Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na Rais Julius Nyerere.
Baada ya kutolewa kwake, Bi Titi Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlaani.
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye makaratasi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".
Mnamo tar. 5 Novemba, 2000 Mohammed alifariki dunia kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.
Moja kati ya mabarabara makubwa ya mjini Dar es Salaam yamepewa jina la Bibi Titi Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.
![]() |
Hapa akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. |
historia ya kweli ya nchi yetu imepotoshwa..na huyu bibi titi ni shujaa wa kweli..chuki a nyerere kwa waislam ndizo zilizompelekea bibi huyu kuzushiwa kesi zisizokuwa za kweli..eti alitaka kupnduwa nchi..bibi titi ni mwanamke aliyekuwa shujaa wa kweli..hakuogopa na alikuwa na imani na dini yake...kabla ya uhuru waislam walikuwa wakinyanyaswa na wajerumani kuhusu ma´swala ya elimu..ndiyo chanzo cha wao kutaka uhuru upatikane ili nao wajikombowe kutokana na dhulma walizofanyiwa...baada ya kuupata ikabidi wampe nyerere mambo yao wakitemea hakuwa mdini kutokana na alivyobebwa na waislam mpka kuwa rais..kumbe naye pia alikuwa mdini..waislam waliadhimia kuwa na chuo kikuu kikubwa cha kwanza pale temeke uwanja wa taifa..makubaliano, misada kutoka nchi za kiarabu waislam walipata, ilipotakiwa Nyerere atie saini makubaliano hayo..yeye nyerere kwa huki zake alimuamisha aliyekuwa kinara wa kiislam bwana tewa said tewa kuwa balozi wa nchi ya china ili auwe ile nguvu ya waislam kuhusu kile huo kikuu..ndipo alipoteuliwa Bibi Titi muhamed..kukaimu ule wadhifa..kwa kuwa alikuwa jasiri..alimfuata nyerere na kumwambia kuhusu ahadi zake za kuwasaidia waislam kuhusu mambo ya elimu..na kuhusu kile chuo kikuu...balaa lilianzia hapo...mpaka kupelekewa bibi titi kusingiziwa mambo kibao....ila wenzetu walikuwa wakipewa maeneo makubwa ya makanisa pamoja na mashule ili wajiendeleze...ndio maana leo kanisa wanataka wamwite Nyerere mtakatifu...ukitaka historia ya kweli ya nchi hii hutoipata mashuleni...wafuateni mababu zetu walioko hai..nenda Tabora kuna mzee anaitwa Bilal waikera...na wengineo wapo moshi..hapa dar es salaam utajuwa....
ReplyDeleteSawa mambo ya kukulalamika tu bila vitendo nikazi bule hakuna mtu mtu anaye wazuia kujenga vyuo kujenga mahosptali, vituo vya kusaidia watu wenye shida mara nyingi mnatafuta vingizio imepta miaka miangapi tangu mjitawale mbona wenzenu wakristo wamefanikiwa
ReplyDeleteWewe acha kutudanganya hapa na udini wako.Unajifanya kukemea udini kumbe wewe ndo mdini mkubwa.Kuthibitisha hilo kila ukiona mwislam katajwa mahali unatahamaki.Halfu mtegee udini kuisha Tanzania kama bado tuna watu wa aina yako?Go to hell with your udini....Huna la kutusaidia kama watanzania.
ReplyDeleteNdugu yangu, mimi pia mwiisilamu, lakini nimeonatatizo kwa sisi waisilamu, kwanini hicho chuo kikuu kilitaka kuitwa cha waisilamu?, umewahi kusikia kuna chuo kikuu cha wakristo, hayo mambo yalitakiwa yawe hivii, safuu nzima ya viongozi wa harakati ya kujenga chuo ingekuwa ya wasilsmu lakini chuo kingeitwa tu chuo kikuu na siyo chuo kikuu cha waaisilamu, kusema chuo kikuu cha waisilamu, hiyo ndiyo udini sasa kitu ambacho nyerere alikuwa hapendi, wakristo wangekuwa wabaguzi wa udini Doctor, Jakaya m. Kikwete Rais wetu,asinge soma Seminary ya wakatoriki nikuambie mwuulize hata sasa hivi atakuambia alisoma seminary ya wakatoriki.hapa waaisilamu tufanye yote lakini tusitaje kwamba hiki ni cha waisilamu umeelewa bwana.
