Katibu Mtendaji wa Taasisi ya WAMA nchini Daudi Nasibu (aliesimama) akichangia katika mkutano wa siku moja wa wadau kutoka sekta binafsi ya kuwashirikisha katika kuchangia mradi wa Pamoja Tuwalee unaofanywa na WAMA pamoja na FHI kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, (nov,18-2011)katika viwanja vya WAMA jijini Dar es Salaa.
Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano wa wadau kutoka sekta binafsi ya kuwashirikisha katika kuchangia mradi wa Pamoja Tuwalee unaofanywa na Taasisi ya WAMA pamoja na FHI kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini. Mradi huo unafadhiliwa na na msaada kutoka Marekani (USAID) .ni mradi wa miaka 5. Mradi wa Pamoja Tuwalee unaendesha shughuli zake katika ukanda wa pwani kwenye wilaya 25 ziliopo katika mikoa ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...