Kampuni ya Songas Limited, ambayo inamilikiwa na kampuni ya Globeleq,inayojihusisha na kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kutoka katika kisiwa cha gesi cha Songosongo kilichoko pwani ya Kusini mwa Tanzania, leo inakabidhi jengo moja lenye vyumba vya madarasa mawili pamoja na madawati yake 50 kwa shule ya msingi Ulongoni iliopo Ilala jijini Dar es Salaam. Hii ni sehemu ya huduma kwa jamii ya kampuni ya Songas.


Madarasa na madawati hayo yanakabidhiwa kwa Mstahiki Meya wa Ilala Mh. Jerry Silaa na Mratibu wa Mahusiano ya Jamii wa Songas Nicodemus Chipakapaka. Majengo haya yamegharimu dola za kimarekani elfu ishirini (US$20,000). Kila chumba kimepewa madawati 25.


Kampuni ya Songas ilianza rasmi kazi zake za operesheni mwaka 2004 na ni sehemu ya kampuni mama ya Globeleq Investment Fund, mfuko ambao huwekeza katika miradi ya umeme katika nchi zinazoenedela.


Songas ni mzalishaji wa nguvu za umeme kwa bei nafuu na uhakika. Umeme unaozalishwa na Songas unatoa zaidi ya asilimia 30 ya umeme wote unaozalishwa kwa mahitaji ya Tanzania na kwa hiyo kampuni ya Songas ni mmoja kati ya wadau muhimu katika kukuza na kuendeleza uchumi wa Tanzania. 


Songas ipo katika mchakato wa mwisho wa kupanua miundo mbinu yake ili iweze kusafirisha gesi zaidi kutoka Songosongo. Upanuzi huu utapelekea kwa kituo chake cha kusafisha na kusafirisha gesi Songosongo kusafirisha gesi mara mbili ya inayosafirisha sasa na kufikia 140MMscfd. Gesi hii itaweza kutumika kufulia umeme na mahitaji mengine ya gesi nchini.


Kwa sasa jumla ya vijiji 48 kutoka Kilwa mpaka Dar es Salaam hupata misaada kupitia mpango wa kuhudumia jamii wa Songas. 


Songas inajikita zaidi katika kusaidia kuleta maisha bora kwa watanzania hususan kwa wananchi maskini na wanaohitaji huduma kwa jamii.


Mchango wa Songas unalenga Zaidi katika kutoa huduma zake kwenye miradi endelevu ambayo ina lengo la kuondoa umasikini na kusaidia katika kuleta maisha bora kwa wananchi na kuwapatia vyanzo bora vya kufufua uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. sawa asnte kwa misaada yao lkn haya makampun yajaribu kwenda vijijin pia wanahitaj misaada tena hal nimbaya kuliko kawaida wasiogope umbali. mi ningesema shule za dar sasa zatosha. waende newala ,chunya huko . kwan nao ni watanzania wanahitaj elimu hawa watoto... any way masive thankx

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...