Mshindi wa Pili wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Tanzania- 2011, Mwandiwe Makame Kali kutoka Chaani, Wilaya ya Kaskazini A, Unguja, akipokea zawadi ya Sola kutoka kwa Afisa Kampeni na Utetezi, Lilian R. Kallaghe wa Shirika la Oxfam (kulia), mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Khadija Ally Juma wa Shirika la Actionaid, ambao walishirikiana na Oxfam kuendesha shindano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Unguja , Mh. Riziki Juma Sinai (wa pili kushoto) akimpongeza Mshindi wa Pili wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula-2011, Bi Mwandiwe Makame Kali (katikati). Shindano hilo liliandaliwa na Oxfam na washirika wake kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake wafugaji na wakulima wadogo katika kuchangia uhakika wa chakula nchini. Jumla ya wanawake takriban 7,000 walishiriki katika shindano hilo. Wengine pichani ni Khadija Ally Juma (wa kwanza kushoto-Actionaid). Wa kwanza kulia ni Lilian R. Kallaghe, Afisa Kampeni na Utetezi wa Shirika la Oxfam na kulia kwake ni Dorcas Erskine (Actionaid).
DAADA MWENYE SURUALI SKINI TAITI SALAM ZAKO.
ReplyDelete