Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kulia) akitoa ushauri wa kitaalamu na uzoefu kwenye Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala wakati wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Katiba ya Mwaka 2011 ambapo mwanasheria huyo mkongwe amewataka watanzania wote kwa ujumla kuwa kitu kimoja katika jambo hili.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala,Mh. Pindi Chana
Wajumbe na wataalam mbalimbali wa Kamati ya Sherai, Katiba na Utawala, Kamati ya Mashirika ya Umma, Kamati ya Fedha za Serikali za Mitaa na Kamati ya Hesabu za Serikali wakiwa katika mijadala mikali-mikali leo.Picha zote na Prosper Minja-Bunge.
Mmmmmhhhhhnnnnn Kaka Misupu
ReplyDeleteMbona kila mjadala unaoripotiwa uko mjini tu...ivi hiii miji yetu ina watu wangapi kuliko sisi tulio vijijini? Au ndo ushakuwa mradi...manake najua hapo kila alotoka anaposho yake ya siku...je sisi wakulima na tusio wafanyakazi tutajadili lini katiba mpya??????????Au katiba mpya ni ya kwa wale wafanyakazi wa mijini na wengine walio town na sisi tulio village ndo tusahau...tusubiri wenzetu mtuamulie....!!!!!!
Asanteni kwa kutusahau...naona Tanzania ina wenyewe...na sisi hatumo.....!!!!