Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Nanihii,
Nimekutana na kipande hiki cha historia katika gazeti moja la huko nchini nikavutika sana, na napenda kushirikisha jamii kupitia blogu yetu ya Jamii kufichua baadhi ya ukweli ambao si wengi katika kizazi kipya wanaufahamu.


Historia ya Tanzania yetu imeporwa na baadhi ya wanasiasa kwa sababu zao. Si siri kuwa Waislamu wa TZ wanahesabika kuwa ni dhalili wasio na elimu wala mchango katika maendeleo ya nchi. Wengine hudai eti waislamu badala ya kwenda shule waliogopa kubatizwa, hivo wakaishia madrasa tu.


kashfa hii imeniuma sana, na Alhamdulillaah ukweli unaanza kudhihirika. Habari hii nimeifuma ndani ya Gazeti la Habari Leo. Wadau mambo hayo:


Kreist Sykes, aliyewahi kuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam, ni mtoto wa hayati Abdulwahid, mpigania uhuru wa watu weusi waliofanya kazi serikali ya kikoloni na mwanzilishi na TAA hadi TANU. Kreist Sykes, kwa maneno yake mwenyewe, ana msisitizo kuwa wakati umefika kwa CCM kuwaenzi wa waanzilishi, waasisi na wapigania uhuru wa Tanganyika.


Wakati akizungumza na HabariLeo mwishoni mwa wiki, anasema, wakati umefika kwa chama na serikali yake, kuiweka historia katika kumbukumbu isiyofutika wala kusahaulika, kwani mali bila daftari hupotea bila kujua.


Anahoji kuwa kwanini inashindikana kuandika historia ya watu waliotoa maisha na mali zao juhudi za TAA na baadaye kuwa TANU? Historia ya sahihi, ya watu sahihi na wakati sahihi inakufa kifo cha mende, kutokana na watu walioshiriki katika harakati hizo, wanatangulia mbele ya haki.


Anajua historia kwa kiwango chake. Anatanabaisha kuwa mara mbili jitihada za kuandika historia ya wapigania uhuru, imejaribiwa, ikashindikana kuandikwa. Sababu hazikuwa na uzito zaidi ya historia yenyewe. Mara ya kwanza walitaka kuandika historia ya TAA hadi TANU mwaka 1964 kwa kumtumia Dk. Wilbert Kleruu, baada ya kutoka masomoni Marekani, ambaye angemtumia Abdulwahid Kreist (baba yake), kuwa chanzo cha habari, ikashindikana.


Mara ya pili ilikuwa mwaka 1978, mwaka mmoja baada ya CCM kuzaliwa. Wakati huo Kingunge Ngombale-Mwiru alitaka kuweka maktaba Dodoma na hayati Ditopile Mzuzuri, angekuwa chanzo cha habari, pia ilishindikana.


Kucha kuchwa waasisi wa Taa na Tanu, walioshuhudia Uhuru Desemba 9, 1961, walioshuhudia kuzaliwa CCM hadi leo, wanazidi kupukutika , katika chama labda amebaki Kingunge Ngombale-Mwiru na wengine wachache hawajiwezi.


Katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru na kabla, tangu kampeni za TAA, hakuna historia ya madhubuti iliyoandikwa ya kuwaenzi waanzilishi wa Taa, Tanu na wapigania uhuru, tunaoushangilia leo.


Tunapoadhimisha miaka 50 ya uhuru, Kreist anasema tuirudie historia kutafuta mchango wa hali na mali wa wapigania uhuru waliokuwapo Dar es Salaam, Rufiji, Dodoma, Mwanza, Songea na mahali pengine.


Pamoja na picha ya pamoja kuonesha watu wapigania uhuru 17 walioshiriki kuanzisha Tanu, ukweli ni kwamba wapo wengi ambao walitoa nguvu na uhaki wao kukipigania chama na hadi kupata uhuru.


Historia ya kujitoa kupigania uhuru ya akina Kreist, Dossa Aziz, Tewa Said Tewa na wengine wengi jijini Dar es Salaam, inapotea polepole. Hakuna mahali panaonesha mchango wa familia ya Paul Bomani kutoka Kanda ya Ziwa Vicotoria na wengine wengi, ambao maisha yao yalikuwa yamechanjiwa rangi ya kijani na nyeusi alama ya chama.


Kuna watu muhimu kama akina Hamza Mwapachu, na familia yake, japo alikuwa mtumishi wa serikali, alitoa mchango na hata kuwatumia watoto wake kusafirisha barua kwenda mahali pengine kwa kugumia masunduku ya wanafunzi wa shule.


Upande wa Kusini, miongoni mwa wengi, yupo Said Chamwenyewe wa Rufiji, ambaye alisafiri umbali mrefu kwa baiskeli akikusanya michango na ada ya sh 50 kutoka kwa wapigania uhuru.
Wengine ni Dustani Omari ambao walijitolea kukipigania uhuru kwa kutumia nyumba, lakini wamekufa na sasa historia yao inapotea.


Kreist amewataja akina Patrick Kunambi wa Morogoro, akina Dk Vedasto Kyaruzi wa Kagera, Joseph Kasella Bantu wa Tabora aliyeshiriki kuandika Katiba ya TANU na John Rupia na wengine wengi, ambao hesabu yao ni ndefu, lakini mchango wao haujaandikwa mahali.


Wananchi hao ambao walipata upinzani kutoka kwa Wajerumani na Waingereza waliotumia machifu kuwakandamiza wazalendo wenzao, wamekufa maskini hata hawaenziwi. Mchango unaonekana kwa kiasi kikubwa ni wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye alichaguliwa kuongoza TAA Aprili 17, 1953 badala ya Abduwahid Skyes.


Lakini, ukweli wapo wengi waliojitolea na kutoa nguvu zao kukipigania chama. Wachache akina kama akina Rashid Kawawa na wengine, wanakumbukwa kwa kujitosa katika kuhamasisha chama kwa wananchi na kuwadundisha kuukata ukoloni.


