani, kila nchi inajitahidi kujikwamua kwa njia mbadala,

    (Mfano Italia imekuwa ktk matatizo ya Ki fedha na kiuchumi na leo wadau wameongelea uwezekano wa uwekezaji kupitia Soka ambapo hisa za soka zitauzwa ili wananchi waweze kuwekeza ktk michezo na kuunusuru uchumi wa nchi yao!).


    Sasa basi, bahati mbaya sana Wadau wahusika watendaji wa shirikisho TFF na Wadau Wahusika Wachezaji wa mpira sio waelewa kwa muono huo hapo juu, mfano TFF ipo na matawi mawili (1.) TFF-Maslahi,(2.) TFF-Malengo, wadau mimi hapo siwezi kufafanua nani yupo wapi wenyewe mtawatambua...sasa kweli tutafika?

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 4 (nne) kutoka juu ukweli umelonga!

    Raisi wetu amejitahidi kujenga uwezeshaji wa kiuchumi kwa vijana na wadau wa soka kupitia maendeleo ya soka!

    ''Yaani piga mpira wa maana upate pesa ,uwe nyota wa Dunia, uwe tajiri, baadae uiwezeshe nchi yetu''

    Uwezeshwaji kiuchumi ni kupitia kuwekewa mipango ya maendeleo ya mpira kama alivyojitahidi Raisi JK na sio kupewa mgao wa fedha!.

    Sasa leo, mpira wenyewe tuna haribu kabisa kama matokeo ya mchezo huu!.

    Raisi JK hawezi kuwa Father Krismasi kwa kuwawezesha wananchi wa Tanzania akiwa anazunguka na magunia ya pesa akigawa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...