Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu (MB) akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi maonyesho ya 9 ya SIDO ya nyanda za juu kusini inayoshirikisha mikoa ya Rukwa, Iringa na Mbeya. Kulia kwake anayeshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana. Maonyesho hayo yanafanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa  kwa kushirikisha wajasiriamali kutoka zaidi ya mikoa 14 nchini na wengine kutoka nchi jirani za Kenya na Burundi.


Naibu Waziri akisalimiana na Meneja wa SIDO Mkoa wa Rukwa ambao ndio wenyeji Ndugu Martin Chang'a mara baada ya kuwaili katika uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa kwa ajili ya kuzindua rasmi maonesho hayo. Kwa mujibu wa Meneja huyo wa SIDO maonyesho hayo yatadumu kwa mda wa siku 6 kuuanzi tarehe 9-14 ambapo ndio itakuwa kilele na atakefunga maonesho hayo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.  

Mkurugenzi Mkuu wa SIDO nchini Ndugu Mike Laizer akifafanua jambo kwa Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu kwenye banda la SIDO. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana.

Naibu Waziri akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Nyalandu amepiga suti yenye rangi ya chama cha "Nguvu ya Umma"

    ReplyDelete
  2. umma wa wachaga sio mimi wala ukoo wangu wa mbali wala wakaribu ambao tuko kama 100 hivi. Nyie wajinga kwel. Fanyeni maandamano basi kama wanaume kweli. Uhuni tu.

    ReplyDelete
  3. CCM hakuna kulala maandamano yanajibiwa na maandamano tuone sasa. Maana kama kuna umma sasa CCM wanao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...