Mpango wa kuwaenzi waasisi wa TAA na TANU, wakiwamo Abdulwahid na Ally Skyes (mdogo wake), aliyechora kadi za TANU, kwa lengo la kutetea maslahi ya wafanyakazi Waafrika katika maeneo mbalimbali ya kazi ni tuzo ambayo CCM ingeweka katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru.


Wapo baadhi ya wafanyakazi wa serikali ya kikoloni, waliojiunga na Taa na baadaye Tanu kwa siri, waliwatumia wanafunzi kusafirisha barua, wakihofia kupoteza vibarua. Mzee Dunstan Omari na Mwapachu aliyekuwa akifundisha Mzumbe Morogoro, waliwatumia watoto kusambaza kampeni za kumng’oa mkoloni ili kupata uhuru nchini.


Kreist anasema mchango wa wanasiasa hao wa zamani, ambao hawakuwa na vyombo vya usafiri isipokuwa kukanyaga kwa miguu ama kwa baiskeli, historia haijawatendea haki kutathaminiwa na kuenziwa.


Marehemu Abdulwahid (baba yake Kreist), akiwa mtumishi wa serikali na akiwa askari magereza, alijitosa kupigania uhuru na kutoa mchango wa hali na mali hadi kuhakikisha Tanganyika inakuwa huru.


Wakati huo alitumia gari lake namba TDP 676 kusaidia kumsafirisha Julius Nyerere kutoka sekondari ya Pugu, Dar es Salaam, alikokuwa akifundisha hadi jijini Dar es Salaam mtaa wa Kipata, kumshirikisha kwenye Taa na baadaye Tanu.


Wakati huo, Waafrika walikataliwa kufika kati ya jiji, isipokuwa mahali ilipo hoteli karibu na Bilcanas. Lakini, walitumia nyumba zao kuwakutanisha wapigania uhuru kwa siri na kujipanga kuikomboa nchi.


Wazee hao, Nyerere, Abdulwahid na Mwapachu, siku za mwishoni mwa wiki walikutana ama nyumbani kwa familia ya Skyes kwa Dossa, kujadili ni mbinu gani watatumia kuupata uhuru mapema.


Gavana wa wakati huo, Edward Twining kama wengine waliotangulia aliwatumia machifu kupinga kampeni za Taa na baadaye Tanu, wakati mwingine alithubutu kuwahamisha watumishi ili wasiendele kampeni hizo.


Kampeni hizo zilikuwa wazi wakati walipoamua kuchelewa kuisajili Tanu hadi Novemba 30, 1954, miezi minne baada ya kuanzishwa rasmi. Kreist anakumbuka kuwa uhuru ulipopatikana alikuwa na miaka 11. Lakini, baba yake na kaka wa baba yake Ally, wamekuwa wakimsimulia kila wakati.


Anakumbuka vizuri mchango wa viongozi wa TAA wakiwamo Waislamu wa Pwani, kutokana na chama hicho kuanzisha vuguvugu zake Pwani, walimpa msaada wa karibu Nyerere, hasa alipoanza safari za kudai uhuru UN.


Mwapachu ambaye alimtambulisha Nyerere kwa viongozi wa TAA na wakampa urais wa chama hicho, wakati wa uhai wake alikuwa akisimulia na kueleza mchango wa familia ya Sykes katika kutafuta uhuru wa Tanganyika.


Mikutano michache iliyofanyika Anatoglou, Dar es Salaam pamoja ya siri nyumbani kwao, ilifanikisha kuanzisha TANU Julai 7, 1954 na miaka tisa baadaye hapo Desemba 9, 1961 ukapatikana Uhuru. Mchango wao si wa kubeza.


Jumatano tutaendelea na mfululizo wa makala hizi za miaka 50 ya Uhuru, ambapo tutakuwa na mama yake Ally Sykes, Mwasaburi Ally Sykes, atakayeelezea mengi mengine juu ya historia ya nchi hii. Usikubali kupitwa na uhondo huo, ikiwa ni pamoja na namna alivyompokea Mwalimu Nyeerere akiwa kijana katika harakati za Uhuru wa nchi yetu.


DODOSO:
Nani alianzisha chama cha TAA?
Nani alimleta Nyerere kwenye siasa?


Mndengereko, Ukerewe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Tunashukuru kwa kuelimisha wananchi juu ya ukweli kuhusu Historia ya Tanzania.
    Ningependa vilevile kupata ukweli kuhusu vita vya majimaji ambavyo navyo kuna majina mengi ya "Kichina" yametumika kwamba watu hao ndio mashujaa walioleta upinzani dhidi ya wakoloni kitu ambacho si kweli.
    Tusaidieni kupata ikweli kwani hata baadhi ya maelezo yalitaifishwa na wazungu na mlioko huko Ukerewe labda mnaweza kutafiti kama haya ni ya kweli.

    ReplyDelete
  2. Nashindwa kuunganisha/kulink kusoma kwa Waislamu na kuandikwa historia ya Tanganyika/Tanzania, kama issue yako ni kuandikwa historia...sema au kazania kuandikwa historia, mimi sioni uislamu unaingiaje hapo maana hata akina Rupia, Bogohe, Kasera, Sykes, Aziz Ally etc walifanya hivyo kwa utanganyika sio kwa uislamu wala ukristo wao, na wakati wa kupigania uhuru haikuwa issue ya shule ila watu walitumia hali na mali kumsaidia Nyerere aliyekuwa na shule, suala ni zuri kuwa tuhangaike historia iandikwe upya lakini sio kuchanganya issue ya waislamu kutosoma na istoria kuandikwa, watanzania tutaanza lini kuwa obkective bila kuwa subjective?

