Mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Maicrobiolojia ‘’ Master of Applied Microbiology’’ Christer Mwageni ,akitunukiwa kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA) , Al Noor Kassam, Novemba 25,mwaka huu wakati wa mahafali ya 27 ya Chuo hicho.
Mhitimu wa Shahada ya Juu ya Baokemia , Fredy Saguti ,akitunukiwa kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA) , Al Noor Kassam, Novemba 25,mwaka huu wakati wa mahafali ya 27 ya Chuo hicho.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA), Al Noor Kassam ,akiongozwa na baadhi ya Viongozi Waandamizi wa Chuo hicho, akiwemo Makamu wa Mkuu wa Chuo, Profesa Gerald Monela ( wa kwanza kushoto) wakati wa mahafali ya 27 ya Chuo Kikuu hicho yaliyofanyika Novemba 25, mwaka huu.
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Udaktari wa Falsafa ( PhD), wakiimba wimbo wa taifa mara baada ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA), Al Noor Kassam ( hayupo pichani) kuhitimisha sherehe za Mahafali ya 27, ya Chuo hicho, Novemba 25, mwaka huu, ambapo watihumu nane walitunukiwa PhD.
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Misitu, wakiwa katika mahafali ya 27, ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA) mara baada ya kutunukiwa Shahada zao na Mkuu wa Chuo , Al Noor Kassam , Novemba 25, mwaka huu.
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Kilimo wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), wakibadirishana mawazo baada ya kutunukiwa shahada zao, Novemba 25, mwaka huu wakati wa Mahafali ya 27 ya Chuo Kikuu hicho.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...