Baadhi ya Wafanyabiashara na wakazi wa maeneo ya jirani na Soko kuu la Mji wa Tunduma jijini Mbeya wakishuhudia moto mkali uliokuwa unateketeza soko lao hilo leo.Moto huo ambao unadaiwa kuwa ulianza kidogo kidogo na baadae kuwa mkubwa kuanzaia majira ya saa 11 jioni ya leo.Taratibu za awali za kuuzima moto huo zilichukuliwa lakini hakukuwa na mafanikio yeyote na baadae walifika askari wa kikosi cha Zimamoto cha Mkoa mkoa wa Mbeya huku wakiwa na magari yao ambayo yalikuwa hayana maji,hali iliyofanya moto huo kuendelea kuteketeza soko hilo pamoja na mali zake.chanzo cha moto huo hakijajulikana mpaka hivi sasa.hivyo Ripota wa Globu ya Jamii ambaye yupo katika eneo la tukio anaendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. This is too much,tunashindwa kudhibiti moto,accident za barabarani,kweli Taifa lisilojiandaa kwa maafa linajiandaa kwa majanga.hii ni aibu kwa wilaya na serikali ya mkoa.

    ReplyDelete
  2. Mh Dk J. Kikwete, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa TANZANIA. Tunatoa shukrani za dhati kwa kuto kuweka sahihi katika makubaliano ya EAST AFRICAN COMMUNITY yanayohusu ARDHI, MALIASILI NA MALIGHAFI YETU WATANZANIA. Kwasababu watani zetu wanazimezea mate na SIKU MTAKAYOKUBALI NA HAYO MAFUTA YALIYOGUNDULIKA UGANDA na TANZANIA BASI SISI HATUNA CHETU BALI (UGOMVI NA VITA)...(KUNATIMU/KAMATI KABAMBE NA MABILLIONI YA DOLLAR KUTOKA NCHI JIRANI IMEPANGA MKAKATI WA HALI NA MALI)..!! TUNAKUSHUKURU NA SAMWELI SITTA !! VYAMA VYA UPINZANI HAKIKISHENI VIPENGELE VYA ARDHI, MALI ASILI NA MIPAKA YETU TANZANIA VIKO KATIKA KATIBA MPYA KAMA MALI YA WATANZANIA NASIO EAST AFRICA AU NCHI JIRANI. [MAFUTA NA MADINI WANAYATAFUTIA UGOMVI KILA KUKICHA ILI WAYAPATE KIURAHISI/BURE NA MIFANO TUNAYO] << KUMRADHI KWA KUTOKA NJE YA MADA >>

    ReplyDelete
  3. Mbona wanaendelea kumchokoza Rais wetu Mbeya, Mh.Sugu?

    ReplyDelete
  4. Kwanini moto unateketeza masoko ya mbeya tu? lazima kutakuwa na mkono wa mtu hapo uchunguzi ufanyike ijulikane ni kwanini moto unateketeza masoko ya mbeya kila mwezi????????? Hii inarudisha nyuma maendeleo ya watu kwani ninaamini watu wengi hawana insuarance ya mali zao. Kuna anayeuhujumu uchumi wa mkoa wa Mbeya achunguzwe.

    ReplyDelete
  5. Mangi wa KiboshoNovember 29, 2011

    Hilo la magari kufika bila maji nalo ni CHIBOKO!!! ni Vikorombwezo katika kusheherekea MIAKA 50 YA UHURU!! ahahaaaaa!! asalaleeeee

    ReplyDelete
  6. MTINDO WA MAAFA YA MOTO MARA KWA MARA KTK MASOKO YA MBEYA::::Hapa sio bure kuna taswira kama sio Siasa ni njia isiyo sahihi ya Hujuma kwa lengo maalum!

    Ikumbukwe kuwa gharama ya hujuma hizi itawafikia wao wenyewe Wadau wa masoko na Wakazi wa Mbeya kwa kuwaendekeza watu wachache.

