Na Idara ya Habari Maelezo - Zanzibar
Ujumbe wa Wafanayabiashara kutoka Singapore ukiongozwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa nchi hiyo umewasili Zanzibar leo asubuhi kwa ziara ya siku moja.
Kwenye Uwanja wa ndege wakimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar ujumbe huo ulipokelewa na Naibu Waziri wa Biashara ,Viwanda na Masoko Zanzibar Thuweiba Kisaasi , Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Viwanda na Wakulima Zanzibar Mbarouk Omar pamoja na maofisa mbali mbali katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar.
Kwa mujibu wa Ratiba iliotolewa na Wizara ya Biashara ,Viwanda na Masoko Zanzibar , Ujumbe huo mchana huu utakuwa na mazungumzo na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd huko
Ofisini kwake Vuga.
Usiku Kwenye Hoteli ya Serena iliopo Mjini Zanzibar Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore ataelezea juu ya hali ya Biashara nchini mwao na baadae kutatolewa maelezo juu ya nafasi za Vitega Uchumi viliopo Hapa Zanzibar.
Aidha Kamisheni ya Utalii Zanzibar nayo itapata nafasi kuelezea juu ya nafasi ziliopo Zanzibar katika mambo ya utalii na baadae kuwa na Chakula cha Usiku pamoja na kuwa na mazungumzo na Wafanya biashara wa Zanzibar na Wanasiasa.
Ujumbe huo Wawafanyabiashara kutoka Singapore ukiongozwa naWaziri wa Biashara na Viwanda unatarajiwa kuondoka Zanzibar hapo kesho asubuhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...