    ReplyDelete
  3. Historia imepotoshwa na Nyerere baada ya kuichukua nchi na kuifanya yake na sio kwa manufaa ya Taifa bali ni kwa kanisa tu.Hakutaka mtu yeyote aijue historia ya ukweli ili aonekane yeye ndie shujaa peke yake na kuwainua wakristo kielimu na kuwatukanisha waisilamu.Na leo hii wapumbavu wanaweza kufungua midomo yao na kusema waisilamu hawataki kusoma shule ila wanapenda madrasa tu.Wakati waisilamu waliosoma vizuri wamedhulumiwa na kunyan'ganywa nafasi zao ktk masomo ya juu na kupewa wakristo ili kuwavunja waisilamu kielimu.Ndio maana nchi mpaka leo haina muelekeo kwa maana viongozi hao waliokuwepo hapo inabidi waifanyie kazi kanisa kwanza hata kama ni muisilamu,Wanasahau Taifa linahitaji muelekeo mzuri ili kuweka hali ya usawa kwa kila mtanzania bila kuchagua dini.
    Tafadhali usiibane Michuzi.

    ReplyDelete
  4. Nachelea kusema kwamba mwandishi huyu ana lake jambo! Sioni kwanini kaanza na lawama juu ya waislamu kutokusoma...maana yanayofuata hayaendani na kile achoanza kukiandika.

    ReplyDelete
  5. Nimesoma kiasi habari ya mhusika huyu na sikupendezwa sana na maelezo yake

    Kwanza inaonekana Bingwa ana chuki binafsi, kitu ambacho ni swala lake mwenyewe. SIdhani kama ni mtazamo wa wengi kuwa Tanzania ni nchi ya udini kama zilivyo Libra, Misri, Somalia na kwingineko.

    Kwa kiwango tulicho nacho cha kuvumiliana katika dini zetu ni cha kusifiwa zaidi ya kuchochewa.

    Mbili, kama kuna maelezo kuwa watu wa dini fulani walikimbia umande, hayo ni maelezo ya watu ya kujaribu kuelezea ama kupambanua ni kwanini dini fulani wamesoma na wa dini fulani hawakusoma sana. Hata kuumbwa kwa dunia kumeelezwa kwa namna nyingi kutokana na jinsi watu walivyoweza kukisia hasa pale ukweli unapokuwa haujulikani vilivyo.

    Sasa Bingwa wetu akiwa kama mtu aliye elimika (aliyeosha macho kwa kuwa katika nchi za wenzetu) alipaswa basi kumfunga paka kengele na kuiandika historia aifikiriayo kwa namna yake akihusisha vihusishi (references) vya kweli. Tutamsikiliza zaidi ya kuzungumza majungu bila data.

    Tatu, anazungumzia zaidi kuandika historia. Kwanini asichukue jukumu hili kuandika habari hiyo ili watu tukamsoma badala ya yeye kulalamika kwamba eti watu wengine wangeliandika na kadhalika? Siku hizi teknolojia ni kubwa na pana na ni rahisi kwake kuandika historia hii na akawa mtu wa kwanza kuziba shimo jeusi (black hole) la historia anayodai.

    Bingwa anapo lalamika alidhani ni akina nani wangeli ifanya hiyo kazi kwa jinsi anayoipenda yeye?
    Zaidi zaidi basi nadhani huyu jamaa amesoma tu kijigazeti kimoja na kukurupuka kwa yaliyojiri humo kwamba historia haikuandikwa. SIO KWELI
    HIstoria kabla ya uhuru imeandikwa kwa kirefu mno na kwa mapana. Hata nadhani kwenye blog hii kuna Kasisi mmoja tena Mzungu aliye andika historia kwa namna yake na jinsi alivyoitambua. Kuna kitabu cha Bibi Titi Mohammed. Kimeandika historia pia kwa namna yake. Kuna vitabu lukuki vya Tanu na vimeandika historia kwa jinsi na namna ya kila kimoja.

    Sasa basi ikiwa kama mwenzetu hujaridhika na hizi nondo zilizopo kwanini usichukue jukumu la kuiandika historia kwa jinsi na namna yako tukakusoma?
    Tabia ya Watanzania ya kupenda kufanyiwa na kulaumu wengine kwamba kwanini hawajaandika hili hawajafanya hili itaisha lini? Wewe sio Mtanzania? Jenga Taifa lako kwa kutoa mchango wako kui tafuta na kuiandika historia ya nchi jinsi upendavyo nasi tutakusoma.

    Nimekuunga mkono kwa jambo moja tu lakini kwa mtazamo mwingine.
    Nilisoma kwenye nondo fulani kuwa Maraisi wa marekani wana establish Library zao kila wakisha staafu. Je kwa Tanzania ni Raisi yupi aliyeweza kuanzisha Library yake na ni wapi? Ningelifurahi sana kujua. Kama ni hola basi sina cha kusema

    ReplyDelete
  6. Ndugu mwandishi wakipande hiki nakushukuru saana kwa kutumia mda wako kuandika nakutafuta nyaraka hizo muhimu.
    Ila hauko makini kwani maneno yako ya mwanzo juu ya uislamu sijayapenda kabisa kwani wakati wa harakati za kupigania uhuru hoja ilikuwa ni uzalendo na sio msimamo wa kiiimani kama unavotabainisha.
    Acha tusherekee kwa kuwasifu wahasisi na sio familia furani eti kwa sababu walitoa mali zao.
    Ivi unafahamu kuna watu waliokufa katika vita ya kumgoa Nduri Idd Amin je hao utawaitaje?au kwasababu hawajatoa ela basi hao sio wazalendo?
    Asanteni