ReplyDeleteaksante nadhani umeelewa.
Hii habari njema ya kumkumbuka shujaa wetu Bibi Titi hapa itaishia kwenye malumbano ya kidini kati ya Ukristo na Uislamu ambayo vyanzo vyake ni habari za mitaani. Watanzania tuweke kando mijadala ya Ukristo vs Uislamu sababu hii mijadala haina tija yoyote na kwingine walipokumbatia aina hii ya mijadala wameishia kwenye kumwaga damu.
ReplyDeleteSawa wewe uliyetoa hoja hapo mwanzo ina maana historia ya kweli ya Tanzania unaifahamu wewe tu na hizo source zako mbili tatu? WAKATI HUO TANZANIA KULIKUWA NA SHERIA NA POLICY YA KUWA NA VYUO VIKUU BINAFSI NA VYA KIDINI? AU KWA MANENO MENGINE, WAKRISTO WALIKUWA NA CHUO KIKUU CHA KIKRISTO? Inaonekana kama wewe ni mdini tu na mtu wa majungu lakini hoja zako si za msingi
ReplyDeleteHizi rekodi nyingine hazutusaidii katika karne ya sasa hi au ijayo. Kuna mambo mengi ya maendeleo ambayo watanzania tunatakiwa kuyafikiria na kuyafanyia kazi badala ya kuanzisha chuki za kidini. Kama ni rekodi/historia za waislamu kunyimwa elimu tunaomba utupatie majina ya watanzania waliofukuzwa shule au chuo kikuu hapa nchini kwa sababu ya kuwa waislamu.
ReplyDeleteRest in peace mamaa, daima tutakukumbuka kwa ushujaa wako.
ReplyDeleteACHENI UPUUZI WENU; DINI MNAIJUA? WAISLAAM WAKO NCHI ZA KIARABU, NA WAKRISTU WAKO HUKO KWA WAZUNGU HUKO ULAYA NA MAREKANI. HAMUONI AIBU TANGU LINI MTU MWEUSI ALIKUWA MUISLAM NA TANGU LINI MTU MWEUSI ALIKUWA MKRISTU? EMBU ACHENI UPUUZI WENU HUO, NDIO MAANA TUTATAWALIWA KILA SIKU YA MAISHA YETU NA AKILI ZETU FÌNYO ZA KIAFRIKA!HATUENDELEI NI MARUMBANO TU KILA SIKU WAKATI WENZETU WANAENDELEA MBELE, SISI TUTAFIKA LINI HUKO NA UDINI WETU HATA HATUJUI KESHO NINI CHA KULA MNALETA UBISHI WA DINI. WOTE MMECHANGANYIKIWA ; TUPIGANE NA MAEBDELEO, AJIRA ZA VIJANA, AFYA, UMEME, BARABARA, ELIMU . HAKUNA MTUME ALIEKUWA MWEUSI KATIKA HISTORY ZA DINI ZOTE. ZAIDI YA KUWA MTUMWA!
