Jamani, hivi mnalikumbuka hili shairi?
kama mlisahau basi enjoy!!!
Mdau
-------------hadithi uliyongoja leo ninakuletea
Alitoka siku moja njaa aliposikia
njaa aliposikia sungura nakuambia
Siku hiyo akaenda porini kutembelea
akayaona matunda mtini yameenea
sungura akayapenda mtini akasogea
Mtini akasogea sungura nakuambia
sungura karuka ruka lakini hakufikia
matunda hakuyashika mikononi hakutia
hakika alisumbuka nguvuze zikapungua
nguvuze zikapungua sungura namwambia
SIZITAKI MBICHI HIZI, sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
Matunda akalilia Sungura nakuambi
Tuma salamu kwa watu watatu.............
ReplyDeleteVema sana mdau kwa kutukumbusha mambo ya shairi la sungura.Tupe na ile ya Karudi baba mmoja na lile la Azimio la Arusha.
ReplyDeletekamili hii hapa
ReplyDeleteHadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia
Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.
Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.
Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.
Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mk-Ia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.
“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.
Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.
Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.
DUUUUUUUUH UMETUKUMBUSHA MBALI SAAAAAAN
ReplyDeleteKarudi baba mmoja toka safari ya mbali
ReplyDeletekavimba yote mapaja na kutetemeka mwili
watoto wake wakaja ili kumtaka hali
wakata na kauli iwafae maishani
Akatamka mgonjwa ninaumwa kwelikweli
hata kama nikichanjwa haitoki homa kali
roho naona yachinjwa kifo kinanikabili
kama mwataka kauli semeni niseme nini
endeleza ...
Da kweli watu mna hazina - umenifanya nikumbuke mengi na watu wengi waliotutangulia mbele ya haki. Mara baada ya CCM kuzaliwa kuna wakati tulikuwa tukiimba kibwagizo cha "CCM,CCM, CCM...!" kwenye huu mwimbo. Jamani nyimbo za mchaka mchaka vipi, hasa JKT tukumbushane jamani...
ReplyDeleteWao, mnanikumbusha darasa la nne n shule ya msingi ya Jamuhuri DSM. Pia inaleta kumbukumbu ya waliotutangulia kama mwalimu wangu kipenzi Salama Thabit/Salama Mfamau, Mwl Tausi Mchopanga, Classmate wangu John Njakale.
ReplyDeleteMila awalaze mahala pema peponi. Amen
ebwana eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee du we mdau unakumbukumbu ile mbaya vipi ile hadithi ya kibanga ampiga mkoloni wadau mnaikumbuka au pazi mtoto shujaa du kweli tumetoka mbali
ReplyDeleteLugha ingefundishwa mashuleni kwa kutumia tungo kama hizo, nadhani elimu ingekuwa juu. Wakaja wale wajanja, wenye akili potovu,
ReplyDeleteWakaanza zao tungo, zenye siasa za chuki.
Wakapandikiza tungo na hadithi za kilimo,
huku wao hawalimi, bali wezi wa kalamu.
Wengi wao wadiriki, kusomesha watoto ng'ambo, hali wao wasimama kudanganya wa masikini.
Twataka karumekenge, na riwaya za abunwasi, tumechoka longo longo na siasa za kichina.
ASANTE KWA KUNIKUMBUSHA MBALI,NAOMBA ANAYELIKUMBUKA SHAIRI LA IDD AMINI JASUSI JOKA HILI NI JOKA KUU,ALIMWAGE HAPA PIA
ReplyDeleteEbwaeee!!!! hiyo haitoshi hata watoto wavivu walikua na shairi lao
ReplyDeleteSIKIRI MIMI MASIKINI,
UVIVU WANGU NYUMBANI
UKIWA HUU NJIANI
NAKUFA HAPA KWA NINI?
Hapo Mdau umepiga Pentagon...SIZITAKI MBICHI HIZI NI NGANO YA WAZANZIBAR KUUKATAA MUUNGANO HUKU WAKIJUA WAO NDIO WANANUFAIKA NAO SANA TU!!!!
