Mkurugenzi mkuu wa Lucas Construction na Mzee Lucas Tarimo (pichani) aliekuwa na makazi yake Moshi na Dar es Salaam alifariki Dunia Tarehe 29/10/2011 jijini Nairobi nchini Kenya. Kihistoria na kazi zake Marehemu Lucas Tarimo alijiunga na kiwanda cha Ngozi mkoani Kilimanjaro mwaka 1969, kama afisa mwajiri,na baadaye alijiunga na kiwanda cha magunia Mkoani Kilimanjaro 1972,akiwa kama afisa mwajiri.
(ADMINISTRATOR) Mwaka 1976 marehemu Lucas Tarimo alijiunga na kiwanda cha Tanzania Gemstone Mkoani Kilimanjaro kama Afisa Mwajiri.
Mwaka 1979 marehemu Lucas Tarimo alifungua kampuni yake ya Ujenzi ''LUCAS CONSTRUCTION” ambapo alikuwa Mkurugenzi mtendaji. Pia Marehemu Lucas Tarimo alifungua kampuni ya TAN OPTIC mwaka 1985 ambayo ilikuwa ni kampuni ya kutengeneza miwani, akiwa mwanahisa mmojawapo katika kampuni hiyo. Marehemu pia alishawahi kushika Umeya mji wa Moshi.
Marehemu Lucas Stambuli Tarimo alizaliwa tarehe 4/12/1936 na alifariki Tarehe 29/10/2011 Nairobi nchini Kenya.
alishapata matibabu katika Hospitali za nairobi - Kenya. India na Dar es Salaam. Mipango ya mazishi inafanyika Moshi Shant Town na Dar es Salaam Mikocheni Magorofa ya TPDC na Mzee wetu atazikwa Huko Tarakia Rombo Tarehe 05/11/2011
Bwana alitwaa na Bwana ametwaa, jina la Bwana litubariki
RIP Mzee, Poleni sana Julius Tarimo and the family
ReplyDelete-Ludo
RIP mzee Tarimo. Nafikiri msiba ulitokea tarehe 29/10/2011 na siyo 29/11/2011. Kosa kidogo kwenye kuandika.
ReplyDeleteAlifariki tarehe 29/10/2011 badala ya tarehe 29/11/2011.
ReplyDeletePoleni sana familia ya Lucas.RIP Lucas.
ReplyDeletePoleni sana, but ni kama mnatania maana kama alikufa tr 29/11/2011 bado hajafa. Lakini ankal kwanini msisome ujumbe kabla hamjautuma? So shame
ReplyDeleteJamani, umakini wa habari. Mbona tarehe imekaa vibaya. leo ni tarehe 2 Nov 2011, inakuaje tarehe hapo ni 29 Nov 2011. Rekebisha bwana.
ReplyDeletePoleni sana familia ya Lucas Tarimo.May he rest in peace.Tumesali na huyu mzee jumuiya kwa miaka mingi.An outstanding man.
ReplyDeleteRIP MZEE LUCAS TARIMO.
ReplyDeletePoleni kwa msiba ila tu tarehe aliyofariki 29/11/2011 haijafika kwani leo ni tarehe 02/11/2011
ReplyDeletePoleni sana Familia ya Mzee Tarimo.Bahati mbaya tarehe ya kufariki imeandikwa ni 29/11/2011 nafikili imekosewa.
ReplyDeletetarehe ya kifo imekosewa, naamini mmemaanisha ni tarehe 29/10/2011
ReplyDeleteMay almighty God rest His soul in peace.
ReplyDeleteHeartfelt condolences to the entire Tarimo family.
Nitesh and family,
Moshi
Tarehe 29/11/2011 mbona bado haijafika?
ReplyDeletemaskini R.I.P mzee lucas, du nakumbukuka tulikuwa tunapita kwake kwenda kuchota maji chemchem kwa waliokaa moshi miaka hiyo wanapajua,
ReplyDeletePoleni wote walioguswa na msiba huo - Thecla, Thadei, Theodore na wengine.
ReplyDeleteMwereni (Moshi) primary school mate
POLENI SANA FAMILIA YA TARIMO KWA MSIBA. NAKUMBUKA WAKATI YUKO NAIROBI KWA MATIBABU MIMI NA MUME WANGU PIA TULIKUWA HUKO KWA MATIBABU NA HOSTEL AMBAYO TULIKUWA TUNALALA "FLORA HOSTEL- NGONG' ROAD FIFTH AVENUE TULIKUWA NA MKE WAKE NA MTOTO WAKE WA KIUME. POLENI SANA, MUNGU AWATIE NGUVU KATIK KIPINDI HIKI KIGUMU.
ReplyDeleteRIP Mr Lucas Tarimo,
ReplyDeleteOur sincerley condolences to Mrs Tarimo, Thadei,Tecla,Theo,Ernest William and Cesar and all other members of the family at this very difficult time of your loss. Our thought and prayers are with you all.RIP Amen.
The Shao's family of Rau Moshi
Wakina-Tarimo, na wakina-Makundi poleni sana kwa msiba wa Mzee wenu/wetu. Mungu amuweke mahali pema peponi Mzee Tarimo.
ReplyDeleteWenu Wakina-Kaaya
Poleni sana familia ya Lucas Tarimo kwa msiba. Rest in Peace Mzee Lucas Tarimo.
ReplyDeleteBy
Jirani miaka ya 80-90 Moshi.
Jamani Mzee Lucas,alikuwa anatupaga hela na lift jamani wakati tunasoma Mawenzi Sec. Alikuwaga mpole na mwenye roho nzuri.Mungu ampe pumziko la milele.
ReplyDeletemzee lucas alikuwa mpole poleni wowe kwa msiba.
ReplyDeleteRIP grand patron! still cant believe you are gone!
ReplyDelete