Naibu Meya wa Mkoa wa Tanga Seleboss Mustafa  akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja  na nusu Mshindi wa kwanza wa mbio za  Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilomita 140,Hassan Sharif (kulia) mara baada ya kuibuka kidedea katika mbio hizo kwa kutumia  muda wa masaa 4:13.07 wapili toka kushoto Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude na msimamizi wa mawakala kanda ya Kaskazini Michael Kasun.
Mwaandaaji wa Mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge Sophy Wakati akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu  kushoto kabla ya mbio hizo kuanza,wa pili kutoka kushoto Buruhani Yakub ambae ni  Mwandishi wa Habari wa Mwananchi Communication na Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Washiriki mbio za Vodacom Tanga Cycle Challenge kwa upande wa walemavu wakimaliza mbio hizo hapo jana mjini Tanga.
Baadhi ya washiriki wa mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilometa 140 wakichuana vikali hapo jana mjini Tanga ambapo Hassan Sharif aliibuka mshindi kwa kutumia masaa 4:13.07 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi laki moja na nusu.


kwa picha zaidi 
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kwa kuchapia huyu!!!! tanda au tanga?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...