    ReplyDelete
  7. Wewe mheshimiwa nimekupunguzia hadhi kabisa ungeacha habari ijieleze yenyewe nadhani ingetosha, Maneno yako ya mwanzo uliyoanza nayo ni dalili fika za ufira finyu na uchochezi wa chuki za kiimani, Eti anaenziwa ni Nyerere, peke yake, hutji Kawawa, au unataka kila aliekuwepo kwa kipindi cha kupigania uhuru siku yake ya kufa iadhimishwe kitaifa? kufanya hinyo mbona mwezi mzima Watanzania tutakuwa na siku kuu?, Kama Takwimu ilionesha Jamii kubwa ya Wenzetu waislamu hawajafikia kiwango cha Elimu walionayo wakristo huoni ni changamoto ili waipate?, Kama ni madaraka, huoni Tutakuwa wapumbavu kama madaraka yatagawanywa eti kwa itikadi za kiimani? Kwa sasa takwimu za Watanzania wenye imani ya Kiislamu ni kubwa hivyo hata ukiangalia katika nafasi za uongozi wapo wengi, Sasa wewe umeshikilia Takwimu ya Mwaka 47 hadi leo. Kama ni kutajwa kielimu, Vipi jamii ya wafugaji,(wamasai) wanaotajwa kila kukicha , nadhani ungekuwa jamii hiyo ungejinyonga ama? maana ni ukweli usiofichika kuwa wengi hawaendi shule, ila tunachukulia ni changamoto kwetu kupeleka wanetu shule nasisi wenyewe kujiendeleze, Funguka akili, Mie Mmasai Bana.

    ReplyDelete
  8. Very interesting piece indeed. I wish we had like a museum explaining how it all started. I remember my Dad (RIP) used to tell us these stories. Most of the people if not all mentioned were his friends. Looking forward to another article on Wednesday.

    Tanzanian in USA

    ReplyDelete
  9. UDINI UNAKUSUMBUA. HILI SI JAMBO JIPYA KUTOKA KWA NINYI WENYE UDINI. MTU ALIYEFILISIKA KICHWANI HOJA ZAKE NI ZAKIDINI AU KIKABILA. KWA TAARIFA YAKO MKWAWA, MIRAMBO, KINJEKETILE HWAKUWA NA DINI. HARAKATI ZA KUPIGANIA UHURU ZILIANZA HATA KABLA YA NYERERE KUZALIWA. MTOA HOJA ANAJIKITA TU KWENYE MIAKA YA HAMSINI KWA AJENDA YAKE YA KIDINI. AKUMBUKE KUWA DINI NI MAWAZO TU YA BINADAMU NA NI YA KUPITA KWANI BINANDAMU WALIKUWAPO KABLA YA DINI.

    ReplyDelete
  10. Ndugu,
    asante sana kwa kusahihisha ukmweli juu ya historia na jitihada za uhuru. Tafadhali, epuka na mambo ya dini. Mimi nafahamu familia ya Sykes na ya Mwapachu na umesema ukweli. Umesahau kina Kirilo Japhet, mkristo toka meru, ambayeLIKUWA MWAFRIKA WA KWANZA KUHUTUBIA MKUTANA WA SECURITY COUCIL UNITED NATIONS MWAKA 1952,mAKABURU WALIINGILIA ARDHI MERU WAKAUA WAMERU.Kirilo Japhet, mkristo, alirudi tanganyika akawa hero na inspiration kwa shughuli zote za uhuru. yeye na wengine SABA wakaanzisha TANU.
    Nashukuru umesema ukweli juu ya harakati za uhuru na michango ya wazee kama sykes na wengine. Bila wao Nyerere asingeweza kitu. Epuka tu na dini. Mimim mwislamu pia lakini sitaki kuweka dini mbele.

    ReplyDelete
  11. Mwandishi wa makala aache udini! Mbona Watanzania hatuchoki kuibua mijadala ya dini isiyo na maana? Nakubaliana na wachangiaji wengine kwamba Mwandishi wa makala hii alikuwa na ajenda nyingine ambayo si njema kwa jamii yetu. Cha kufanya ni kuwapuuza watu kama hao ila sisi Watanzania tuendelee na umoja na upendo wetu bila kujali tunaabudu nini na wapi?

    ReplyDelete
  12. HISTORIA ALIYOTOA MWANDISHI NI YA UKWELI!: ISIPOKUWA TAFADHALI TAZAMENI HAYA HAPA CHINI:
    1.UTANGULIZI WAKE AMEUTOA WA MOJA KWA MOJA hivyo ameshikwa na jazba kidogo.
    2.USHAHIDI WA HISTORIA HUENDANA NA ARTIFACTS AND ARCHIVES(Nyaraka) Wataalamu wa Historia wanalijua hili, kwa vile Historia hiyo aliyoitoa INAVYO VIGEZO HIVYO, yaani Vipande vya magazeti kwa makala ktk siku hizo kabla ya uhuru na mara tu baada ya uhuru, tarehe na jina la Mhariri ,zaidi ya hapo pale jumba la makumbusho vitu hivi mabaki yake bado yapo.
    3.KWA VILE HISTORIA SAHIHI ILIPINDISHWA KAMA MWANDISHI ANAVYODAI ,NDIO MAANA HITIMISHO LAKE LINAONEKANA KUTOFAUTIANA NA UTANGULIZI WAKE KTK MAELEZO!....NI BUSARA MAWASILIANO YAKAFANYIKA KUMFIKIA ILI ATOE DALILI HIZO ANAZODAI ILI SUALA LIELEWEKE VIZURI....HAZINA KUBWA KWA WATANZANIA TULIYONAYO NI KUWA JAMII ILIYO NA KISIMA CHA BUSARA!

    ReplyDelete
  13. Hivi kama mtu unajua historia kwa nini usiandike kitabu? kuna mtu amekukataza kuandika kitabu? Viongozi wengi wa nchi nyingine na wananchi wa kawaida wanapeleka hoja na miono yao kwenye vitabu, kwa nini hii inakuwa ngumu Tanzania? Unataka mtu akuandikie au? Andika hata biography. Kama kitabu kina hoja watu watanunua na kunukulu kama hakina hoja kitakosa soko. Watu tuache kulalama lalama kuhusu historia kama mna hoja andikeni vitabu. Haya na siku hizi magazeti binafsi yako kwa nini msiepeleke makala buko? Mko addicted kwa kulaumu

    ReplyDelete
  14. Wewe ni kama yule wa jana aliyekuja na hoja kwamba dini fulani ilikataliwa kuanzisha chuo kikuu miaka ya 60 na 70!!. Mambo ya udini udini tu, choko choko, harakati zisizo na tija na kupandikiza chuki za chini chini, hakuna lolote. Use your time more productively!

