Jumuiya ya Watanzania Rome (TZ-RM) inayofuraha kuwakaribisheni wanajumuiya wote kwenye mkutano mkuu wa kufunga mwaka wa Jumuiya siku ya tarehe 19th Nov. 2011 kwenye ukumbi uliopo mtaa wa Via Cassallatico 6, maeneo ya Cassia mjini Rome, kuanzia saa tisa jioni mpaka saa tatu usiku.
Kwenye huu mkutano, wanajumiuya kwa pamoja, watajadili maswala mbalimbali kama vile mafanikio na matatizo yaliyojitokeza kwenye mwaka mzima wa 2011 na kisha kutafuta mbinu mpya za kuimalisha jumuiya.
Baada ya Mkutano kutakuwa na chakula na mziki kwaajiri ya kujipojingeza kwa kumaliza mwaka wa jumuiya. Kwa wale wote watakaopenda kushiriki kwenye mkutano huu, mnaombwa kuwasiliana na katibu wa jumuiya ndugu Andrew Chole Mhella kwa kupitia namba hii watanzaniaroma@yahoo.it,
au kwa e-mail hii, au kwa kutembelea blog ya jumuiya,
Nyote mnakaribishwa.
Andrew Chole Mhella
katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome
Andrew Chole Mhella
katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome
NDUGU ZETU HUKO ITALY NA UGHAIBUNI KWA UJUMLA::::::::::::::::::::::::
ReplyDelete-----------------------------------
Tushirikiane kwa pamoja ili kujikwamua wote mjaribu kufikiria ni nini na rahisi chenye TIJA cha kufanya baina yetu na nyinyi huko ili tulisukume gurudumu la maendeleo badala ya kushiriki shughuli haramu na zisizo rasmi kama BIASHARA YA MADAWA, WIZI WA BENKI, UHALIFU na UCHANGU KWA WANAWAKE...TUITANGAZE TANZANIA VIZURI!