Familia ya Bryson K.B Masambaji,kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru ndugu, jamaa, majirani na marafiki wote waliofanikisha shughuli zote za msiba wa Marehemu baba yetu Mzee Bryson K.B Masambaji (pichani), ambaye alifariki katika hospitali ya mkoa Morogoro tarehe 14/Octoba/2011 na hatimaye kuzikwa tarehe 16/Octoba/2011 kijijini kwao Usangi Mwanga Kilimanjaro.
Tunapenda kutoa shukrani nyingi kwa Madktari waliokuwa wakimuudumia na wachungaji wote waliokuwa wakija na kututakia heri ,pia wachunagiji wote wa usharika wa usangi wailaya ya mwanga na morogoro, majirani wote, ndugu, jamaa na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na pia kushiriki katika shughuli zote za mazishi. Shukrani kwa wote mliofika nyumbani katika kutufariji, mliotupigia simu au kutuma ujumbe kwa njia zingine kwa nia ya kutufariji na kututia nguvu. Asanteni sana na MUNGU awabariki.
Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee, tunaomba shukrani hizi mzipokee wote mliohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya msiba huu wa mpendwa baba yetu Bryson K.B Masambaji hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia katika shughuli zenu za kila siku.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe [Ayub. 1:21]
Amen
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...