ReplyDelete<<<>>>
Dah umetukumbusha mbaaaali sana mpaka chozi limenitoka! those were he OLD good days that will NEVEr roll back! Aiseee ..kisa cha madenge na mandawa ! HERI MIMI SIJASEMA ! BABU ANAPULIZA CHAI KIJANNJA KWA KUSEMA WATOTO NAWASIFUUUU! HII NYUMBA INA SIAFUUUUU! DAH! those were th days
ReplyDeletenamshukuru sana mdau aliyetukumbusha hizi tungo, hii ndio iliyokuwa elimu sio sasa hivi. mimi nilisoma kijijini lakini shairi hili niliimba darasa la tatu na la nne, tena wakati huo kitabu kimoja wanafunzi watatu, lakini leo hii kila mtu anatoa kitabu mitahala haieleweki mara masomo ya sayansi kimu yameondolewa matokeo yake watu wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika,lakini hata kupika kufua hawajui. Tungo hizi zilitufundisha maisha ukakamavu na mambo mengine sasa hivi sijui hata wanasoma nini maana ukienda sekondari za kata mtu hata jina lake hawezi kuandika, ukimuuliza Kigoma iko wapi anakuambia ipo nchi za njee. Jamani turudie mitaala ya nyuma na jiografia tufundishe watoto waijue hata dunia ikoje.
ReplyDeleteNamshukuru sana Mdau kwa Kutukumbusha ila na wadau wa elimu waangalie kwa mtazamo tofauti ili tuboreshe elimu
tuwekeeni na sikukuu ya sabasaba ilianza julai saba, wakoloni kuwakaba, sikukuu ya sabasaba,ooooooo, jamani wanalijua zaidi waendeleze. maana nalo zuri sana
ReplyDeleteJAMANI EE MBONA MMELISAHAU SHAIRI HILI
ReplyDeleteKarudi baba mmjoa toka safari ya mbali
kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja aili kumtaka hali
wakakata ta shauri liwafae maishani
Asante wadau mlioweza kukumbuka mashairi mengine...Zamani tulikuwa tunafundishwa bwana hadi leo mashairi yako vichwani..kama alivyosema mdau mmoja hapo juu wakaja wajanja wakaanzisha nyimbo za siasa..
ReplyDeleteSIKIRI MIMI MASIKINI..Weee nilikuwa naogopa kweli wimbo huo..Watoto wasingeweza kuzamia mijini kama ilivyo sasa
David V
EE jamani blog ya Michuzi ina mambo,,,EE kweli kiswahili ni lugha ya kujivunia sana,nawashangaa hao wanaopenda kuvuruga kiswahili eti wanajifanya hakuna maneno ya kiswahili kukamilishia sentensi zao,,wanaweka kithungu,,yaani Swanglish,yaani huwo ni ushamba wa hali ya juu,,,hayo mashairi nani aliyatunga jamani,,basi kamilisheni na hizo tungo zingine Idd Amin,Karudi baba mmoja na sikiri mimi masikini(hivi kwani ni sikiri au fikiri mimi masikini?),Azimio la Arusha...Ahlam UK
ReplyDeleteWengi wanakumbuka mengi kama vile tumbo niachie nimwachie madenge, ila maisha ya ulimwengu yamewashinda akili ya shule ukiwa nayo huku akili ya maisha huna ni upuuzi tu kwangu.Unapaswa umanage school na elimu dunia.
ReplyDeleteNdio kweli kabisaa...Wazanzibar ndio wanaonufaika na Muungano lakini wanaleta ...SITAKI NATAKA ...SIZITAKI MBICHI HIZI...ukiona Mzanzibar analalamikia Muungano ujue ajira tatizo hana pesa ana njaa...mfano Maalim Seif alikuwa mpinzani mkubwa wa Muungano je? sasa anaongelea kuvunja Muungano???... hapana ameona pana Maslahi!!!!!!
ReplyDeleteWimbo wa JKT:
ReplyDeleteIdd Amiini akifaa, mimi siwezi kulia,
Nitamtuupa Kageraa, awe chakuuula cha mambaa.....
Je mnaikumbuka pia ile hadithi:
Mama kanambia winga Kuku,
Nami siwezi kuwinga Kuku,
Nimekalia Kiteletele,
Mtama wa mama waliwa na ndege....
Idd Amin Jasusi, tena hili joka kuu, limefanya uvamizi kuiteka ardi yetu.
ReplyDeleteHatuna kazi nyingine ni kulifunza adabu ndipo litakapojua Tanzania ni ya watu.
Kwa kweli hatukutaka kuchezewa na shetani mengi tumevumilia dunia ina habari.
Katumwa na mabeberu kuja kutuangamiza, Idd amini malaya .. wa kwanza mwafrika........
Wadau hii imenikumbusha mbali sana!
