Jana Mwalimu Mwanaisha Kikwete alikula Nondozz ya BA. Education kutoka Chuio Kikuu Huria -OUT mahafali yaliyofanyika Kibaha na baadae kukafanyika Maulid Nabii iliyofuatia na dhifa ya chakula nyumbani kwao Mwalimu Kikwete huko Temeke ambayo pia ilihudhuriwa na wifi yake Mama Salma Kikwete.
Mwalimu Mwanaisha akiwa na kaka zake Mdau Charles Semiono kushoto na Mdau Abdul Issa Kihenya kulia.
Ndugu, jamaa na marafiki wakimpongeza Mwalimu
Watoto wa madrasa wakighani qasda wakati wa sherehe hiyo
Wifi yake Mama Salma Kikwete akitoa pongeza na nasaha kuwahimiza kinamama nchini kufuata mfano wa Mwalimu Mwanaisha kuwa Elimu haina mwisho na kwamba Wanawake wakiamua wanaweza!
Picha na Mdau Ankal Midladjy Maez
Hongera Mwalimu, lakini ankal ningependa kujua huyu nia Mwanaisha Kikwete au Zainab Kikwete mbona siku ya graduation kule kibaha waliita Zainab Kikwete na sio Mwanaisah.
ReplyDeleteHongera sana tena sana dada Mwanaisha, hukujali umri wako ukaamua kujiendeleza mpaka kufikia hapo ulipo, heshima ya mwanamke ni elimu.
ReplyDeleteSAFI SANA SHEREHE ZA NAMNA HII. SIO KILA SIKU MZIKI TU MAPOMBE,
ReplyDeleteHongera Mwl. Mwanaisha Kikwete kwa kujua umuhimu wa Elimu na kuweka msisitizo hadi kupata Shahada!!!.
ReplyDelete