ReplyDeleteAMKENI WAAFRIKA1 WENZETU WAKO BIZE KUTATUA GOGORO LA UCHUMI DUNIANI NINYI MNAAMKA NA UBISHI DINI , HAYA KULENI HAYO MABISHANO YENU KAMA NDIO YATAWARUDISHA MITUME
NDIO MAANA SASA WAZUNGU WANATUONA HATUNA AKILI, MPAKA WANAANZA KUTUWEKEA SHERIA ZA USHOGA NA ZITAFUTWA TU KWANI TUNAWATEGEMEA WAO KAMA WALIVYOKUJA KUTANGAZA DINI AFRIKA. NA WATAFANIKIWA TU KWANI SISI HATUNA LA KUPINGA KWANI KILA KITU BADO TUNAWATUMAINIA WAO NDIO WATUSAIDIE KWA MAWAZO NA KILA KITU KTK MAISHA YETU TA KILA SIKU. TUNASUBIRI TU MISAADA KUTOKA UARABUNI KUJA KUJENGA MISIKITI, NA WAZUNGU WAJE KUJENGA MAKANISA, BASI THATS ALL WE KNOW-
WAKE UP VIJANA WA KITANZANIA, HASA GENERATION HII. SAHAU MAMBO YA MABABU ZETU WALIOKWISHA PITA
WALIKUWA HAWANA ELIMU WAO WALIKUWA NI WA KUVUTWA TUNA KUFUATA WALICHOSEMA WAARABU AU WAZUNGU
TUKUMBUKE HIVI SASA NI MILLENIUM, MIAKA 2000 BAADA YA YESU NA MUHAMMAD
MDAU NEW YORK. Rama
Huyu jamaa hapo juu nadhani hajui historia ya nchi yetu au anapotoshwa na watu ambao enzi hizo za zamani walikuwa na malengo yao tofauti badala ya kujali nchi kama ilivyotokea baada ya Nyerere kustaafu.Udini ndugu yangu hautufikishi popote duniani.Watu wengi wanamlaumu Nyerere kuwa alikuwa anawapendelea wakristo sio kweli fanya utafiti wa ndani na uamgilie na nani walikuwa wanashirikiana nae wakati wa harakati za kupigania uhuru na angalia baraza lake la mawaziri lilikuwa na waislamu wangapi.Pia nataka kukuelemisha kidogo kuwa ukiwa kiongozi ambaye unataka maendeleo ya nchi yawe sambamba kwa kila raia unatakiwa uache kuwa na uchu wa mali,kwa hiyo viongozi wengi enzi zile walishindwa kukubaliana na yeye kutokana na wao kutaka kujilimbikizia mali wao binafsi na kuweka maslahi ya nchi nyuma.kwa hilo basi ilibidi awatose viongozi hao wabaya na wao wakaanza kusema kuwa anapendelea dini fulani.ukweli ni kuwa hata viongozi wa kikristo aliwatosa kama walikiuka maadili ya serikali.Namalizia kwa kukuomba kuwa elewa kuwa mtu akiwa anashindwa kukueleza ni jinsi gani yeye alitoa mchango kwa nchi asikuburuze kwa kutoa visingizio visivyokuwa na mbele au nyuma.Wewe amini dini yako na waache wengine waamini dini yao.Usilete visingizio kwa dini fulani kuwa hawakusoma sababu ya fulani.
ReplyDeleteMlio jua habari hizi kwa nini hamkuhoji wakati yupo hai na Nyerere kafa sasa hivi kama za kweli basi ni bi Titi ndie mkosa kutofikisha ujumbe
ReplyDeleteASANTE ANONY WA TISA 'MDAU RAMA, TOKA NY' NINAWAOMBA WOTA SOMENI MAONI YAKE.
ReplyDeleteMTU MWEUSI AMEKUWA MJINGA ASIYE NA ITIKADI YEYOTA AU MUELEKEO KATIKA MAISHA. TUMEKUWA WATU WA KUYUMBAYUMBA TU, TUMEKUWA WATU WA KUPOKEA IMANI NA ITIKADI ZA WATU OVYO OVYO. TUWACHUKUWE HAO WAZUNGU WALIOTULETEA UKRISTO NA BIBLIA YENYE HADITHI ZA SODOMA NA GOMORA. WATU HAOHAO LEO HII WANATUSHURUTISHA TUKUMBATIE USHOGA, HARAFU BADO TUNAWAAMINI NA DINI ZAO KIASI CHA KUBISHANA HATA KUUWANA SISI KWA SISI! HII INA MAANA KUWA MTU MWEUSI HAPA DUNIANI NI KAMA MPANGAJI TU, YAANI HANA KAULI YEYOTE WALA HAWEZI KUJIFANYIA MAAMUZI YAKE KWA MANUFAA YA KIZAZI CHAKE. JAMANI KWELI TUMEKUWA VIPOFU KIASI HIKI? HATA KAMA NI UJINGA, NI UJINGA GANI HUU?