ReplyDeleteSikiri mimi maskini, uvivu wangu nyumbani, ukiwa huu njiani nakufa hapa kwa nini,Sadiki sasa ashiba chakula kingi kwa baba,....Nimekosa baba na Mama nisameheni. Enzi za mafunzo tabiti kwa vijana, na hadithi ya sungura ikiwafunza kuwa madhubuti na kutochukulia vitu kama ni haki yao ya msingi badala yake ni kutokana na utendaji kazi...Naamini.AHERI ZAMANI...Mashairi ya saadani, Chonya of chilonwa me!! na mengi mengi yaiwafunza vijana stamina ya maisha... JKT ....Eee mola wetu tubariki tuelewe tuendako, ututoe katika kiza na utuwezeshe kuuthamini utamaduni wetu na mila na desturi zetu...Vinginevyo ndiyo mambo ya bwana Cameron kutuambia bila ya kukubali ushoga hakuna misaada.....INASIKITISHA
ReplyDeleteHuo wimbo wa Idd Amini umenichekesha sana, inaonyesha jinsi gani serikali ilikuwa inamuogopa hadi wakamtungia wimbo, Jamni siku hizi kuna mchakamchaka mashuleni? T'was very nice in those days we have to go to school 6am because of mchakamchaka. Ndo maana siku hizi watoto wanawaza tu mapenzi maana hakuna mazoezi
ReplyDeleteMchakamchaka utoke wapi wakati watoto wanakuja kwa school bus wawahi class
DeleteMimi sidhani kuwa shairi hili linawagusa wazanzibari musiwapige madongo ni haki yao ya msingi kama ilivyo kwa mimi,nyinyi na wengine kwalolote lile unalohisi unanyongwa. Kwani muungano huu ni wa ridha ya viongozi tu waanzilishi na unaenziwa kwakuwa tu mwalimu yumo na hatajwi kwa makosa yake.
ReplyDeleteMuundo wa muungano ndio zimwi likulalolisokwisha. kama zanzibar inafaidika ndio haki yake na kama wanakosewa ni haki yao kupiga kelele na kama hazisikilizwi basi hakuna lisilo na mwisho watafika na kufunguka kutoka katika dema liliundwa na mvuvi mwalimu.
kwamaoni yangu sungura huyu mjanjambile ni CHADEMA juu ya mchakato wa kutunga sheria ya katiba ambao waliulilia njaa na kupelekwa shambani wakashindwa vuna matunda yake kwa ubole wao wa kujitwisha ujanja pori wa kurukaruka.
Sikuzote ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu lakini mara hii sungura Mjanja hunasa mtegoni tena aliyeutega mwenyewe.
Mjomba usinibanie
hahaha na hapa mabata wadogo dogo wanaogolea katika shamba zuri la bostani duuu kweli ilikuwa raha zamani bila ya kusahau maua mazuri yanapendeza ukiyatizama ukayechekela hakuna mmoja asiyependeza zumm zummm ee mama nyukiliaa ee
ReplyDeleteOLD GOOD DAYS FOR REAL! HIVI NAWEZA KUPATA WATU HIVI VITABU VYA ENZI ZILE, PAMOJA NA CHA JUMA NA ROZA
ReplyDeleteAnonymous wa Fri Nov 18, 05:50 PM 2011
ReplyDeleteUHUSIANO WA WAZANZIBAR NA SHAIRI LA SIZITAKI MBICHI HIZI!
Umenifurahisha sana kwa vile sasa lengo la mshairi kutupa mistari limetimia!
Ninakukumbusha kuwa Mashairi,Methali,Nahau na vingine huwa na lugha za mafumbo na wakati mwingine hutoa maana kinyume nyume, au maana kwa misingi ya ulinganishi wa mambo halisi...MFANO WA SIZITAKI MBICHI HIZI ..NA MSIMAMO WA KI SIASA WA WAZANZIBAR...hii ndio sanaa ya ushairi bana!
Asante sana, ila wadau wamalizie tungo hizo za Karudi baba mmoja..
ReplyDeletena Azimio la Arusha pia Ninaye ndege mzuri hadi raha....
Hilo shairi msianze kuhusisha na siasa... Hiyo ni lugha iliyotumika kwa hadhira iliyokuwepo na wala siyo siasa kama wengine wanavyotaka tuamini
ReplyDeleteBABA ANA NG'OMBE
ReplyDeleteHuyu ni Baba,
Baba ana ng'ombe.
Ng'ombe wake ni mweusi
Baba anasema, kimbia ngo'mbe.
Kimbia upesi, Kimbia nyumbani.
Baba ananjaa.
Wiki ijayo tawaletea hadithi ya Juma na Roza ila mniambie kama hii mmeipenda na ijayo mnaihitaji!