    ReplyDelete
  15. NASISITIZA KTK NUKUU 3. NILIZOTOA MWANZO KUHUSU UHALISIA WA HISTORIA YEYOTE ILE:.......NI KUWA HISTORIA HAIPINDISHIKI KIRAHISI.......
    (ARTIFACTS AND ARCHIVES) ZIPO KTK MUUNDO WA:
    1.MAPOKEO YA HADITHI KTK MASIMULIZI SAHIHI KUTOKA KWA WATU WALIOKUWEPO WAKATI HUO,
    2.NAKALA ZA MAGAZETI YA WAKATI HUO, Majina ya magazeti,Makala,tarehe na Majina ya Wahariri wa WAKATI HUO KABLA YA UHURU NA MARA TU BAADA YA UHURU.
    3.PICHA
    4.MABAKI YA HISTORIA YA TANGANYIKA YALIYOPO KTK JUMBA LA MAKUMBUSHO YA TAIFA, AMBAYO PAMOJA NA KUPINDISHWA KWA MWENYE AKILI ATAGUNDUA TU.
    -----------------------------------
    MFANO HUU NI KAMA SUALA LA PALESTINA JINSI ISRAEL NA MAREKANI ZINAVYOJARIBU KUPINDISHA HISTORIA SAHIHI YA MASHARIKI YA KATI NA KUUDANGANYA ULIMWENGU HUKU WAKIPAISHA ITIKADI NA UENEZI WA KIZAYUNI......IMEFIKIA MWEZI HUU BAADA YA UNESCO (SHIRIKISHO LA HISTORIA LA UMOJA WA MATAIFA)KUIPA UANACHAMA PALESTINA TU, MAREKANI IKAJITOA KWA MASLAHI YA ISRAEL HUKU WAKIPINGA UANACHAMA WA PALESTINA USITISHWE,,,,,HUU NI MFANO TU KTK MIFANO YA UPINDISHWAJI WA HISTORIA SAHIHI DUNIANI AMBAO UNA FANANA KABISA NA MAKALA YA MWANDISHI KTK BLOGU HAPA KUHUSU HISTORIA YA UHURU WA TANZANIA.

    ReplyDelete
  16. WEWE MDENGEREKO WA UKEREWE NAONA WINTER INAKUSUMBUA UNATAFUTA CHOKO CHOKO ZA KIDINI. TAFUTA UWEZEKANO UPATE JOTO LA KUTOSHA UTAPATA MAWAZO MAZURI NA YA KUJENGA (POSITIVE)

    ReplyDelete
  17. Hii blog inataka kuleta Balaa sasa.Weka pembeni udini,Hisotri ni muhimu iandikwe upya..Hivi hakuna kweli vitabu vinavyoelezea hiwtoria ya TZ?Tumekalia kusoma dola za Songhai,Mwanamtapa,Ghana,Mali na akina Askia Mohamed-the great,Mansa K Mussa,sijui Timbuktu tunasahau historia yetu.Mimi nimesoma sayansi ila napenda sana Historia

    David V

    ReplyDelete
  18. yani huyu jamaa sijui analengo gani hasa, lengo si kueleza historia ya TZ, anasababu zake binafsi za udini, yuko UK lakini ndio wale jamaa wasiobadilika hata kidogo kuwa exposure hakujamsaidia kabisa, habari nzima tangu alipoianza imegawanyika sehemu kubwa mbili UDINI na HISTORIA ya Tanzania, sasa atufafanulie anachotaka kukisema au kukiandika ni kipi kati ya hivyo viwili, ukitaka kujua hata yeye mwenywewe hana amani na anayoongea ameshindwa hata kuweka ID yake tumjue yeye ni nani, siamini muislamu safi kabisa mwenye kuelewa dini inasemaje anaweza kuwa na mawazo kama yake, tunaomba utufafanulue unataka kusema nini? ili wachangiaji waelewe wanachangia hoja gani, huko uliko unatakiwa kubadilika ili ubadilishe wengine wenye mtazamo kama wako, itasaidia sana jamii, usiwe mtu yule yule before and after, wengi wanatamani nafasi uliyoipata yakua ughaibuni, wakitamani pia mabadiliko uliyonayo na uliyoyapata huko, hivyo leta mada iliyo wazi bila kuzungusha mpira ili usaidie jamii, hata rais wetu ni mwislamu msomi pia utasemaje? growup!!!!

    ReplyDelete
  19. Mimi sitaki kuzungumzia suala la dini lakini ni kweli upo umuhimu wa kuandika historia na kuwaweka wale wote waliochangia katika kufanikisha uhuru wa Tanganyika kwa hali na mali.

    Kama alivyozungumza mmoja hapo juu, nani atamfunga paka kengele? Jamani wenye taaluma ya uandishi jitoleeni mufanye hiyo kazi. Wengine ndiyo akina sisi tulioogopa umande tukaishia .... ah naona aibu hata kusema.

    ReplyDelete
  20. mimi nahisi mada ni nzito swala la idd amin hapa alipo kabisaa hiyo ni janja ya mwalimu kumtaka m7 aingie madarakani ilikuwaje watu uwapige hadi nyumbani kwao halafu huchagulie rais hiyo c sawa.dhuluma popote zipo hata ulaya uingeireza lazima uwe agrocanas ndio upate hata ujumbe wa serikali za mitaa