yULE BWANA PALE BONDENI 'PRESIDAA' ANAITWA jACOB. SINASHAKA KUWA PIA NI MKRISTO, KWA KUWA JINA JACOB 'YAKOBO' NI JINA MOJA KUBWA KATI YA MAJINA YA BABA WAKUU WATATU WA KIYAHUDI. NINACHOTAKA KUSEMA HAPA NI KUWA YEYE AMENG'AMUA UONGO WAO NA KAWAPUUZA AMEKUMBATIA UTAMADUNI WAKE NA AMEJIOLEA WAKE ZAIDI YA MMOJA. HAWA WATU WANATUJENGEA HOFU MAISHANI KWA NJIA ZA DINI LAKINI WAO NDIO WAOVU NAMBALI WANI. BIASHARA YA UTUMWA, UKORONI NA VITA VYA UPOLAJI KILA LEO.
TAFADHARINI NIELEWENI VEMA SIJASEMA MWENYEZI MUNGU HAYUPO, LA HASHA. NIKO KANISANI KILA JUMAPILI. ILA UTAPELI WA WATU WEUPE NA UJINGA WETU WATU WEUSI, NI MAUTI KWETU.
Wapendwa ndugu zangu waislamu...asalam alekum. Maji yakimwagika hayazoleki..yaliyopita si ndwele...tugange yajayo. Rais wetu wa sasa ni ndugu yenu na idadi ya vyuo vinavomilikiwa na waumini wa kiislamu ni vichache sana kulinga nisha na vyuo vya madhehebu mengine. Tatizo ni la waislamu wenyewe kususia shule na kubaki kutupa lawama kwa wengine. Kama Nyerere alifanya makosa mbona mpaka leo hii kasi ya ujenzi ya vyuo vya miliki ya kiislamu ni vichache na marehemu hayupo nasi. CHANGAMOTO YA KWANZA NI KUONGEZA IDADI YA DIVISION ONE AT KINONDONI MUSLIM BADALA YA SHUNGI NA UVUTAJI BANGI. mIMI NIPO NJE YA NCHI KWA WAKIRISTO NA HAWANA MPANGO WA KUKUULIZA DINI. WANACHOTAKA WAO NI KULIPA FEDHA YAO. KUFAULU AU KEFELI NI JUU YAKO. wAKE UP MUSLIM. VITENDO NI MUHIMU KULIKO MANENO.KILA IJUMAA MISIKITI YOTE ICHANGE FEDHA KUANZISHA CHUO KIKUU KIKUBWA BADALA YA KUOMBA MISAADA YA KUJENGEWA MISIKITI MIKUBWA KUTOKA KWA WAARABU. vYOTE MUHIMU. FEDHA ZIKICHANGWA HAKIKISHENI ZINATUMIKA VIZURI BADALA YA WAJANJA WACHACHE. MSIAMINI KANZU WALA JOHO LA MTU. UFISADI UPO POTE..MAKANISANI NA MISIKITINI.
ReplyDeleteUkweli ni kwamba Nyerere alikuwa ni mtu ambaye hapingiki. Enzi hizo ukimpinga tu ulikuwa ni haini. Kubambikizwa kesi ilikuwa ni kitu cha kawaida. Wale walitoa kauli ya kumpinga alichosema Nyerere walikuwa na kesi ya kujibu. List ni ndefu. Na kinachotia wasiwasi ni kwamba wengi katika hao walikuwa waislamu tena. Akina Hanga wako wapi? Nyie vijana wa leo hamjui historia na hamuitafuti mnakurupuku tu.
ReplyDelete