CRDB Benki inawataarifu wateja wake wote kuwa tawi letu la Lumumba lililoko katika Jengo la Ushirika, Barabara ya Lumumba, jijini Dar es Salaam halitatoa huduma siku ya Jumamosi tarehe 05 Novemba 2011.

Hali hii inasababishwa na ukarabati mkubwa unaofanywa na mmiliki wa jengo la Shirikisho la Vyama Vya Ushirika Tanzania (USHIRIKA) ambalo CRDB Benki ni mpangaji. Ukarabati huu ni kwa ajili ya kuboresha eneo lililounguzwa na moto na kuboresha mandhari ya jengo.

CRDB Benki inawashauri wateja wake kupata huduma za kibenki kupitia matawi yake mengine ya Kariakoo (Barabara ya Uhuru), Vijana (mtaa wa Lumumba), Azikiwe na Azikiwe Premier (mtaa wa Azikiwe) na matawi yetu mengine zaidi ya kumi kwenye maeneo mengine hapa jijini pamoja na ATM lukuki zilizosambaa kila kona ya Jiji.

Huduma katika Tawi la Lumumba zitarejea tena kama kawaida Jumatatu tarehe 07 Novemba 2011.

Kwa mawasiliano zaidi, tupigie kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja (CRDB Bank Call Centre) kupitia namba:

022 2197700, 0714 197700, 0755 197700, 0789 197700 au kwa barua pepe customer-hotline@crdbbank.com au kupitia facebook na twitter: www.facebook.com/crdbbank , www.twitter.com/crdbbankonline

Tunaomba radhi wateja wetu kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Uongozi

CRDB Benki, Benki inayomsikiliza mteja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hili tangazo limechelea kwa hata sasa ni vigumu kidogo kupenyapenya kwenye uzio wa tawi hilo ili kupata huduma. Kwa hakika walipaswa kutarifu mapema zaidi mana hata sasa huduma pale ni za kisumbufu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...