    ReplyDelete
  21. WADAU
    NINA FURAHA SANA KUWA MADA HII IMECHOKOZA WENGI. NDIVYO NILIVYOTEGEMEA. IMEAMSHA HISIA ZILIZOLALA, NA HIYO NI DALILI NJEMA. SIUDHIKI HATA NINAPOSHAMBULIWA BINAFSI BADALA YA MADA. MADA NDIYO INGESHAMBULIWA, NADHANI, NA SI MIMI MNDENGEREKO.
    KATIKA TZ YA AWAMU YA KWANZA, NINGESHUPALIWA KWA SABABU YA KUTOA MAWAZO YANGU, KWANI ZAMA ZILE HAZIKURUHUSU HILO. BAADA YA HAPO, KIONGOZI WA TZ ALIYEFUATA AKAACHA WAZI UHURU WA KUTOA MAONI. RUKSAAAA!
    KWA AJILI HIYO NILIDHANI NAMI NNA HAKI YA KUELEZA NINAYODHANI NI SAHIHI. HATA KAMA YOTE SI SAHIHI, NIHESHIMIWE, SABABU NNA UHURU WANGU. NA HII WALA SI KAMPENI YA KUCHAFUA AMANI, NISIELEWEKE VIBAYA.
    HARAKATI ZA KUMKOMBOA MWANAMKE ZILIANZA KWA MAONI MAKALI MAKALI.
    HARAKATI ZA KUIKOMBOA AFRIKA KUSINI ZILIANZA KWA VISHINDO VINGI.
    NAAMINI, KUTOKANA NA IDADI YA WATOA MAONI MPAKA SASA, HARAKATI ZA KUANDIKA HISTORIA MPYA, YA KWELI, YA KULE TULIKOTOKA NAYO ITABIDI IWE NA UKALI KWA SABABU, KAMA NILIVYOSEMA KATIKA UTANGULIZI, NADHANI KUNA WATU KWA MAKUSUDI WAMEEPUKA KUTWAMBIA KWELI!
    NDIO LEO HISTORIA YETU IMEJAA MAPUNGUFU.
    MIMI NILISOMA TZ. SIKUSOMESHWA CHOCHOTE JUU YA WAPIGANIA UHURU WETU.
    KWA NINI?
    KULIKUWA NA UBAYA GANI KUAMBIWA KWELI?
    NANI ALIIANDIKA HISTORIA?
    NANI ALITUNGA MTAALA?
    KWA NINI ALITUNGA UONGO UONGO?
    KWANGU MIMI UISLAMU NI MUHIMU KULIKO UTZ, KWA SABABU UISLAMU UNANISHURUTISHA KUITHAMINI NCHI YANGU NA WATU WAKE.
    DINI YANGU HAIPINGI CHEMBE HATA NDOGO YA UBINADAMU.
    DINI YANGU HAIRUHUSU UTAWALA WA MABAVU NA UONEVU. KINA SYKES WALIUONA UKWELI HUO. SIJUI KAMA KUNA WANAOJUA HIVI LEO KUWA BAADHI YA WATZ WALIZUILIKA KUMFUKUZA MKOLONI KWA SABABU WALILISHWA KASUMBA KUWA MKOLONI ALILETA DINI NA USTAARABU.
    HIVI MNAJUA KWA NINI ILIBIDI BABA WA TAIFA AKIMBILIE PWANI?
    DATA ZIPO WADAU, LAKINI MIMI NI MCHOKOZA MADA TU, NYIE OSHENI VINYWA.
    SIAMINI KUWA MADA YANGU INACHOCHEA, BALI INSHAALLAH ITALETA MAELEWANO ZAIDI.
    HARAKATI ZA VIJANA WA KIPALESTINA KUTUMIA MANATI NA KURUSHIA VIFARU MAWE NDIVYO VILIVOMFANYA MKE WA TONY BLAIR CU CONFESS KUWA ALIELEWA KWA NINI WALIFANYA VILE!! NA ALIJUA WAINGEREZA WENGI WANGEMPINGA, NA KWELI WALIMPINGA NA KUMZOMEA, LAKINI PALESTINA NA ISRAEL ZIMEBADILIKA SANA, NA MENGI WAMEAFIKIWA TOKEA KAULI ILE ILIPOTOKA.
    JAMAA MIMI MTU WA AMANI, ILA KWELI INAUMA! SICHOCHEI FUJO, NACHOCHEA UKWELI.
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  22. Mndengereko chemka chemka winter kali hiyo! tayarisha majibu bro michuzi aki update wewe una copy na kupaste tu. Du, kaaaazi kweli kweli. Jamii Forum umehama nini wewe???

    ReplyDelete
  23. Nyie wote mnaosema kuwa jamaa ni mdini, nyinyi hamjioni...?lazima azungumze...tukiwapa takwimu za udini mnazoziendeleza serikalini mtabisha, kodi tunalipa wote waislam na wakristu iweje leo kanisa mmejiwekea mkataba wa MOU na serikali?mwaka 1992 serikali iliwekeana mkataba rasmi na makanisa nchini ambapo serikali iliweka ahadi kadhaa, zikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya kuzipa taasisi za afya na elimu zinazomilikiwa na makanisa kwa ajili ya maendeleo yenu..na ktk makubaliano hayo waislam hawakualikwa na wala serikali haikuona haja ya kupata maoni ya waislam...ilihali kodi tukilipa wote..sasa tukisema nchi hii ni ya upande mmoja manjifanya eti tunaleta udini...taasisi za kiafya za kikristo hutumia fedha nyingi za walipa kodi wa tanzania ikilinganishwa na taasisi za serikali...matumizi ktk hospital za serikali mwaka 2009 - 2010..
    KILIMANJARO XRISTIA MEDICAL CENTRE(KCMC)2008/2009 TZS 6,030,736,000 2009/2010 7,507,132,100 Nikiorodhesha zote itakuwa mlolongo mkubwa...nitakupa jumla zote za kwa makanisa na taasisi zake...2008/ 2009. 40,518,946,000...2010/2011..46,624,820,500
    Kwa 2008/2009 Ni sawa na asilimia 53.8 ....2010/2011 ...asilimia 54.4
    wakati hospital na taasisi za huduma ya afya zinazomilikiwa na serikali zilipatiwa sh 39,151,552,700 sawa na asilimia 45.6...tukihoji mnaanza kutwambia sisi ndio wadini..iweje kodi yangu mimi kama muislam mnufaike nyinyi? Nyerere ndiye aliyetufikisha hapa...na ndio maana kanisa linataka limpe cheo cha mtakatifu...waislam huwa hatuna papara na maamuzi yetu..nyie jafanyeni..tu eti wadini..Mtake msitake asilimia 95 ya uhuru wa nchi hii umeletwa na waislam baada ya kuchoka kunyanyaswa na wakoloni wa kijerumani ambao walikuwa wakiwapendelea waziwazi wakristo..ndio maana babu zetu wakajikusanya ili kujikomboa..nyie aslimia kubwa mlikuwa mnapendelewa milikuwa mmesharidhika sasa iweje mdai uhuru na wakati mlikuwa huru?..sisi tutasema tuu mpaka kitaeleweka..! tutamfunga paka kengele...!

