Mkurugenzi mkuu wa Lucas Construction na Mzee Lucas Tarimo (pichani) aliekuwa na makazi yake Moshi na Dar es Salaam alifariki Dunia Tarehe 29/10/2011 jijini Nairobi nchini Kenya. Kihistoria na kazi zake Marehemu Lucas Tarimo alijiunga na kiwanda cha Ngozi mkoani Kilimanjaro mwaka 1969, kama afisa mwajiri,na baadaye alijiunga na kiwanda cha magunia Mkoani Kilimanjaro 1972,akiwa kama afisa mwajiri.

(ADMINISTRATOR) Mwaka 1976 marehemu Lucas Tarimo alijiunga na kiwanda cha Tanzania Gemstone Mkoani Kilimanjaro kama Afisa Mwajiri.

Mwaka 1979 marehemu Lucas Tarimo alifungua kampuni yake ya Ujenzi ''LUCAS CONSTRUCTION” ambapo alikuwa Mkurugenzi mtendaji. Pia Marehemu Lucas Tarimo alifungua kampuni ya TAN OPTIC mwaka 1985 ambayo ilikuwa ni kampuni ya kutengeneza miwani, akiwa mwanahisa mmojawapo katika kampuni hiyo. Marehemu pia alishawahi kushika Umeya mji wa Moshi.

Marehemu Lucas Stambuli Tarimo alizaliwa tarehe 4/12/1936 na alifariki Tarehe 29/10/2011 Nairobi nchini Kenya.

alishapata matibabu katika Hospitali za nairobi - Kenya. India na Dar es Salaam. Mipango ya mazishi inafanyika Moshi Shant Town na Dar es Salaam Mikocheni Magorofa ya TPDC na Mzee wetu atazikwa Huko Tarakia Rombo Tarehe 05/11/2011

Bwana alitwaa na Bwana ametwaa, jina la Bwana litubariki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. RIP Mzee, Poleni sana Julius Tarimo and the family
    -Ludo

    ReplyDelete
  2. RIP mzee Tarimo. Nafikiri msiba ulitokea tarehe 29/10/2011 na siyo 29/11/2011. Kosa kidogo kwenye kuandika.

    ReplyDelete
  3. Alifariki tarehe 29/10/2011 badala ya tarehe 29/11/2011.

    ReplyDelete
  4. Poleni sana familia ya Lucas.RIP Lucas.

    ReplyDelete
  5. Poleni sana, but ni kama mnatania maana kama alikufa tr 29/11/2011 bado hajafa. Lakini ankal kwanini msisome ujumbe kabla hamjautuma? So shame

    ReplyDelete
  6. Jamani, umakini wa habari. Mbona tarehe imekaa vibaya. leo ni tarehe 2 Nov 2011, inakuaje tarehe hapo ni 29 Nov 2011. Rekebisha bwana.

    ReplyDelete
  7. Poleni sana familia ya Lucas Tarimo.May he rest in peace.Tumesali na huyu mzee jumuiya kwa miaka mingi.An outstanding man.

    ReplyDelete
  8. RIP MZEE LUCAS TARIMO.

    ReplyDelete
  9. Poleni kwa msiba ila tu tarehe aliyofariki 29/11/2011 haijafika kwani leo ni tarehe 02/11/2011

    ReplyDelete
  10. Poleni sana Familia ya Mzee Tarimo.Bahati mbaya tarehe ya kufariki imeandikwa ni 29/11/2011 nafikili imekosewa.

    ReplyDelete
  11. tarehe ya kifo imekosewa, naamini mmemaanisha ni tarehe 29/10/2011

    ReplyDelete
  12. May almighty God rest His soul in peace.

    Heartfelt condolences to the entire Tarimo family.

    Nitesh and family,
    Moshi

    ReplyDelete
  13. Tarehe 29/11/2011 mbona bado haijafika?

    ReplyDelete
  14. maskini R.I.P mzee lucas, du nakumbukuka tulikuwa tunapita kwake kwenda kuchota maji chemchem kwa waliokaa moshi miaka hiyo wanapajua,

    ReplyDelete
  15. Poleni wote walioguswa na msiba huo - Thecla, Thadei, Theodore na wengine.
    Mwereni (Moshi) primary school mate

    ReplyDelete
  16. POLENI SANA FAMILIA YA TARIMO KWA MSIBA. NAKUMBUKA WAKATI YUKO NAIROBI KWA MATIBABU MIMI NA MUME WANGU PIA TULIKUWA HUKO KWA MATIBABU NA HOSTEL AMBAYO TULIKUWA TUNALALA "FLORA HOSTEL- NGONG' ROAD FIFTH AVENUE TULIKUWA NA MKE WAKE NA MTOTO WAKE WA KIUME. POLENI SANA, MUNGU AWATIE NGUVU KATIK KIPINDI HIKI KIGUMU.

    ReplyDelete
  17. RIP Mr Lucas Tarimo,
    Our sincerley condolences to Mrs Tarimo, Thadei,Tecla,Theo,Ernest William and Cesar and all other members of the family at this very difficult time of your loss. Our thought and prayers are with you all.RIP Amen.
    The Shao's family of Rau Moshi

    ReplyDelete
  18. Wakina-Tarimo, na wakina-Makundi poleni sana kwa msiba wa Mzee wenu/wetu. Mungu amuweke mahali pema peponi Mzee Tarimo.
    Wenu Wakina-Kaaya

    ReplyDelete
  19. Poleni sana familia ya Lucas Tarimo kwa msiba. Rest in Peace Mzee Lucas Tarimo.

    By
    Jirani miaka ya 80-90 Moshi.

    ReplyDelete
  20. Jamani Mzee Lucas,alikuwa anatupaga hela na lift jamani wakati tunasoma Mawenzi Sec. Alikuwaga mpole na mwenye roho nzuri.Mungu ampe pumziko la milele.

    ReplyDelete
  21. mzee lucas alikuwa mpole poleni wowe kwa msiba.

    ReplyDelete
  22. RIP grand patron! still cant believe you are gone!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...