![]() |
Marehemu Mama Mwingira enzi za uhai wake |
Imetimia Mwaka
mmoja tangu utuage Mama. Ni simanzi
isiyoelezeka! Kila kukicha tunaona kama ndoto Mama.
Ni vugumu kukubali hili pamoja kwamba ni mwaka sasa…Tunakupenda mama, tunakukumbuka sana, Mama yako Sabina anakukumbuka sana, tunamlea kwa Upendo wote mama.
Ni vugumu kukubali hili pamoja kwamba ni mwaka sasa…Tunakupenda mama, tunakukumbuka sana, Mama yako Sabina anakukumbuka sana, tunamlea kwa Upendo wote mama.
Mama ulijitoa kwa kila hali hadi kufa kwa ajili
yetu Watoto wako (Upendo, Edmund, Josephine,Sabina, Cassian, Wilfred and
Cecilia).Tunakumbuka mafunzo yako ya
“Upendo usio na masharti “na mshikamano.
Tunakuombea Mama nawe uzidi kutuombea. Tutakuenzi Daima Milele ….
Asante sana
sana Mama!!
Wajukuu wako (Gladys, GloriousMary, Edmond, Andreas, Crystaline,
Cassian, Olivia na Prince John) wanauliza
“bibi mbona hurudi ??”
Unakumbukwa pia
na shemeji, wifi, wadogo zako, marafiki, ndugu,Majirani na Jamaa wote Mama.
Sote tunabubujikwa na machozi mazito Mama.
Familia ya Marehemu
John na Mary Mwingira wa Upanga ,Familia ya Dr Edmund Ndalama wa Kunduchi ,Dar
salaam, pamoja na ndugu na jamaa wote wanapenda kuwaalika wote kwenye Misa Takatifu
itakayofanyika Tarehe 19 Novemba 2011,Saa 5 kamili asubuhi, Kunduchi
SEAMIC road plot 390/1, (Nyumbani kwa Dr
Ndalama.)
Karibuni wote tumuombee
Mpendwa wetu Mary John Mwingira.
RIP mama! Ulikuwa mtetezi wa wanyonge
ReplyDeleteRIP mama Mwingira
ReplyDeletemungu aipumzishe roho yako mahali pema peponi, daima tunakukumbuka mkwe wetu tunaona kama umesafiri na siku moja utakuja tutembelea kama ilivyokuwa kawaida yako.
ReplyDeletePole sana watoto wa Mama Mwingira. RIP mama.
ReplyDelete