    ReplyDelete
  24. SUALA LA UDINI: Sio DHAMBI ni haki ya Kikatiba na miongoni mwa moja ya haki za binaadam ni Uhuru wa kuabudu,

    ISIPOKUWA ZAIDI YA HAPO NI MUHIMU KWA HUYO ANAYEITWA ''MDINI'' AHESHIMU NA KUTOA NAFASI KWA WATU WA IMANI ZINGINE:::
    --------------------------------------
    NIRUDI KTK MADA HUSIKA:ZAIDI YA KUPOTOSHWA KWA HISTORIA YA TANZANIA, PANA TASWIRA YA UPENDELEO WA DINI AU DHEHEBU MOJA KWA VITU HIVI:
    1.KATIBA YA TANZANIA ,INASEMA NCHI YETU HAINA DINI ILA WANANCHI WAKE NDIO WANA DINI, SASA JE SERIKALI YETU YA TANZANIA KUITAMBUA MAMLAKA YA KIDINI KAMA VATICAN, HUO SIO UPENDELEO WA UDINI?,UDHEHEBU? NA KUWA NJE YA MISINGI YA KATIBA?
    2.KUTOKUWAPA HAKI YA KUABUDU WENYE IMANI NYINGINE UHURU WA KUWA NA SHERIA YAO YA KIDINI (MAHKAMA YA KADHI) SIO KUPINDISHA KATIBA NA HAKI ZA BINAADAM?
    3.KUTOKUTOA NAFASI YA KUJIUNGA NA OIC SIO KUWANYIMA WATU HAKI ZA MAFAO YA KIUCHUMI KWA VILE OIC NI JUMUIA YA KUCHUMI NA SIO YA KIDINI KAMA VATICAN?
    (((NCHI INA RAIA WA DINI, MADHEHEBU NA IMANI MBALIMBALI NA WENGINEO HATA DINI HAWANA JE HAKI IMETENDEKA?)))
    --------------------------------------
    HITIMISHO: HISTORIA YA UHURU TANZANIA NA MATUKIO MUHIMU ''CHRONOLOGY ORDER'' VIMEPINDISHWA, HUKU DALILI ZA UPENDELEO WA UDINI/ UDHEHEBU UKIJIONYESHA WAZI.

    ReplyDelete
  25. Sioni kama kuna ujumbe sahihi sambamba na Kupigania Uhuru na Uislam. Kama lengo ni juu ya Uislamu sema tu kwa mada nyingine. Watu walipigania uhuru kwa uzalendo siyo kwa itikadi ya kiimani.

    Tafuta mada mwafaka, huu ni uchochezi. Tusherehekee miaka 50 ya Uhuru kwa upendo wa kitanzania na siyo dini gani ilifanya nini.

    Waliomng'oa nduli Amin watasema nini?

    Kama ni historia hata wewe waweza kuandika kwani kinakushinda nini? Hao unaowajua wanajua historia kawafuate ili upate cha kuandika tukusome. Unataka akuandikie nani? Huo ni uzandiki na unafiki.

    Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga mbele ndiyo ujumbe wa Taifa katika sherehe za miaka 50 za uhuru. Siyo kengele ya kanisa gani wala adhana ya msikiti gani. Acha uchochezi, kasome ili nawe uweze kuandika historia na upate nafasi unazolilia.

    ReplyDelete
  26. Mndengereko wa UK mboka kimya? Ume solvu tatizo la winter nini?

    ReplyDelete
  27. MNDENGEREKO wa UK winter sio issue kwake muhimu ameanzisha na sisi tumemalizia kwa comments hizo hapo juu (((HISTORIA YA UHURU WA TANZANIA IMEPINDISHWA HUKU ,MKIMWITA MNDENGEREKO 'MDINI' ilhali KUMEKUWA NA UDINI MKUBWA KWA DINI/DHEHEBU moja kupendelewa zaidi mfano UWEPO WA AMLAKA YA VATICAN ambao ni nje ya KATIBA YA NCHI-TANZANIA HAINA DINI)))

    ReplyDelete
  28. HISTORIA YA UHURU WA TANZANIA IMEPINDISHWA kama MNDENGEREKO alivyo lalamika ingawa kwa JAZBA..yeye sio ''MDINI'' ila MDINI NI YULE ALIYEFANYA HAYA HAPA CHINI:
    1.KUITAMBUA NA KURUHUSU UWEPO WA MAMLAKA YA VATICAN AMBAYO NI YA KIDINI HUKU KATIBA YA NCHI YA TANZANIA IKISEMA SERIKALI HAINA DINI.(((HATA KAMA MALIZIO LA KIPENGELE HICHO LINASEMA ''RAIA WAKE WANA DINI'' ITAKUWA WENYE DHEHEBU LAO NA DINI WAMEPENDELEWA DHIDI YA WATU WA IMANI ZINGINE))).
    2.KUMNYIMA UHURU WA KUABUDU MTU WA IMANI INGINE KWA KUIKATAA SHERIA YA DINI YAKE ''MAHAKAMA YA KADHI''
    3.KUKATAA KUINGIZA NCHI KATIKA JUMUIA YA KIUCHUMI OIC AMBAYO SIO YA KIDINI KUNAWANYIMA WATANZANIA WOTE HAKI KWA KUWA FAIDA ZAKE ZITAKUWA KWA WATU WOTE WANANCHI WA TANZANIA SIO KWA WATU WA DINI MOJA TU.

