Jumla ya makandarasi 7 waliofanikiwa kupita katika mchakato wa awali wa kumpata mkandarasi atakayeshinda zabuni ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni walifanya ziara ya ukaguzi mapema wiki hii. 

Mtaalam Mshauri kutoka Kampuni ya Arab Consulting Engineers (ACE) Mhandisi Mohamed Shaeb aliongoza ziara hiyo iliyokuwa na lengo la kuwapatia maelezo ya kitaalam Wakandarasi hao kuhusu maudhui ya mradi husika na changamoto zake kabla ya hawajawasilisha makisio yao kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.
Awali kabla ya mchakato huu walikwisha jitokeza Makandarasi 16 ambao baada ya kuchambuliwa ndipo kati yao wakapatikata hao 7 ambao wanashindanishwa.
Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF kwa kushirikia na Wizara ya Ujenzi wanaendelea na mchakato wa kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambalo ujenzi wake unatarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa mwaka 2012. 

Daraja hilo ambalo ni la kisasa zaidi kujengwa hapa nchini ambapo litakuwa na barabara tatu kila upande yaani kuwa na uwezo wa kuruhusu magari sita kupita kwa wakati mmoja.
Daraja la Kigamboni linatarajiwa kuwa na urefu wa mita 600 na hapo litakapokamilika litakuwa ni kiungo muhimu kati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni na pia litachangia katika jitihada za kupunguza msongamano wa magari hapa jijini.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mnamo mwezi Machi mwaka huu wa 2011 ililiagiza Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha kuwa usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Kigamboni unaimarishwa na hivyo kuondoa kero na adha nyingi wanazozipata kwa sasa. 

Agizo hilo lilitolewa wakati wa ziara aliyoifanya Waziri Magufuli alipotembelea eneo la Kurasini Vijibweni, ambako daraja hilo litajengwa. Waziri Magufuli alichukua hatua hiyo kutokana na mazungumzo kuhusu ujenzi wa daraja hili kuwa yamechukua muda mrefu bila ya hatua madhubuti kuonekana.
Ujenzi wa daraja hili utachangiwa kwa asilimia 60 na NSSF wakati ambapo Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi itachangia asilimia 40 zilizobakia.
NSSF tayari imekwishatenga kiasi cha Shilingi bilioni 100 hadi sasa kwa ajili ya mradi huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. naomba utueleweshe vizuri kuhusu hilo daraja,maanake umesema litakuwa na njia tatu kila upande hilo sawa je vipi waenda kwa miguu,baiskeli,mikokoteni,n.k?

    ReplyDelete
  2. Flyovers ndio zimeyeyukia wapi?

    Kabla ya uchaguzi wa raisi mlituahidi ooooh flyovers zinaanza kujengwa mwezi huu, oooh mkandarasi ameshaanza kupima. Mara ukiwa bungeni ukawatangazia wananchi kuwa tayari kazi ya ujenzi imeshaanza kwenye makutano ya TAZARA. UONGO MTUPU!

    ReplyDelete
  3. subiri uone magari yatakavyokuwa yanatumbukia baharini.

    ReplyDelete
  4. Jamani tunaomba serikali isiwadanganye watanzania. Kila linapokuja swala la kupigiwa kura, serikali inaibuka na vishawishi kwa wananchi ili waonekane wanachapa kazi na kushughulikia kero zao. Kwa mfano, hili swala la kujenga daraja la Kigamboni linaloibuliwa sasa hivi ni mbwembwe tu za CCM kuwapumbaza watanzania ili wasiwe wakali juu ya mchakato mbovu wa kuitafuta katiba mpya. Watanzania, swala la katiba si la chama wala mtu mmoja, tunapaswa kuungana wote kutafuta katiba mpya yenye kukidhi mahitaji ya watanzania wote bila kujali itikadi zao. Utaratibu aliouongelea rais ni mbovu, umepitwa na wakati na ulikuwa ukitumiwa na marais waliopita bila kuwapa wananchi fursa tosha ya kuchangia tangia mwanzo. Ndio maana tunahitaji kitu kipya, utaratibu mpya wa kukidhi mahitaji yetu ya sasa na yajao. Utaratibu huu unapaswa kushughulikiwa na watu huru (ikibidi wasiofungamana na chama chochote) na kwa vyovyote vile hawapaswi kuchaguliwa na rais. Rais anaweza kuidhinisha tu kuchaguliwa kwao. Wanasiasa wanatuharibia nchi, utaratibu uliopitishwa usingekuwa mbovu wasingeung'ang'ania kuupitisha kwa nguvu wakati watu bado wanalalamika. Kweli kwa mtindo huu, panaweza kuwepo vurugu nchini.

    ReplyDelete
  5. Daraja hilo litakuwa na tal za malipo kama vile pantoni naomba tueleweshwe.

    ReplyDelete
  6. Jamani tunaomba serikali isiwadanganye watanzania. Kila linapokuja swala la kupigiwa kura, serikali inaibuka na vishawishi kwa wananchi ili waonekane wanachapa kazi na kushughulikia kero zao. Kwa mfano, hili swala la kujenga daraja la Kigamboni linaloibuliwa sasa hivi ni mbwembwe tu za CCM kuwapumbaza watanzania ili wasiwe wakali juu ya mchakato mbovu wa kuitafuta katiba mpya. Watanzania, swala la katiba si la chama wala mtu mmoja, tunapaswa kuungana wote kutafuta katiba mpya yenye kukidhi mahitaji ya watanzania wote bila kujali itikadi zao. Utaratibu aliouongelea rais ni mbovu, umepitwa na wakati na ulikuwa ukitumiwa na marais waliopita bila kuwapa wananchi fursa tosha ya kuchangia tangia mwanzo. Ndio maana tunalalamika na kuhitaji kitu kipya, utaratibu mpya wa kukidhi mahitaji yetu ya sasa na yajao. Utaratibu huu unapaswa kushughulikiwa na watu huru (ikibidi wasiofungamana na chama chochote) na kwa vyovyote vile hawapaswi kuchaguliwa na rais. Rais anaweza kuidhinisha tu kuchaguliwa kwao. If you make a faulty start you end up with faulty results!!! Wanasiasa wanatuharibia nchi kwa sababu ya ubinafsi uliopitiliza na kujisahau, utaratibu uliopitishwa usingekuwa mbovu wasingeung'ang'ania kuupitisha kwa nguvu wakati watu wengi sana bado wanalalamika. Kweli kwa mtindo huu, panaweza kuwepo vurugu nchini. Watanzania tuamke na tuache ubinafsi, kuwa na raslimali ni muhimu sana ila si msingi tosha wa maendeleo. Tunapaswa kuwa na vitu vingine zaidi ya hapo (i.e. intangible resources, e.g. aggressiveness, good governance/rules and regulations, diligence, knowledge, desire for positive change, integrity, entrepreneurial spirit, patriotism, etc). Swala la katiba si la kufanyia utani hata kidogo, tukifanya utani litatugharimu sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...