    1.Wadau wa soko wenyewe watajihujumu kiuchumi kwa kukosesha wakazi huduma za bidhaa na Wadau wenyewe kukaa na njaa.

    2.Uimarikaji wa huduma za soko unaakisi hali yao wenyewe kiuchumi ,kwa kuwa itawagharimu wenyewe kuchangia upya ujenzi na kuchelewesha mwenendo wa soko kurudi ktk hali yake ya kawaida.

    3.Wadau wa soko na Wakazi wa Mbeya wakumbuke kuwa kujenga kuna ugumu kuliko kubomoa.

    4.Watafute njia sahihi za kufikia malengo na sio njia za namna hii.

    5.Siasa za Mbeya wastani kiujumla na za Arusha ni za mlengo wa chama kimoja fulani cha siasa, lakini kwa nini wenzenu Arusha hawaunguzi masoko yao kama ninyi Mbeya?

    6.Wanyalu,,,ebo mnajilostisha wenyewe halafu mnailalamikia serikali, huku mkijua hali ya kiuchumi duniani ni ngumu na masoko ndio ajira ya ukombozi mliyobaki nayo!!!.

    Hivi kwa nini masoko ya sehemu zingine nchini yasiungue ,inakuwa ni Mbeya tu???.

    ReplyDelete
  7. Mgonjwa anaweza kujihujumu mwenyewe kwa kutupa dawa za dozi uvunguni mwa kitanda...''Mbeya wanaugua ugonjwa wa itikadi''...ndio mazingira ya kuungua mara kwa mara kwa masoko ya Mbeya!

    ReplyDelete
  8. Next Watachomeana Moto Nyumba Zao Zote.

    ReplyDelete
  9. Inasikitisha Gari la zima moto linaenda kwenye tukio halima maji?au mwamndishi umekosea kuwakilisha habari hii?Kama ni kweli,basi NASHAWISHIKA KUSEMA WANAOCHOMA MASOKO NI WATUMISHI NA WAMEPEWA MAELEKEZO YOTE JINSI YA KUFANYA.Haiwezekani mtu aliyesomea kazi ya kuzima moto na kuapa na kupewa zana unaenda kuzima moto na gari halina maji??????KULIKONI??JE HII SIYO JINAI??

    ReplyDelete
  10. YAANI HIZI SIMU ZA MIKONONI SHUGHULI PEVU BADALA YA KUSAIDIA UOKOAJI KILA MTU ANA BONYA KUPATA TUKIO THEN UNAPELEKA WAPI NA NINA HAKIKA HUNA HATA CHETI CHA UANDISHI

    ReplyDelete
  11. MBEYA KUNANI???? INVYOELEKEA NI MKONO WA MTU HASA SIASA WANACHADEMA HAO SIJUI WATAWACHOOMEEA HADI NYUMBA HAO WAFUASI WA CHADEEMA KA MASHETANI WAMMEETUMWA HAPO SI BURE. CHADEEMA CHADEMA SIOO VIZURI MWAFANYA WENZENU KUWA MASKINI. ACHANEENI NA CHADEMA

    ReplyDelete
  12. CHADEMA:::MBEYA Hujuma sio mwendo wa kimaisha!!!.

    Hiyo siyo Siasa sahihi!

    Hayo masoko ndio machaka yenu ya kuponea kimaisha huku mkiona hali ya maisha na uchumi duniani ukidorora!

    Viongozi wenu wa Kitaifa walishaona Mabavu na Hujuma sio mwelekeo sahihi jana na juzi tu, ili kufikisha malengo kwa njia sahihi na kwa mafanikio na wametafuta kuonana na Raisi!

    ReplyDelete
  13. Kuungua kwa Masoko ya Mbeya.....imani za Kishirikiana, inasemekana pana aina ya Wafanyabiashara wanavuta nyota za bahati kwa kufuga majoka makubwa chini ya meza zao za biashara Sokoni ili kuvuta biashara na kuwa Chuma ulete kwa wengine, sasa wahanga wa kupigwa hiyo chuma ulete wanawasha moto kuangamiza majoka hayo...kalaga baho!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...