    ReplyDelete
  29. MNDENGEREKO GESI IMEKATA TENA NA WINTER IMEANZA KUKUNYANYASA. MAREKANI KUNA MIZAZAMO "SCHOOLS OF THOUGHT" NYINGI TU ZA HISTORIA, CIVIL WAR, NK NA WATU WANAANDIKA VITABU, JOURNAL ARTICLES NA KUSOMEA PHD KUTETEA HOJA ZAKO. KAMA UNA KIPYA CHA HISTORIA YA TANZANIA ANDIKA KITABU WASOMI KAMA SISI TUSIOTAKA FITNA FITNA TUKISOME. FANYA MAMBO KISOMI KAMA MTU ALIYE UK - USI BEHAVE KAMA MTU WA KIJIJINI. MEANWHILE PIGA BOXI TAFUTA HELA YA KULIPIA GESI. UKIPATA JOTO ITAKUSAIDIA

    ReplyDelete
  30. WEWE Anymous wa 29 siku ya Wed Nov 09, 09:46:00 PM 2011 HAPA SIO MNDENGEREKO KUWA GESI IMEMKATIKIA ::::ZIMETOKA COMMENTS ZENYE DATA ZA UKWELI NA SIO KWAMBA MTU ANATAFUTA PhD. ILA UNATOLEWA UKWELI WA MAMBO ,TUMEZOEA SANA UTAMADUNI WA KIMAPOKEZI BILA KUFANYIA KAZI MAMBO ''THINK TANK'' NA PENYE UKWELI UONGO HUJITENGA!!!

    ReplyDelete
  31. MIMI NI MWANA TAALUMA NA NDIO NAYEMKANDIA MNDENGEREKO WA HUKO UK KWAMBA KAKOSA GESI! TOFAUTI ZA KIMAWAZO KWENYE HISTORIA ZIKO SISI TUNAITA "SCHOOLS OF THOUGHT". UNAPOLETA SCHOOL OF THOUGHT YAKO YENYE MAMBO SENSITIVE KAMA YA KIDINI INABIDI UWE NA HOJA ZA NGUVU ZINAZOELEWEKA. HAYA MAMBO MNDENGEREKO ANAYOLETA NI MAPYA KWETU NA TUMEZOEA KUSOMA FITNA FITNA NA SISI HATUTAKI, NDIO MAANA NIKAMWAMBIA KAMA ANA MSIMAMO MPYA KUHUSU "RE-WRITING TANZANIAN HISTORY" ATOE KITABU AU JOURNAL. MIMI KAMA MSOMI HOJA ALIZOTOA BADO NAZIJA NISHAWISHI - SANA SANA NAONA ZA KICHOCHEZI TU. NI SAWA SAWA NA MIMI KUIBUKA SASA NA KUSEMA WATU WA DINI FULANI WALIHUSIKA KATIKA LILE JARIBIO LA KUPINDUA SERIKALI NA KUMUUA RAIS NYERERE, HALAFU NI-QUOTE SOURCE MBILI TATU KUTETEA HOJA YANGU! UNLESS NATOA DATA ZA KUTOSHA KUTETEA HOJA YANGU NA IKIWEZEKANA NAANDIKA KITABU, THEN HUU UTAKUWA NI UCHOCHEZI TU....!!! NA HAPO NDIO UNAWEZA TOFAUTISHA MSOMI NA MTU ASIYESOMA...!!!

    ReplyDelete
  32. KWAKO MWANATAALUMA UNAYEMLALAMIKIA MNDENGEREKO:::::::::::::::::::::::
    -----------------------------------

    MIMI SIO MWNATAALLUMA KAMA WEWE, ILA MIMI NI ANLYST.

    SASA HAPA CHINI NASASAMBUA MZIZI WA MATATIZO:
    -----------------------------------
    1.UCHAMBUZI KUWA, KTK MAMBO SENSITIVE YA KIDINI HOJA ZA NGUVU UNAZOTAKA ILI KUDHIHIRISHA UKWELI KUWA KUNA UGANDAMIZAJI WA KIDINI IMESHAZUNGUMZWA NA WACHANGIAJI HAPO JUU KWA USHAHIDI KAMILI KAMA HIVI:
    -SERIKALI KUWA NA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA NA MAMLAKA YA KIDINI (VATICAN)INAYO WAKILISHA DHEHEBU MOJA TU LA KIKRISTO LA KATOLIKI, HUKU KATIBA YA NCHI IKISEMA KUWA TANZANIA HAINA DINI ILA WATU WAKE WANA DINI
    -SERIKALI KUEGEMEA UPANDE MMOJA NA KUBANA HAKI ZA WATU WA DINI INGINE ISIPATE FURSA YA SHERIA ZA KIDINI, WAKATI KATIBA YA NCHI NA HAKI ZA BINAADAMAU ZIKITOA UHURU WA KUABUDU.
    -SERIKALI KUKATAA KUINGIA KTK JUMUIA YA KIUCHUMI OIC ILI KUIRIDHISHA DINI FULANI NA HUKU KUKWAMISHA UPATIKANAJI WA MANUFAA YA KIUCHUMU KWA UANACHAMA WA JUMUIA HIO, WAKATI JUMUIA YA OIC NI YA KIUCHUMI SIO YA KIDINI KAMA VATICAN. MFANO MSUMBIJI NI MWANACHAMA WA OIC NA INA INADI KUBWA YA WAKRISTO KULIKO DINI ZINGINE NA KILA MWAKA INA NUFAIKA NA GAWIO LA US$ 6 BILLION KUTOKA KTK OIC.

    SASA MWANATAALUMA UNATAKA UZITO GANI WA HOJA ZA MSINGI ZISIZO NA FITNA FITNA ZAIDI YA USHAHIDI HUO AMBAO NI HALISI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...