Asalaama Alaykhum wajina

Kwakweli hali bado ni tata sana ya mafuta kwa mji wa mtwara kwa hata kile kituo kimoja cha Gapco kilichokua kina mafuta ya kusubiri kwa foleni ya masaa 8 had 10 nacho sasa kimeishiwa toka juzi usiku na jana yote hapajauzwa mafuta sehemu yeyote halikadhalia leo mji mzima hauna mafuta.

Sasa bei za bajaji, piki piki na taxii zinapanda na wengine kulazimika kupaki kabisa magari yao. Wamejitokeza wachuuzi walifanikiwa kununua mafuta kwa magaloni sasa wanauza mafuta haya kwa shilingi elfu 5000
kwa lita moja nunua hutaki acha watanunua wenye pesa.

Walah tunateseka wenye vyombo vinavyotumia petroli kila mmoja anasema yake ukweli haujajulikana je ni kweli bidhaa hii ni hafifu au kuna mgomo baridi?????

WAHUSIKA WENYE MAMLAKA LIANGALIENI HILI MTUNUSURU YARABI

MDAU MTWARA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Miaka 50 ya "UHURU TUMESUBUTU TUMEWEZA TUNASONGA MBELE + MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA= CCM OYEEE!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. MAFUTA...suluhisho lake bado kitendawili!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...