Mwanariadha mkongwe aliyewahi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa, Gidamis Shahanga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanzishwa kwa Taasisi ya Michezo ya Gidamis Shahanga (SSI) yenye lengo la kuinua michezo, hususani riadha, jana kwenye hoteli ya Courtyard Protea, Upanga jijini Dar es Salaam. Kulia ni mwanariadha wa zamani, John Haygahimo.
Gidamis Shahanga (katikati), mmoja wa wanariadha waliowahi kuiletea Tanzania medali katika michuano ya kimataifa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanzishwa kwa Taasisi ya Michezo ya Gidamis Shahanga (SSI) yenye lengo la kuinua michezo, hususani riadha, jana kwenye hoteli ya Courtyard Protea, Upanga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mmoja wa Wakurugenzi wa taasisi hiyo, Deusdedith Mayomba Duncana na kulia ni mwanariadha wa zamani, John Haygahimo.
Hivi, mbona wanariadha wa Tz huwa wana majina ya kiaina aina sana??? Mmeshtukia??? Kama kuna mtu ana orodha ya majina atuwekee hapa muone.
ReplyDeleteEndapo wewe una jina la kiaina aina na huna jobu cheki na riadha, au mwanao kama vipi muelekezee kwenye fani.
Mhe. Shahanga asante sana kwa habari ya kuazisha hii shughuli, labda utaiokoa Tanzania tupande juu kama majirani zetu Wakenya.
ReplyDeleteUkweli ni kwamba TAAA na TOC wameshindwa kufanya kitu, la maana pia kama wanaohusika wanasoma itabidi waachie ngazi uongozi.
Bado siku 250 hamsini tuu kabla ya ufunguzi wa michezo ya OLIMPIKI huko London lakini ukweli ni kwamba bado tumelala maana timu hatuna tunasubiri tujenge timu wakati zitakapobakia wiki mbili kabla ya michezo!!
Majina wa wanariadha waliopita ambao nawakumbuka ni kama hawa;
ReplyDeleteFilbert Sanka Bayi
Suleiman Mjaya Nyambui
Gidamis Shahanga
Alfredo Shahanga
John Haygaimo
Peter Mwita
Juma Ikangaa
Boay Akonay
Mossy Ali
Mwinga Mwanjala
Banuelia Mrashani
Simon Mrashani
John Bayo
Chris Malundi (marehemu)
Ali Nyonyi
Maxmillian Iranghe
Zakaria Gwandu
Zakaria Maleko
Simon Naali
Simon Robert,,,,,,,,,,,,,
Mwingine aendelee na orodha hii
Orodha ya wanariadha ...umewasahau wawili:
ReplyDelete1.Agapius Massong
2.Afande mmoja jina lake la mwanzo silikumbuki ila la mwisho la ukoo ni Isegwe.
Gidamus Shahanga,,,ahsante umefanya jitihada nzuri sana ni kuwa kwa sasa kimichezo inabidi tuangalie maeneo mengine kama hii Riadha, pia Ndondi kwa vile imejidhihirisha wazi kuwa ktk suala la ''soka'' gharama kubwa inatumika, mipango yetu haipo sawa na bado tunakanyaga tope!
ReplyDelete