Mwanamuziki mahiri nchini Kenya ajulikanae kwa jina la JAGUAR (pili kulia) ,akiwasili nchini Tanzania tayari kwa kuangusha bonge la shoo kwenye tamasha la BODA KWA BODA BEACH CONCERT.

Kuzungumzia na uthibitisho wa ujio wa Mwanamuziki huyo Dar,Meneja wa Masoko wa kampuni ya G5 CLICK COMPANY,Desy Ernest amesema kuwa,Mwanamuziki Jaguar kutoka nchini Kenya anatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la BODA KWA BODA BEACH CONCERT litalofanyika kaika fukwe ya Mbalamwezi Beach,Mikocheni jijini Dar Es Salaam LEO majira ya saa moja jioni huku akisindikizwa jukwani na wasanii wakibongo wakiwemo Sumalee,GodZilla,Country Boy & Stamina,Young D,Beka na wengineo wengi tu

Desy Ernest amesema kuwa mpaka sasa mambo yanakwenda sawa bin sawia,na kwamba shamra shamra za BODA KWA BODA BEACH CONCERT zitakuwa tofauti na zenye msisimko mkubwa, ambalo ni kubwa katika anga ya burudani ndani ya Tanzania.

Jaguar awasihi mashabiki wake kujitokeza kwa wingi ilikukamilisha mpango mzima wa BODA KWA BODA BEACH CONCERT.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...